STORY : URITHI WA BIBI . Ep.1
AUTHOR : STEVEN MORGAN
EMAIL : stevennemes2k@gmail.com
PHONE : +255659115223
Habari zenu! Bila Shaka mu wazima wa afya! Ndugu msomaji , karibu sana kwenye story hii nzuri yenye kufundisha na kusisimua . Utayajua mambo mengi usiyoyajua au unayo yasikiaga kupitia story hii.
Kwa jina naitwa chuma mashaka, naishi na bibi yangu kwa Sasa. Katika Kijiji Cha ndolelo kinacho patikana katika safu ya milima ya ulugulu.
Wazazi wangu baba na mama sikuwahi kuwaona kwani inasemekana ,walifariki Mimi ningari mdogo sana.
Mimi ni binti wa miaka kumi na tano kwa Sasa,naitwa chuma kwa sababu hilo ni jina lenye asili ya kabila ya kilugulu. Yani Kama nitamzaa mtoto wa kike basi angeitwa mwenda au Kama nitamzaa wa kiume basi angeitwa mkude. Yani huo ni mtiririko tu wa majina ya kilugulu.
Kijiji Cha ndolelo ndiko ninapoishi na bibi kwa sasa. Ndolelo ni jina lililotokana na tabia za kinamama wa zamani walipokua wanakwenda kuuza biashara zao sokoni,na wanaporudi kutoka sokoni,watoto zao wakiwa nyumbani wanatazama chini bondeni kabisa wanatazamia Kama mama zao wanarudi kutoka sokoni ,Sasa ile sehemu ambayo mama zao au Bibi zao walikua wakikatiza na kuonekana ndio mpaka leo inaitwa ndolelo yani kwa tafsiri ya haraka ni sehemu ya kuonea/tazamia/angalizia.
Bibi yangu anajulikana kwa jina maarufu la Bibi mbokeleni, huku neno mbokeleni likiwa na maana ya mpokeeni/nipokeeni. Aliitwa hivyo kwa sababu kila anapobeba mzigo wake huwezi kumpita ,ni lazima umpokee mzigo wake na kuupelaka mpaka kwake ,hata Kama ulikua huna nia hiyo! Sijui kwa nini lakini kiukweli Bibi yangu aliheshimika na kuogopeka sana na watu.
Siku moja Bibi yangu aliniita tukiwa nyumbani "we chuma" bee bibi,nilimjibu Bibi Kisha nilitoka nje kumsikiliza . " Njoo kaa hapa kwenye mkeka nina mazungumzo muhimu sana na wewe" "mh!" Nilishtuka kidogo baada ya kusikia kua bibi ana mazungumzo muhimu na Mimi! Sikuhisi kua huenda yakawa mazungumzo yapi! Hivyo,niliamua kuketi kwenye mkeka ili nimsikilize bibi yangu.
"Chuma mjukuu wangu sasa umekua na unajitambua sana.wewe ni mjukuu wangu wa pekee Sina mwingine.kwa Sasa Mimi tayari ni mzee sana ,Sina nguvu tena Kama zamani hivyo, natumaini wewe ndio mtu pekee wa kunipokea mizigo yangu!"
Mizigo gani bibi? Nilimuuliza bibi nikiwa nataka kujua kua ni mizigo ipi anayotaka kupokewa. " Usiwe na haraka chuma! Hivi si unakumbuka jinsi watu walivyokua wakiniheshimu!,na mashamba yangu watu wakiyaogopa ? Mpaka ndizi zinaivia juu lakini haziibwi?" Ndio Bibi nakumbuka sana na mpaka Sasa bado nalijua hilo kua watu wanakuheshimu mpaka wanakuogopa! Nilimjibu Bibi Kisha bibi akaniwahi kwa kuniuliza " unajua ni kwa nini ,watu wananiheshimu na kuniogopa Mimi na mari zangu?" "Hapana Bibi sijui!" Nilimjibu kwa haraka. "Je,na wewe unapenda uje kuheshimika na kuogopwa wewe na mari zako?" Ndio Bibi napenda kuheshimika lakini sipendi kuogopwa maana nitakosa marafiki! Nilimjibu Bibi huku nikiwa sijui dhumuni la Bibi kwangu! "Hahahaha, hahahaha!" Alicheka sana Bibi baada ya kumjibu hivyo! " Chuma wewe ndio chuma changu ninacho kitegemea kwa Sasa na baadae, hivyo sitaki uniangushe , kuna kazi nataka nikuachie,ni ngumu lakini ni nyepesi nikikufundisha.Wakubwa wamekuchagua wewe ,kuna mizigo nataka unipokee,ni mizito lakini ni myepesi ukisha ibeba.Utaheshimika sana ,utafanya lolote unalolitaka duniani." " Sawa Bibi nimekuelewa lakini hao wakubwa walio nichagua ndio akina nani?" Nilikubali Kisha nikamuuliza Bibi. " Wakubwa ni viongozi wetu, huwezi kuwaona mpaka na wewe uwe mwanachama." " Mwanachama?" "Ndio ,bila kua mshirka huwezi kuwaona wakubwa,usiwe na haraka muda si mrefu utawajua tu,hebu nenda kapike kwanza maana Mimi njaa imeshaanza kuniuma ." Alinijibu hivyo Bibi Kisha Mimi nikanyanyuka kwenye mkeka na kwenda jikoni kupika.
Nikiwa jikoni kwenye kibanda kidogo Cha miti kilichoezekwa kwa vipande vya mabati ya madebe,bibi akaja nae akaketi pembeni kwenye kigoda au kiti Cha miguu mitatu. Niliendelea kupika huku bibi akiendelea kuzungumza . Alizungumza mambo mengi sana mpaka mwishoni nikahisi kabisa kua huenda Bibi akawa ni mchawi japo sikuwahi kumshuhudia lakini nasikiaga tetesi mtaani kua bibi ni mchawi. Na ndio maana na Mimi pia mtaani watu wazima na watoto wenzangu pia hua wananiogopa kwani hata nikiwakosea hua hawaniadhibu Kama watoto wengine wanavyo adhibiwa!!
Chakula kiliwiva nikatenga kila kitu na tukala palepale jikoni . " Inamaana we chuma unataka kuniambia kua hujawahi kusikia tetesi zozote kuhusu Mimi huko mtaani?" "Nasikiaga bibi " , " mbona huniambiagi Sasa ! Unachokisikiaga huko?" " Hapana bibi sikuambiagi kwa sababu ninacho kisikiaga ni kibaya sana lakini pia hua siamini kile ninachokisikiaga kwa watu!!" Bibi aliendelea kuniuliza , "Sasa niambie unasikiaga nini kwa watu wakisema kuhusu Mimi?" " Watu huwa wanasema kua wewe ni mchawi,lakini Mimi siamini !!" Nilimjibu Bibi bila woga Kisha bibi akasema " unajua watu wanachukulia Kama uchawi ni kitu hatari sana kuliko kitu kingine,lakini kiukweli uchawi ni kinga na ulinzi Kama ulinzi mwingine.Anaye shika panga au bunduki au bomu ujue anataka kujilinda.Na anayeshika uchawi pia huyu nae hana tofauti na aliye shika bunduki au panga .labda uchawi huenda ukawa na nguvu nyingi kuliko panga au bunduki ndomana unaogopeka na watu" "mjukuu wangu usiku wa leo nataka nikuoneshe jinsi uchawi ulivyo ili usije ukauogopa sawa chuma?" "Ndio Bibi !!" Niliitikia kwa woga kwani kwa maongezi ya Bibi tu,tayari nimeshaanza kumwogopa.
Kiza kilishamili, ilikua ni usiku wa saa mbili.Bibi aliniambia tuingie ndani ili anioneshe huo uchawi unao zungumzwa.
Nilikua na hamu kubwa sana ya kuuona huo uchawi ukoje! Tukaingia ndani ndani kabisa kwenye chumba Cha Bibi .Bibi alitoa kapo kubwa mvunguni mwake likiwa limejaa tunguli /vibuyu mbalimbali na madawa mengi ya miti shamba.Niliogopa sana lakini ilinibidi nivumilie kile ninacho kiona.
"Chuma ,Mimi ndio Bibi mbokeleni,Sasa si unaliona hili kapo? " Ndio Bibi,naliona. Nilimjibu Bibi kwa woga. " Hivi vitu unavyoviona kwenye hii kapo ndio vifaa vya uchawi ila uchawi ni maneno yako mwenyewe!, Huu muda ni saa mbili usiku,bado mapema sana ila ndio muda pekee ya wachawi kujiandaa kwa shughuri zao za kiwanga na kichawi.maandalizi yanafanyika muda huu Kisha kuanzia saa sita za usiku ndio cheketu zinapoanza japo unaweza kucheketua muda wowote lakini mida hiyo niliyokwambia ndio mizuri!" Duh! Bibi aliongea maneno ya kutisha sana ambayo sikuwahi kuyasikia. " Chuma hebu shika hiki kibuyu" nikakishika kibuyu Kisha Bibi akachukua kibuyu kingine kwenye lile kapo Kisha akasema maneno kwa sauti kubwa mpaka niliogopa!! " Wakubwa!, wakubwa,chuma amekua Sasa na leo ndio ile siku ambayo tuliyokua tunaisubiri kwa hamu ,tumkabidhi mizigo yake mapema!!" Bibi aliongea kwa sauti kubwa mpaka nikamwambia " Bibi punguza sauti watu watatusikia huko nje " " chuma kuanzia Leo ujue kua mchawi hua anong'oni,ukisha vaa vazi lako la kichawi hutakiwi kuongea taratibu kwani kila mtu atakusikia,unatakiwa kuongea kwa sauti kubwa na hata ukicheka ,cheka kwa sauti kubwa ukiwa ndani ya vazi la kichawi tu!!"
Bibi alinipa Siri hiyo Kisha akaendelea kuchanganya madawa na akanipaka usoni nikawa Kama kinyago Cha mpapule! Akachukua kile kibuyu alichokishika Kisha akaniamuru niasame mdomo ,nilitaka kukataa lakini nikajikuta nafanya hivyo bila ubishi. Akanimiminia kitu Kama majimaji ya asali mdomoni kutoka kwenye kile kibuyu .Nasema asali sababu ilikua tamu sana . Akanichanja chale na nyembe mwilini kisha akachukua dawa ya unga kwenye lile kapo,aknipaka mwilini,muda huo nipo uchi kabisa wa mnyama. Ila nilipomtazama Bibi ,nilimuona amevaa kipande Cha kaniki kiunoni ,huku mwili wake ukiwa umegubikwa na madawa ya ungaunga yani nae alionekana Kama kinyago Cha mpapule ila kinachotisha sana.
Baada ya hapo ,bibi alisema kua maandalizi yamekamilika na hapo tayari tumeshavaa mavazi ya kichawi. " Bibi mbona wewe umevaa, warau hiyo kaniki mbona Mimi nipo uchi kabisa ?" Nilimuuliza bibi.." hata Mimi pia nakuona wewe umevaa kaniki na mimi pia najiona niko uchi!! Kiukweli hapa tuko uchi kabisa ila mtu yeyote akibahatika kutuona ,basi atatuona Kama tumevaa kaniki kumbe tuko uchi kabisa." Bibi akatoa mifagio miwili ,mmoja ule wa ndani uliotengenezwa kwa kindu,na mwingine wa nje ulitengenezwa kwa mti mrefu na njerewa za mikuti ya mnazi. Kisha akaleta na ungo unaotumikaga sana kupepetea nafaka. Vitu hivyo vyote alivitoa mvunguni kwake japo kwa miaka mingi sikuwahi kuviona na wala sionagi chochote .
Baada ya hapo akaniambia.." unaviona hivi vitu? Mifagio na ungo! Hivi vitu ni aina za usafiri tunao utumia katika shughuri zetu,huu mfagio mdogo wa ndani hutumika kwa safari fupifupi za ndani ya mkoa.Na huu ungo hutumika kwa safari ndefundefu za ndani ya nchi,yani mkoa mpaka mkoa .Na huu mfagio mkubwa wa mti ,huu hutumika kwa safari za masafa marefu ya nje ya nchi,iwe ulaya au popote pale japo hata ungo pia hutumika kwa masafa marefu ya ndani na nje ya nchi."
Duh! Usiku huo Bibi alinifundisha mambo mengi sana .
" Sasa mjukuu wangu chuma umeshakua chuma,Sasa kilichobakia ni vitendo tu!" " Kama nilivyo kwambia kua sehemu kubwa ya uchawi ni maneno yako mwenyewe,Sasa ukisha vaa vazi la uchawi unaweza kuongea chochote na kikawa Kama unavyotaka" alizidi kuongea Bibi. " Sawa Bibi lakini mambo hayo yanawezekana vipi?" Nilimuuliza bibi.." unataka kujua ngoja nikuoneshe!, Hebu tazama kwenye kiganja changu ,Sasa hivi namuamuru zefania atokee hapa kwenye kiganja changu ,na iwe hivyo!!" Duh! Huwezi amini kweli aliyoyasema Bibi ndivyo ilivyokua ,nilimuona mmama mmoja aliye muita kwa jina la zefania akiwa amesimama juu ya kiganja Cha Bibi!!.
" Usijari chuma muda si mrefu utayajua yote haya" na usiku wa leo nitakufundisha kuendesha hizi aina zote za ndege za kichawi na kuwasumbua watu majumbani mwao." " Sawa Bibi lakini ni kwanini tuwasumbue watu bila kosa?" " HataMimi sipendi watu wasumbuliwe lakini kazi zetu ndizo zinaitaji ufanye hivyo kwani kwa kufanya hivyo ,unakua na nguvu nyingi sana ,kinyume na hapo,utakua dhaifu sana." Basi kwakua muda ulisha kwenda sana ,bibi mbokeleni akachukua ungo Kisha tukatoka nje na kuelekea njia ya panda, tulitembea bila kuonekana na yeyote ila mbwa walitubwekea sana tulipokatiza kwenye nyumba zenye mbwa,niliogopa sana lakini Bibi aliniondoa hofu . Tukafika kwenye njia panda nne ( 4ways cross road) tukasimama katikati ya njia nne ,Bibi aliweka ule ungo pale chini Kisha akachota vumbi la ile njia ya panda akaweka kwenye ule ungo Kisha ghafla kikatokea kichwa Cha mtu ambaye macho yake yakiwa yanatazama ,akakiweka kwenye ungo Kisha akanyosha mkono wake juu na akaita aina flani ya dawa ikaja palepale mkononi,niliogopa sana ilinibidi nimuulize.." Bibi vitu hivyo vinatoka wapi?" "Hahahaha!, Chuma umeshakua subiri uyaone, mjukuu wangu chuma uchawi una mambo mengi sana,yani Kama ungekua unafundishwa daraeani elimu hii,usingeweza kushika kila kitu kichwani!, Hivi vitu nilivieka mbali sana na vipo vingi sana siwezi kuvibeba na kutembea navyo,hivyo popote ninapokua ,ninachokihitaji ,nakiita kwa kukiamuru kwa imani kali ,kinakuja mpaka nilipo haina haja ya kubeba furushi kubwa la mzigo utachoka chuma,haa haa haha haaa haaahaaaa!" Alimalizia kwa kusema hivyo bibi, Kisha akacheka sana mpaka nikaingiwa woga. Basi baada ya hapo kile kichwa baada ya kuwekwa juu ya ule ungo na kumimina baaadhi ya dawa za ungaunga na damu ,Bibi aliongea maneno akiamuru ule ungo utanuke uwe mkubwa was kuenea watu wawili,ikawa hivyo !nikapanda juu ya ule ungo baada ya kuambiwa na Bibi ,Kisha Bibi nae alipanda na kunifundisha maneno fulani ya kiufundi,baada ya kumuelewa ghafla ungo ukaanza kunyanyuka na kwenda juu ya anga. " Bibi mbona Sasa usafiri huu hauna usukano?" (Staring wheel) nilimuuliza bibi baada ya kuona kua kile chombo kinakwenda hukuu sisi tukiwa tumetulia . " Hiki chombo mjukuu wangu msukano wake ni akili yako yani vile unavyo waza wewe ndivo chenyewe kinavyotenda kwa mfano hapa Mimi na waza kuzunguka zunguka kwenye mawingu tu ,Kama unavyoona nacho kina fanya hivyo na nikiwaza kutua au kurudi nyumbani ,mara moja kwa haraka kinanirudisha, hata na wewe mwenyewe siku ukiwa peke yako fuatisha Kama ninavyo fanya sawa?" " Sawa bibi, " nilimjibu Kisha nikakaa kimya , tuliendelea kuyakata mawingu,Kisha Bibi akakiamuru kile kifaa watu hukiitaga kibeku kitupeleke kwa haraka nchi jirani ya Kenya mjini Nairobi.
Sijui nini kilitokea lakini nilihisi upepo mkari ukinipuliza kwa kasi mpaka nikahisi kufakufa!! Ghafla tukajikuta tunatua mjini Nairobi ,tulitua kwenye njia panda moja ambayo Bibi si mara yake ya kwanza kufika hapo,maana alionekana kuijua mitaa vizuri Sana. " Usijari chuma nataka nikutembeze mitaa yote ya Nairobi kwa muda mchache Kisha turudi nyumbani si utafurahi?". " Ndio bibi nitafurahi sana" nilimjibu Bibi huku nikiwa na furaha moyoni. Tulipumzika kidogo Kisha bibi na Mimi tukapanda chombo chetu ,na kuanza kukatiza mitaa,huwezi amini sijui ilikuaje lakini tukajikuta tunatikisika Kama vile tunatingishwa mara ghafla chombo kimeenda mlama tukajikuta tupo chini kwenye uwanja mkubwa wa jengo la kanisa la kiroho. " Mama wewee! mjukuu wangu umekwisha ,Sina jinsi lakini unisamee" Bibi aliongea hivyo,sikumuelewa lakini nilikuja kumuelewa baadae, nikataka kumuuliza kitu Bibi kua mbona tumekwama pale inakuwaje? Lakini Bibi kabla hajajibu ,akapaa angani juu sana na kupotea Kisha nikasikia sauti masikioni mwangu ikiniambia kua kesho asubuhi ikifika nilale kifudifudi ili nipate msaada ,zaidi ya hapo nitaumbuka.Nikawa Sina Cha kufanya ikabibi nibakie pale Mimi nikiwa uchi na ungo wangu .Sijui Cha kufanya nikangoja asubuhi ifike ili zijulikane mbivu na mbichi. ........... ....... ......................
*********** ITAENDELEA ************
Je,nini kitamkuta binti chuma baada ya kuachwa na Bibi kwa mzee kenyata kwenye uwanja wa kanisa la upako wa kiroho? Je, bibi amekwenda wapi? Usikose sehemu ya pili ya URITHI WA BIBI,. Uhondo ndio kwanza unakorea. Fanya ku like page , share na wengine wapate kuburudika na kuelimika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni