Ijumaa, 8 Novemba 2024

URITHI wa Bibi 15

 Story... URITHI WA BIBI EP.15. Mwisho.

Mtunzi....Steven Morgan

📲......... 0659115223


Naam kwa Mara nyingine tena ndugu msomaji tumekutana tena katika kufunga ukurasa wa mwisho wa story yetu ya URITHI WA BIBI.  Wacha tumalizie story yetu kabla hatujaanza kigongo kingine.


Kama kawaida pale tulipoishia ndipo tunapo anzia.


Ilipoishia ep.14

Chuma msalaba huu wa kulipiza kisasi Cha Bibi yako utakua peke yako mwenyewe,sitaki uwaponze wengine kwaajiri ya nafsi yako.Jipange vya kutosha Kisha Anza kumdondosha mganga Alumbile Kalumba Kisha mmalizie mzee Foya ,sawa?"


Mkuu alinisisitizia.

"Sawa mkuu" 

Nilimjibu.


"Basi Kama tume elewana kila mtu atoweke mahara hapa Mara moja na muende mkaendelee na shughuri zenu nyumbani."


Mkuu alituruhusu Kisha kila mtu alitoweka kwa stahili yake,kurudi nyumbani. Wengine walitoweka Kama radi,wengine walitoweka Kama upepo ,Yani zilikua ni mbwembwe tu za kichawi katika kuonesha uwezo.


 ENDELEA...

Basi Mimi nilirudi nyumbani ,nilipofika sikua na chakufanya zaidi ya kuniweka Safi katika hari ya kiubinadamu kamili.Nilikaa na kuwaza Sana kwamba ni kwa namna gani nitaweza kumuangusha mganga Alumbile Kalumba!!

Siku hiyo sikupata usingizi kabisa .


Wazo likanijia , nikachukua kioo alicho niachiaga bibi Kisha nikapiga ndumba nikiwa nimerudi Sasa kwenye hari ya kikazi. Alitokea palepale yule mganga kwenye kioo. Alikua ni mtu wa makamo kidogo. Nilimwangalia kwa makini nikagundua kua yule alikua si mganga wa mchezo mchezo.


Nikaamua kulitengeneza pembe ili nimtume aende akamchunguze yule mganga. 

Ndugu msomaji bila Shaka katika jamii yako iliyo kuzunguuka ,ulishawahi kusikia kua flani ni mchawi na ana miliki  mapembe .

Je,unajua pembe ama mapembe ni nini katika imani za kichawi?

Najua wengine mnafahamu vizuri zaidi yangu ila wengine pia hawajui kabisa kua pembe ni nini!!!

Kwa tafsiri nyepesi kwa mtu asiye fahamu ,atakwambia kua pembe ni,kitu chenye mfano wa pembe za ng'ombe ,au unapozungumzia habari za mapembe unazungumzia mapembe ya wanyama .


Wenye mawazo hayo,wako sahihi kwa uelewa wao lakini, katika imani za kichawi pembe ni jina tu ila halifananii hata kidogo na pembe ya mnyama.


Ndugu msomaji,niliposema kua nilitengeneza pembe na kumtuma akamchunguze yule mganga,unaweza ukajiuliza kua ,pembe ni kiumbe wa namna gani na anatengenezwaje?


Ndugu msomaji pembe hutengenezwa kwa kutumia Mara nyingi Midori ya kuchezea watoto. Mdori huo hufanyiwa ndumba za kichawi na kua kiumbe chenye uhai Kama mtu kamili akiwa kwenye kimo kilekile Cha mdori.Lakini pia pembe huyo anakua na uwezo wa kubadirika kua kiumbe mwingine yeyote yule mfano;

Pembe anaweza akabadirika kua panya na akaja kwako kufanya Lile alilotumwa Kama kubukua unga wa ugali au Mchele. Ndugu msomaji labda ulikua ukidhani kuwa watu wabaya huwa wanabukua pesa tu peke yake. Hapana watu wabaya huwa wanabukua hata mazao yanapokua shambani au nyumbani.

Wakati mwingine ndugu msomaji umeshawahi kusikia au kuona panya wanasumbua Sana ndani ya nyumba na unapoweka sumu ,wapo watakao kufa lakini,Kuna wengine wasumbufu zaidi bado wataendelea kusumbua hata ukiweka tena sumu kwenye chakula,watakila mpaka watasafisha lakini hawafi!! Ukiona hivyo panya hao sio wa kawaida bali ni mapembe. Kua makini na vyakula vyako ndani, maana Kama ulinunua kilo 20 za unga na kilo 30 za Mchele,ujue mtakula wote yaani utakuja kushangaa vyakula hivyo vitakuja kuisha muda usio utarajia. Kama uritarajia kua msosi wako utakaa wiki mbili,ujue utashangaa ndani ya wiki na siku mbili msosi umekatika.


Pia pembe,ana uwezo wa kujigeuza paka au nyau ,na hutumwa kazi mbalimbali Kama za upelelezi ,Yani wakati mwingine mnaweza mkakaa sehemu mkawa mnapiga story,lakini baadae akatokea paka na kuketi karibu yenu,nyie bila kujua mnaanza kuteta kua flani mbaya Sana na yule jirani yetu nae ni mtu mbaya Sana.Kumbe yule paka ni pembe atawasikiliza mwanzo mwisho na atarekodi kila kitu na kupeleka ujumbe huo kwa aliye mtuma.


Ndugu msomaji ngoja turudi kwenye story yetu,basi nilitengeneza yule pembe na kumtuma kwa yule mganga akachunguze ulinzi wake ukoje kabla sijaenda Mimi moja kwa moja.


Nilikaa na kutulia ,nilikua nikisubili pembe alete majibu sahihi. Ndugu msomaji kumbuka pembe ni Kama kifaa kinacho tumwa na opareta wake alikua ni Mimi. 

Na akipatwa na tatizo lolote ni lazima nijue hata Kama nipo mbali nae .


Haisee! Muda mchache baadae ,nilihisi kichwa kuuma Sana baadae mwili mzima ulikua na maumivu. Hii ilikua ni ishara tosha kua pembe wangu amehangamizwa !!


Baadae alirudi pembe wangu akiwa tayari mfu au kifaa kisicho faa tena. 

"Mh! Inaonekana huyu mganga si wa mchezo." Nilijisemea moyoni  Kisha nikaamua kulala maana ilikua ni Usiku Sana na siku hiyo sikua na hamu hata ya kwenda kuwanga.

Asubuhi ikafika nikaamka mapema Kama kawaida ,nikaoga Kisha nikawa naendelea na shughuri zangu za nyumbani za kawaida.


Nilipomaliza shughuri zangu zote za kufua na kujipikilisha, nikala Kisha nikajifungia ndani ,niakaanza kuandaa mkakati mzito wa kumshinda yule mganga. Mbinu niliyoitumia kuandaa bomu zito lenye kafara nzito ya manuizi yaliyoambatana na kufunga kwa siku 30.

Baada ya kuandaa lile bomu ,nikaliweka na ili lile bomu lipate nguvu zaidi ni lazima nijinyime Yani nifunge kwa siku 30.


Ndugu msomaji hakuna rahana kubwa Kama kumrahani mtu kwa maneno na kwa kufunga haswa kwa mtu ambae sio mchawi ,akifanyiwa mabaya ,Kisha yeye akaamua kumwomba Mungu kwa kufunga ili, Mungu amripize mbaya wake ,haisee dua hii ya maombi na kufunga ni hatari Sana.


Haswa kwa wewe ambae sio mchawi ,unaweza ukamrahani mbaya wako kwa kufunga siku 30 na kumnuizia maneno mabaya kila siku. Mfano wa maneno ya rahana ya kumnenea mbaya wako kila siku yanapatikana katika BIBLIA TAKATIFU  katika kitabu Cha ZABURI ya 109: 1- ........


Ila kwa sisi wachawi,kwetu ni tofauti huwa hatutumii biblia sababu inatudhuru,na wakati mwingine dua zetu huwa zinagoma pia.


Basi,siku zilizidi kwenda na hatimae ikafika siku ya ishirini na tisa. Nikajiandaa vya kutosha ili kesho yake mapema niende nikamlipue mganga Alumbile Kalumba. Niliamini kabisa kua nitashinda vita hiii,japo nilijua kua naenda kupambana na mtu hatari lakini nilijiamini na kujipa moyo.


Usiku ukafikia giza lilitawala kila kona.kama ilivyo kawaida,Usiku wa deni haukawii kucha. Kulikucha hasubui na mapema siku ya 30 ya mfungo wangu,nikajiandaa kichawi na kubeba kila aina ya dawa. Nikacheki kwenye rada yangu na kuona kua mazingira yanaruhusu kuondoka. Nikapotea Kama mware wa radi. Fyaaaaaaaaaa!!!!!


Nikaenda kuibukia nje ya nyumba ya yule mganga Alumbile Kalumba. Nikawa naangaza macho huku na kule kutazama usalama . Lakini kabla sijafanya chochote ,nikasikia sauti ya kiume ikinikaribisha ,kwa kua mbele sikuona mtu,nikageuka nyuma kutazama Kama kutakua na yeyote.lakini nyuma pia sikuona mtu.! Lakini pia ile narudisha shingo mbele ,nakutana uso kwa uso na Mganga Alumbile Kalumba akiwa na uso wa mnyama mbogo.


"Haa haa haaaa hahaha!"

Mganga alicheka Sana Mimi nikiwa namtazama.

" Karibu Sana Chuma, ujio wako ni Kama marehemu Bibi yako alivyo nijiaga. Na mwisho alifia hapa hapa. Wewe ni binti mdogo Sana halafu pia ni mzuri Sana ,hakika unafaa kua hata mke wangu. Hahaha hahaha!"


"Usinichekee mjinga wewe! Sikuja kwa masihara hapa ,leo ndio mwisho wako babangu huna pa kutokea."


"Chuma wacha kujidanganya na hako kasiraha chako ulicho kihandaa,huwezi kunihangamiza Mimi kirahisi hivyo! Bibi yako alishindwa akapotea na mama yako mkenya alishindwa akapotea. Sasa wewe bado mdogo Sana harafu ni mrembo Sana, hutakiwi kupotea na utamu wako. Cha msingi wacha hiyo tabia ya uchawi Kisha nikuoe tuishi maisha mazuri ya kiganga ."


Mganga alikua akiongea huku akinitamani maana nilikua uchi kabisa hivyo aliniona mwili na shepu na utupu wangu wote. Sijisifii lakini kiukweli nilikua Niko vizuri kwenye shepu japo sura si Sana. Yule mganga hakua na mke ndo maana ananirubuni lakini Mimi sikua na masihara hayo kwani nilienda kikazi kwani nilishafunga siku30 kwa ajili yake.


"We mbwa sikiliza Sina muda wa kupoteza,kabla hakujapambazuka vizuri,ngoja nikuoneshe."


" Hapana Chuma usifanye hiko unachotaka  kukifanya ,ni hatari Sana kwako nami napenda uishi I'll uwe wangu."


Mganga aliendelea kuongea lakini Mimi sikutaka kupoteza muda tena, nikamrushia kombora zito ,nililo liandaa . Mganga alilia Sana baada ya kukutana na pigo zito la mauaji. Alianguka chini na kupoteza fahamu.

Nikajua kua nimesha maliza kazi ,nikawa namsogelea ili kumkagua, lakini kilichonikuta baada ya kufika pale alipoanguka ilikua ni hatari zaidi kwangu.


Nilimkaribia pale alipoanguka nikainama ili nimguse au nimtingishe nione Kama ata amka. Nikamtingisha mwili wake,ghafla aka amka kwa kucheka Sana  mpaka nikahisi woga lakini pia nilijishangaa maana sikua na uwezo wa kufanya chochote kile. Niligundua kua hata miguu yangu ilishindwa kunyanyuka kabisa. Sikua na ujanja sijui ni nini alicho nitendea huyu mpuuzi.


" Hahaha , Chuma nilikwambia kua wewe bado mtoto Sana kwenye sekta hii, ona Sasa ,muda si mrefu nawe unakwenda kufa Kama wenzako walio tangulia. Nakuonea huruma maana bado binti huna hata mtoto mmoja. Kwaheri Chuma."


"Hapana mganga naomba Sana unisamee ,sitaki kufa mie ,nipe adhabu yoyote ile nitaifanya."


" Chuma huwezi tena kunipangia Cha kukufanya,ila una machaguo mawili tu na si vinginevyo, chagua moja,kufa au nikutoe uchawi Kisha nikuoe uwe mke wangu!"

 

Mganga alinipa sharti zito ambalo sikuwahi kutarajia kukutana nalo. Kiukweli alinitaiti kweli kweli,nami sikua tayari kufa Yani ni bora kuolewa ni Jambo la heri kuliko kufa kizembe wakati chansi ya kuishi ipo. 


" Nipo tayari mganga kuacha uchawi na kuolewa na wewe"


" Safi Sana Chuma karibu kwenye ulimwengu Safi wa maisha mapya."


Basi ndugu msomaji kuanzia siku hiyo niliacha uchawi na nikawa mke bora kwa mume wangu Alumbile Kalumba. Tuliishi vizuri na tulikuja kuzaa  watoto watatu. 


Kwa Sasa nipo Safi ,nimemrudia Mungu. Ndugu msomaji Uchawi ni mbaya Sana usije kushawishiwa kuingia kwenye chama hicho.  Asanteni 🙏 na karibuni tena nyumbani kwetu kumenoga.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

URITHI wa Bibi 15

 Story... URITHI WA BIBI EP.15. Mwisho. Mtunzi....Steven Morgan 📲......... 0659115223 Naam kwa Mara nyingine tena ndugu msomaji tumekutana ...