Ijumaa, 8 Novemba 2024

URITHI wa Bibi 4

 Story : URITHI WA BIBI . EP.4


Author........... Steven Morgan


📞 : .............+255 659 115 223


Email : ................. stevennemes2k@gmail.com


Karibu tena ndugu msomaji katika mwendelezo wa story yetu. Tulipoishia ndipo tunapo anzia .


ILIPOISHIA.

Binti chuma na wenzake  wakiwa msituni waki hapishwa na mkuu wa wachawi.


Basi,mvua ikaendelea kunyesha na jua likaendelea kuwaka ,mara ghafla mvua ikakata na likabakia jua Kama mwanzo. Mkuu wa wachawi akatupongeza na kusema kua Sasa tunatakiwa  kuusumbua ulimwengu. Natumaini mtakua mawakala wazuri Sana wa shetani katika kuleta ubovu ulio kidhiri katika Dunia . Mbarikiwe Sana na lusifa ,na mkafanikiwe katika kutenda dhambi zenu zilizobarikiwa na shetani". 

 Mkuu alipomaliza kusema hayo Mimi nikajihisi mwenye nguvu Sana na nikajikuta naweza kufikiria na kufanya mambo makubwa bila ya kufundishwa. Macho yaliniwiva kama nyanya ya utunguja. Mkuu alinitazama Kisha akasema " Chuma ,wewe unaonekana kua na nguvu nyingi sana ,kafanye kazi ,jamii ikutambue na kukuogopa ,hakuna kiumbe atakae weza kukudondosha , ulimwengu ni wako chuma , chochote unaweza kufanya kuanzia Sasa,umesha pewa nguvu ya mamlaka!"  Hayo yalikua maneno ya mkuu akinisifu,baada ya hapo tukanyanyuka na kurudi nyumbani baada ya kuruhusiwa na mkuu.


                      ENDELEA.

Kwakua ilishafika jioni Sana ya saa kumi na mbili ,Mimi na bibi tulishilikiana kupika  chakula Cha jioni kwa haraka Kisha ilipofika saa mbili kamili usiku ,tukaandaa chakula na kuanza kula huku maongezi ya hapa na pale yakiendelea.

Siku ikaisha hatimaye asubuhi ikafikia ,Kama kawaida nikaamka na kufagia uwanja  ,nikaanda chai na maji ya Moto ya kuoga.  Bibi alipoamka alienda kuoga baada ya Mimi kumaliza. Baada ya hapo tukatandika mkeka wetu nje na kuketi kwa ajili ya kunywa chai. 

"Chuma mjukuu wangu,kwa Sasa umeshakua kamili tena una nguvu nyingi zaidi yangu. Sasa ni Wakati wako wa kutamba unavyo taka"

Natamba kivipi bibi?"  "Kwa nguvu ulizonazo unaweza ukafanya chochote na kupata chochote unachokitaka,kwa mfano Kama kuna mtu unamchukia unataka kumfanya vibaya awe kichaa au awe na mikosi au maradhi, unaweza fanya."  "Sawa Bibi hayo uyasemayo Kama yanawezekana nitayatenda maana kuna watu nawachukia Sana."  Hayo yalikua ni maongezi ya hapa na pale Kati ya Chuma na Bibi yake,  Chuma anaendelea kueleza ...tukiwa bado tupo pale nje tukinywa chai mara akaja mtu mmoja wa kiume ni mbaba kwakua alikua  ni mtu mzima . " Hodi hodi wenyewe hapa!!"  " Karibu " tukamjibu yule mbaba kwa pamoja. " Bila Shaka hapa ndio kwa bibi Mbokeleni au kwa bibi chuma?" Aliuliza yule mgeni tusie mfahamu. " Ndio bila Shaka umefika Mimi ndio Bibi Mbokeleni na huyu ndio mjukuu wangu Chuma" Bibi alimjibu yule mgeni. " Nashukuru kuwafahamu! Bila Shaka hamnifahamu ,Mimi naitwa Foya ni mwenyeji wa moshi lakini kwa Sasa makazi yangu naishi Dares salaam.Kuja hapa nimeelekezwa na ndugu yangu mmoja ambaye ni mwenyeji wa hapa Ndolelo anaitwa Bibi zubeda anaishi hapo ng'ambo ya pili" " aaah! Bibi zubeda namfahamu  vizuri,Sasa nambie shida yako ni nini?" Bibi alimjibu yule mgeni. " Shida yangu nilikua nahitaji binti wa kunifanyia kazi za ndani,nipo Mimi,mke wangu na wanangu wawili wadogo wa kike na wa kiume . Sasa nimeambiwa kua kuna binti anaitwa chuma unae hapa ,ndo maana nimekuja kukuomba Kama itawezekana niende nae dar es salaam akanifanyie kazi." Yule baba mgeni alijieleza Wakati huo wote Mimi nilikua nipo kimya nikisikilizia kinachoendelea Kati ya Bibi na yule mgeni. " Sasa wewe umetoka huko kote umepaona hapa ndio kwenye mfanyakazi?" " Nimekuja hapa kwakua nime elekezwa raha sivyo, nisinge fika,nisamehe lakini Kama nimefanya kosa kuja hapa"  " ha ha ha haaa! wewe huna kosa ila kosa analo aliekuelekeza kuja hapa!, Sasa je, utaweza kwenda kuishi na mjukuu wangu kweli huko dar es salaam?, " Bila Shaka Bibi ,Kama Chuma mwenyewe atakubari, basi hakuna kitakacho shindikana ,ataishi vizuri Sana atakua Kama yupo nyumbani"  " sawa ,Mimi Kama bibi na Kama ndio mzazi wa Chuma,sina neno tena labda tumsikia mwenyewe Chuma anasemaje kuhusu hilo? Maana nae pia ana maamuzi yakepia"  Bibi alimalizana na yule mgeni kisha bibi alinigeukia na kuniuliza ," Chuma nadhani umesikia mazungumzo yote hapa ,Sasa je,upo tayari kwenda dar es salaam kufanya kazi?  " Bibi Mimi bana  sitaki niende mbali nikuache wewe peke yako,siwezi kuishi mbali nawe"  " Chuma kumbuka wewe umeshajitambua na unaendelea kua mtu mzima ,kumbuka sasa unatakiwa kujitafutia maisha yako mwenyewe ,naamini ukifanikiwa unanikumbuka na Mimi Bibi yako kwa kuninunulia upande wa kitenge na kaniki na sukari utaniletea au we unasemaje?" Bibi alinig'ang'ania Sana Mimi kukubari kwenda kufanya kazi dar es salaam,sijui kwa nini! Lakini nahisi alikua na maana yake. " Sawa bibi kwakua wewe umekubari Mimi niende ,siwezi tena kupinga,niko tayari ila nataka nijui kwanza nitalipwa shilingi ngapi?

"Nashukuru Sana Bibi, pia nakushukuru Sana Chuma. Kwa kukubali kwendakufanya kazi kwangu, mshahara nitakulipa shilingi elfu kumi, na ukifanya kazi vizuri nitakuongeza!!"  Aliongea yule mgeni alie jitambulisha kwa jina la Foya ndugu na Bibi Zubeda. Basi kwa kua ilikua  asubuhi ya alhamisi ,bibi alimwambia  yule mzee Foya kua aje juma tatu kunichukua . Mzee Foya alifurahi Sana bila kujua kua anamkaribisha shetani alietoka depo. Alituaga Kisha akasema kua atakuja juma tatu asubuhi kunichukua na tutaianza safari asubuhi hiyo hiyo.

Bibi alifurahi Sana na akaniambia kua " Sasa Chuma huko unakokwenda ndio pa kujikomaza mjukuu wangu sawa?"  " Sawa bibi kwa Sasa huna haja ya kunielekeza najua nini cha kufanya. Watamjua chuma kua ni mtu wa aina gani!!


Story ................ URITHI WA BIBI EP. 4.B

Author..............Steven Morgan

📞..................... +255 659 115 223


Kwa mara nyingine tena bado tupo sehemu ya 4 ya story yetu ambapo tunaingia katika kipengele B ya sehemu ya 4. Kabla hatuja endelea katika kipengele B,ngoja tukumbushane kidogo yaliyopita katika kipengele Cha 4.A.


ILIPOISHIA,

Tumeona kua Bibi Mbokeleni au Bibi chuma amepata ugeni wa baba mmoja asubuhi na mapema ambaye alijitambulisha kwa jina la Foya . Mzee Foya alikua anahitaji mfanyakazi wa ndani ili aondoke nae Dares salaam ,ambako ndiko anako ishi yeye na  familia yake ,akiwemo mkewe na watoto wawili wadogo.Binti chuma ndio mlengwa anae hitajika kwenda huko dares salaam kufanya kazi. Kumbuka binti chuma siku si nyingi ametoka kufuzu depo la kichawi na kuhapishwa. Bibi yake amemruhusu chuma aende akafanye kazi. Mzee Foya ameambiwa aje juma tatu kumchukua binti chuma ili aondoke nae dar es salaam. 

 

ENDELEA.

Bibi alifurahi Sana Mimi kupata kazi ,japo Mimi sikupenda kua mbali na bibi yangu maana yeye ni Kama mzazi wangu alie bakia katika Dunia hii.

Lakini kwakua bibi ameridhia ,basi Mimi pia siwezi kumpinga kwani bibi alitaka na Mimi pia nijitafutie maisha yangu ili baadae nikifanikiwa ,nimsaidie na yeye.

 Kama wasemavyo waswahili kua usiku wa deni haukawii kucha,basi siku zilikwenda Sana na juma pili ikafika ,ambapo nilijiandaa vya kutosha,nilifungasha kila kilicho changu kwaajili ya safari ya dar es salaam. Usiku ukaingia,Bibi aliniita katika chumba chake Kisha akanipa kioo Cha pembe nne ,akaniambia nikitunze maisha yangu yote,na yeyote ninaye mtaka kumwona nimwite kwa jina lake nitamwona pale kwent kioo.

Ndugu msomaji,kioo kina maajabu mengi usiyo yajua ambayo unaweza ukafanya hata wewe ambae sio mchawi!! Nitakwambia hajabu moja wapo la kioo unacho jitazamiaga nyumbani kwako. Baadhi ya watu ukiingia vyumbani mwao,utakuta vioo vya kujitazamia ,vimefunikwa kwa nguo au boksi au karatasi kubwa na vitafunuliwa Wakati mtu anapotaka kujitazamia tu!!

Huwa wanavifunika kwa sababu,vioo hutumika Kama CCTV Camera ya wachawi,na huona na kusikia chochote mnacho ongea au kuteta mkiwa ndani huku vioo vya kujitazamia vikiwa wazi. Ndugu msomaji unashauriwa kufunika kioo chako Cha kujitazama na ukifunue pale unapotaka kukitumia tu!!, Kwani unapo viacha wazi muda wote ,wachawi watajua kila kitu kinacho endelea ndani mwako.

Hajabu lingine lakioo,nikwamba kwa kupitia kioo unaweza kumwita jini yeyote akaja na unaweza kuzungumza nae kwa kupitia kioo chako Cha kujitazama. Unacho takiwa kufanya hapa ,ni kuchukua kioo chako Cha ukubwa wa kutosha wa pembe nne Kisha jifungie ndani mwako,hakikisha hakuna kelele Kisha chukua kioo chako kiweke mbele ,mezani ,ukutani au Kama kipo kwenye dressing table yako ni vizuri zidi.simama mbele ya kioo chako Kisha kitazame kioo chako bila kubwenza kwa dakika kadhaa huku katika akili yako fikiria kua kuna jini au kiumbe Cha hajabu utamwona!! Kisha  taratibu utaanza kuona sura yako inabadirika na kua sura mbaya ya kutisha ,ukiona hari hiyo inajitokeza ,ujue jini ameshafika ,unachotakiwa kufanya Sasa ni kumwomba unachokitaka akutendee. Angalizo : usije ukafanya zoezi hili Kama wew ni mwoga ndugu msomaji,kwani inatisha mno. Na usije ukafanya zoezi hili usiku,ni hatari Sana.


Basi nikiwa bado nipo chumbani na Bibi huku nikikiweka kioo alicho nipa kwenye begi langu la kusafiria. Baada ya happy kwakua ilikua tayari ni usiku Sana ,tukatoka nje kichawi,yani tulitoka bila ya kufungua milango,moja kwa moja tulienda kwa Bibi zubeda ambae yule mgeni Foya ndipo alipo fikia,ilikua ni usiku Sana ,wote ndani walishalala fofofo, Mimi na Bibi tuliruka na kutua kwenye paa la nyumba la Bibi zubeda.Tulipotua juu ya bati,hapakua na kelele wala kishindo zaidi Kama aliekua ndani Kama hajalala basi anaweza akasikia Kama mchanga au vimawe mawe vinamiminika kwenye bati!! 

Ndugu msomaji ukisikia Hari hiyo,ujue wanga wamesha tua na Kama hujalala basi utalala kwa lazima .unachotakiwa kufanya baada ya kuona Hari hiyo ni kumwomba Mungu Sana akunusuru na ibirisi huyo.

Basi tukatua kwenye lile bati la bibi zubeda ,japo bati zake zili oza lakini hatuwezi kuanguka kwani tunakuaga wepesi sana . Tulimwaga madawa yetu ili asie lala kwa muda huo ,alale kwa lazima ili sisi tuendelee na kazi yetu.

Tulitazama kwa kupitia jicho la tatu la kichawi tulimwona yule bosi Foya anaye taka kesho juma tatu twende wote dares salaam amelala fofofo huku simu yake ya tachi ikiwa chini. Tulirukaruka huko juu ya bati huku tukiimba nyimbo za kichawi kwa sauti. Hata Kama hujalala huwezi kutusikia. zaidi, utahisi wimbo flani unao ufahamu ume play katika kichwa chako ,ukiona hivyo ujue wazee wa kiza wapo nje au ndani wanacheza na kuimba.   Basi tukacheza Sana Mimi na Bibi baadae  tukaingia ndani chumbani kwa yule mgeni Foya . Taa ilikua inawaka tukaizima  Kisha tukaanza kumsotea kwa makalio ,muda mwingine tulimjambia mdomoni akawa anashtuka na kukohoa  sana. Bibi aliniambia kua nimkalie tumboni kwa makalio yangu Kisha nimsotee sotee !! Nami nikafanya hivyo tena kwa haraka . Lakini ghafla yule mzee Foya alishtuka usingizini kwa haraka na akanikamata nikiwa palepale juu ya tumbo lake!!! Huwezi amini Bibi aliondoka na kuniacha nimekwama juu ya tumbo la mzee Foya ambae ni bosi wangu mtarajiwa  huku nikiwa uchi wa mnyama na makalio yangu makubwa yaliyojaziana minyama yakiwa juu ya tumbo la mzee Foya.

******* ***** ITAENDELEA ************

 JE,nini kitafuatia?

Mzee Foya atamtambua binti Chuma?

Je,safari ya dar es salaam ipo?

 Hayo na mengine mengi utayajua katika sehemu ya EP. 5 ya URITHI WA BIBI


USISAHAU KU LIKE , COMMEnt


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni