Ijumaa, 8 Novemba 2024

URITHI wa Bibi 11

 Story............ URITHI WA BIBI EP. 11

Mtunzi ........Steven Morgan.

Contact......................+255659115223


Naam kwa mara nyingine tena Mungu yu mwema, tumekutana tena ndani ya story za Morgan, bila Shaka ndugu wasomaji wangu mu Wazima wa afya!!

Bila kupoteza Muda tunasonga mbele na hiki kigongo chetu Cha URITHI WA BIBI EP. 11 . Tukiwa tuna karibia mwishoni mwishoni . Staki nikuchoshe na story ndefu zisizo julikana zitaisha lini!!


Basi Kama kawaida, pale tulipoishia,ndipo tunapoanzia.                            


ILIPOISHIA EP.10

IKaribu ndugu Sadiki,unaweza kuketi hapo, mmhmm! Bila Shaka nakumbuka nilikutana na wewe kule barabarani na nikakosakosa kukugonga na gari langu ,si ndio?"

"Bila Shaka mchungaji!"

"Sawa kabisa na ulinielezeaga tatizo lako na mkewe kuhusu uzazi vipi ! Uliishia wapi ? 

" Tulienda hospital na mke wangu tulipima ,lakini Cha hajabu! Wote tukaonekana hatuna tatizo,Yani wote ni wazima,ila dokta ametushahuri tu tumwombe Mungu tu maana yeye ndie anae toa!!

"Mh!  Sawa ndugu sadii,Mungu pekee ndie anaye toa na ndie anaye twaa,umekuja sehemu sahihi tatizo lenu litakwisha "

"Amen mchungaji! Lakini ukiachana na hilo mchungaji, Kuna Jambo lingine linanitatiza Sana"


Nilimuelezea mchungaji kila kitu kuhusiana na ile ndoto na ile siku narudi nyumbani na kusikia mke wangu anaongea na mtu Kisha baadae baada ya kuingia ndani anasema alikua ni yeye tu na tv pekee.

" Sadiki upo kwenye hatari kubwa sana,tena ni hatari ya kufa,inaonekana Kuna hadui anakufuatilia,na ameshaanza kukushambulia, na hadui huyo hayupo mbali ,yupo ndani kwako."...................


          ENDELEA...............

Sadiki upo kwenye hatari kubwa sana,tena ni hatari ya kufa,inaonekana Kuna hadui anakufuatilia,na ameshaanza kukushambulia, na hadui huyo hayupo mbali ,yupo ndani kwako."...................


Nilishtuka Sana ! Baada ya mchungaji kuniambia kua nipo kwenye hatari kubwa!


" Sasa ,wacha tusali Kwanza ili tulikemee Jambo hili baya linalotarajia kukudhuru"


"Sawa mchungaji!" Nilimjibu mchungaji kua niko tayari kwa maombi muda huo.


"Baba katika jina la Yesu Kristo,namkabidhi kwako kijana  Sadiki, umuwekee ulinzi ulio imara,malaika wote wenye nguvu wamzunguuke kila aendapo , Roho zote Safi ziwe upande wake ,zimlinde dhidi ya hadui anae mkabili. Ee ,Mungu baba ,jidhihirishe kwa kijana huyu ili apate kuamini uwepo wako na aweze kuokoka na kulitangaza jina lako. Baba tunaomba na kushukuru katika jina la Yesu Kristo.Amen."


"Amen." Niliitikia baada ya mchungaji kuniombea. 

" Sadiki Sasa upo salama,ila Jambo la msingi ,usiache kulitaja jina la Mungu baba na Yesu kristo katika kila Jambo haswa unapohisi hari ya hatari."

"Sawa mchungaji nimekuelewa"

" Karibu Sana Sadiki ,juma pili unaweza ukaja kwa ajiri ya ibada ya pamoja ,lakini pia unaweza ukaja na mke wako ,pia unaweza kuniharika nyumbani kwako kwa ajili ya ibada."

"Sawa mchungaji,nitakuharika siku moja uje nyumbani"

" Asante Sadiki karibu tena! "


Niliagana na mchungaji Kisha niliondoka kuelekea nyumbani. Lakini kipindi nipo njiani nilijiuliza maswali mengi Sana ! Wakati mwingine nilihisi kua huenda mpenzi wangu Chuma akawa sio mtu wa kawaida. Kibaya zaidi nikakumbuka kipindi kile Cha mwanzo nilipokutana na Chuma kule baa ,alinileteaga masihara kwa kusema eti yeye ni jini!! Nilijua ananidanganya kwani jini hawezi kula chakula Kama kile alichokua anakula yeye pale! Lakini kauli yake ya kusema kua yeye ni jini! Wakati mwingine nikilinganisha na haya Mambo ninayo yaona ,nahisi kabisa Kama Chuma sio jini,basi atakua ni mchawi!!!


Nilikua bado nipo barabarani nikiongea peke yangu Kama chizi,nimesahau kabisa hata kupanda gari ,nikawa natembea tu kwa mguu kutoka segelea kuelekea buguruni!!!  Nilipokuja kushtuka! Nilishafika mbali Sana,kwakua nilichoka Sana kutembea,ilibidi tu nipande gari.


Nilifika nyumbani nyakati za saa kumi jioni .

" Karibu mume wangu,Mbona umechelewa Sana ! Ulikua wapi?"

"Swali gani Tena hilo mke wangu? Si nimetoka mihangaikoni? Mimi kazi zangu ni za kutafuta Yani day worker. Kwa hiyo kurudi nyumbani mapema inategemeana na muda nilioanza kufanya kazi."

"Sawa mme wangu lakini Mimi nimeuliza tu! Wala si ugomvi!"

"Usijari mke wangu,"

"Sawa ,haya Nenda ukaoge Kwanza maji tayari yapo hukohuko bafuni ,sawa mume wangu?"

"Nashukuru mke wangu wacha niende nikaoge Kisha niandalie msosi kabisa maana Nina njaa Sana"


Sadiki alienda kuoga bafuni. Bila kupoteza muda,nikahisi Kuna Jambo linaendelea ambacho Mimi silijui. Nikaenda chumbani nikachukua kile kioo changu Cha kichawi,nikaanza kumfuatilia mume wangu tangia anatoka nyumbani ,watu alio ongea nao barabarani , maongezi yao waliokua wakiongea, mwisho wa Safari yake niliona kua alienda kanisani kwa mchungaji, maongezi yao waliokua ,wakiongea yote niliyasikia.Hivyo nikahisi kabisa kua huenda mume wangu ameanza kunishtukia ila sio Sana. Nikarudisha kioo changu. Mara ghafla!!

Mume wangu Sadi aliingia ndani!

" Haaa! Yani Mimi nilifikiri ,umeshanitengea msosi mezani,sijui ulikua unafanya nini Sasa!!!"

"Mume wangu ,si ubadilishe hizo nguo Kwanza? Wacha gubu bana msosi upo kabatini nakuekea Sasa hivi"


Mume wangu alibadilisha nguo Kisha akaja pale mezani ,akataka tule wore chakula huwa hapendi kula peke yake,hata Kama Mimi nimeshiba atanifosi nile nae tu! Tukawa tunakula huku story za hapa na pale zikiendelea.

Mara simu ya mume wangu ikaanza kuita  kwenye mfuko wa kushoto wa suruali yake. Akaitoa na akapokea simu.


"Halloo mwambe! Mambo vip rafiki yangu,naona Sasa hivi dili zako unapiga mwenyewe hatushtuani kabisa!!"

"Sasa si ndio maana nimekupigia simu rafiki yangu ili nikujulishe kua Kuna dili nimelipata la kujenga mabanda ya kuku kwa mzee mmoja wa kichaga hapahapa dar es salaam. Kama una nafasi kesho uje ili twende "   

" Sawa mwambe Mambo si ndio hayo Sasa,kesho mapema tu ntakupigia simu"


Mume wangu alimaliza kuongea na simu Kisha akakata Kama alipiga yeye vile! Kisha akaendelea kula.

" Mke wangu dili hili tayari ,kesho mapema naenda kuanza nalo" 

"Safi Mungu ni mwema"

Tulimaliza kula Kisha ,tukawa tunaangalia filamu za kibongo , mpaka Usiku uliingia ,tulikula Cha Usiku tukawa tutaendelea kuweka CD na kuangalia muvi.

Ilishafika saa tatu na nusu Usiku, mume wangu akachukua CD moja ambayo haijajulikana ni cd ya aina gani,akaiweka ili tuitazame,kumbe ! Ilikua ni CD ya kibongo pia ! Lakini ilikua ni ya kichawi! Ilikua inaitwa " Mkoba wa babu"  inatisha Sana wakati mwingine niliogopa!!

" Aaah! Bana kumbe hata wewe unaogopa Mambo haya?"


Mume wangu aliniuliza.

"Ndio ,kwani nisiogope Mimi nimekua nani?" Nilimjibu.

"Si unakumbuka mwanzoni kipindi kile tulivyokutana kule baa,uliniambiaga kua wewe ni jini,Sasa Mbona unaogopa kutazama Mambo haya tu,ya kuigiza?


Aliendelea kuniuliza mume wangu Sadi ,sijui alikua na maana gani .

"Nilikudanganya tu! Ili usinisumbue uniogope ukae mbali nami! Sema tu ulikua king'ang'anizi Sana wewe! Eti ,ulikua unantaka hivyo hivyo hata Kama ningekua jini!! Shauri yako siku utakuja kulitongoza jini kweli litakuua!"

Nilimjibu mume wangu.

"Thubutuuuu!!! Kuniua haiwezekani labda hilo jini lipate ruksa kwa Mungu zaidi ya hapo atakufa yeye!!"

"Mmh! We mume wangu nawe kwa kujigamba sijui unachoringia ni nini! Mpaka jini akushindwe wewe kukuua?"

"Wee! Mimi naringia kuwa karibu kabisa na Mungu wangu pamoja na Yesu kristo wa Nazareth.Hakuna wa kunisumbua"


Basi ile sinema ilikua ikiendelea ,mume wangu aliitazama kwa umakini lakini Mimi nilikua nakwepesha macho kwenye vipande vilivyokua vinatisha. Story zikiendelea lakini wakati mwingine nilikua  naingiwa na hasira pindi tu ! Mume wangu anapolitaja jina Yesu Na Mungu baba. Ndugu msomaji jina la Yesu ni dawa na kinga ya kweli kwa wenye imani nalo.Ni kweli jina la Yesu lina nguvu kushinda majina yote unayoyajua wewe . Hili ndilo jina pekee la uponyaji. Nadhani Kama wewe ni mlokole tutakua tunaelewana vizuri hapo! 


Basi Usiku ulizidi kukolea Kama chumvi ya mawe, mume wangu akapitiwa na usingizi akalala palepale kwenye Kochi,sikutaka kumwamsha nilimwacha palepale! Mara ghafla! Nikasikia kishindo kikubwa juu ya bati " kwapuuuu!!!" Nilishtuka kiubinadamu lakini nilijua kua ni nini, kinachoendelea.

Mara , akatokea yule mmama mkenya ,pale chumbani akasema ," Mbona unachelewa Sana kujiandaa wewe! Muda ndio huu twende zetu " 

"Nilikua na mume wangu muda mwingi nilijisahau kwa kweli ,samahani ila,tumfanyize mtu wa bandia abaki hapa kitandani badala yangu ili mume wangu akija huku chumbani ajue kua nipo nimelala asishtuke."


Basi,tukamfanyiza mtu wa bandia Alie fanana na Mimi ili alale pale kitandani badala yangu kipindi ambacho Mimi sipo pale kitandani.Tukamlaza yule mtu pale kitandani.  Hapa naomba nieleweke hivi,nikwamba mchawi anapotaka kuondoka Usiku Kama yupo na mumewe au mtoto, Basi mchawi huamua kutengeneza kopi yamwili wake ubaki pale kitandani ili mume au mtoto akiamka ,asijikute kua yupo peke yake na kujiuliza maswali, ndo maana huacha ile kopi ili aonekane yupo kumbe hayupo.

Na ule mwili wa bandia unao bakia pale kitandani,hata uutingishe kiasi gani hauwezi kuamka Wala kuongea,japo unaweza ukauona Kama mtu tu ,amelala na anapumua ila ukiuamsha hauwezi kuamka kabisa Wala kuongea kutokana na kwamba ule sio mwili wa kweli kiukweli, ule mwili unaweza kua ni mgomba,mchi au kinu!!!!


Basi , tuachane na hayo ,mimi na yule Mama mkenya, tukafanya yetu Kisha tukatoka nje kichawi,Kwanza tuliwachawia wapangaji wenzangu wa pale ,haswa wale wanao jifanya kula wali nyama,samaki kila siku,niliwasotea kweli kweli. Ndugu msomaji kwa wale mnao ishi nyumba za kupanga ,jaribuni kua wastaarabu ,wakati mwingine usitake kila mtu ajue umepika nini,pia usiwe mwema Sana sababu kwa wema wako huohuo, Kuna watu wanateseka!! Na si kila unae msaidia ni mwema kwako wengine ni wabaya Sana japo unawasaidia lakini bado watakuona Kama unaringa na watautumia wema wako Kama sampo ya kukushusha. Yani Kama ulikua unatoa Sasa utapokea! Yani Kama ulikua unasaidia masikini Sasa wewe ndo utakua ombaomba. Na hii ndio ubaya wa uchawi Yani watu wema na wazuri wasio kua na hatia ndio wanao andamwa bila sababu za msingi,ni ujingaujinga tu!!!


Basi tuliendelea kuwachawia wapangaji Kisha tukapotea Kama upepo unaovuma na kutulia ghafla, tukajikuta tupo kilingeni Yani kwenye makutano ya wachawi .Tulikuta wachawi wengi Sana kilingeni, wakiendelea na shughuri zao za kichawi .mkuu akaniambia kua ni kwanini bado sijakamilisha suala la utoaji wa sadaka.?

Lakini Mimi nilimjibu kua ,nimeshaweka mtego na tayari mhusika yupo kwenye kalenda ya kifo!

" Sawa Chuma kua makini Mambo yasije kua tofauti!". "sawa mkuu" nilijibu.

" Lakini Chuma unatakiwa Sasa ,umuite huyo mhusika kwanza hapa kilingeni ,umpige ndumba Tena Kisha leo umtangulize mbele kwenye kuwanga kwako huko mtaani haswa kwa jamaa zake huyo mhusika ."

Kama kawaida kwa maneno ya mamraka yasio pingika nikamuamuru Sadiki wangu atokee pale kilingeni , akatokea akiwa anashangaa shangaa! Lakini hakuna anachokielewa, nikampiga ndumba tena kwa kumnuwia mabaya mikosi na nuksi zote zikawa upande wake.


Basi,baada ya hapo,nilimwacha yule Mama mkenya pale kilingeni Mimi nilimchukua Sadi ,nikamtanguliza mbele ,yeye ndio akawa dereva anaye jua njia. Nikamuamuru twende kwa yule rafiki yake Mwambe aliye mpigia simu kua kesho Kuna dili la kujenga ,mabanda ya kuku . Tukaenda mpaka kwake tukaingia ndani , Sadiki akiwa mbele hajitambui kua anawanga kwa niaba yangu. Tulimwangia Sana Mwambe lakini kibaya zaidi Mwambe alishtuka ghafla usingizini na akamwona Sadiki.


"Sadiki!,Mbona si hamini macho yangu,kumbe wewe ni mwanga ?"


Mwambe alijiuliza maswali lakini hakuna wa kumjibu Wala kumthibitishia hilo Jambo aliloliona kua ni ndoto au ni kweli?

 Wakati anajiuliza hayo maswali Mwambe ,sisi tulipotea chapu na kuibukia nje ya nyumba,nikacheka Sana tena sana Yani Kama vile ninavyo fanya ni vizuri kumbe ni ujinga tu!! Sauti ya kicheko ilikua ni kubwa sana lakini kwa mwanadamu wa kawaida huwezi kuisikia sauti hiyo katika uharisia wake. labda,Kama utaisikia sauti hiyo,basi utahisi ni sauti ya ndege wa hajabu,au mnyama wa hajabu,au unaweza kusikia wimbo unao ujua unapiga katika kichwa chako Yani ni Kama unaimba kimoyomoyo.  Ujue hapo Kuna mtu mbaya anapiga kelele ,Kama sio cheko  basi anaimba nyimbo ya kichawi.


Baada ya hapo tukatoweka ,tukarudi nyumbani,Sadi nilimlaza kitandani,Kisha nikaupoteza ule mwili wangu wa bandia pale kitandani. Nikajiweka sawa Kisha nami nikalala.

⛅ Asubuhi ikafika ,nikaamka mapema Kama mwanamke ,nikaandaa chai , nikaandaa maji ya kuoga pia. Mume wangu alichelewa Sana kuamka ,aliamka saa mbili na robo .

"Dah! Mke wangu ,kwa nini hukuniamsha mapema wakati unajua wazi kua leo ,Kuna dili natakiwa niende nikafanye nipaye pesa?"

"Mimi mwenyewe nilijisahau mme wangu , samahani" nilikua mnyenyekevu Sana kwa mume wangu.

"Sawa wacha nkaoge niondoke zangu"

Sadi alienda kuoga Kisha akarudi nikamtengea chai akanywa . 

"Asante mke wangu kwa chai,wacha niende kibaruani,japo leo najihisi nimechoka kweli sijui naumwa?"

"Hapana mume wangu ,huo ni uchovu tu, umelala Sana umechelewa kuamka ."

" Sawa Chuma wacha niende"

Mume wangu aliniita kwa jina langu, mara ghafla simu yake ikaita. ( Tilililii, tilililii, tililililiiiiiix2 )

"Halloo mwambe,nakuja Sasa hivi mtu wangu"

" Wahi rafiki yangu ,muda umeenda sana bosi amenipigia simu,alafu Kuna Jambo lingine nataka nikueleze ukweli maana naona umeanza kunipanda kichwani,najua nikikukaushia siku nyingine utanipanda hata matakoni wewe!"

" Mwambe Mbona sielewi unachokiongea? Hebu ngoja nije Kwanza utanielezea vizuri"

 Mume wangu sadi nilimsikia akikwaruzana kidogo na jamaa yake Mwambe ,Mimi nilijua kinachoendelea.Basi mume wangu akaondoka. 


Hodi hodi!  " Nanii?" " 

Nani ugomvi bana ! Njoo nje huku ,Mimi Sadi.

"Aaah! Ngoja nije "

Mwambe akatoka nje na vifaa vya kazi ,nikavichukua na kuvibeba ,bila kupoteza muda tuliondoka kazini.Tukiwa njiani .." eheee rafiki yangu Mwambe, vipi Mbona sijakuelewa ulicho kizungumza kwenye simu kwa ukali ,kwani Kuna nini?" 

" Sadiki sijui nianzie wapi lakini wacha twende kazini Kwanza nitakueleza hukohuko"

"Ok sawa "

Mwambe hakutaka kuniweka wazi kabisa , kiukweli aliniweka kwenye mawazo kua hiyo ishu inayomkwaza yeye ni ipi? Na maimi Sadi nahusika vipi ? Nikawa Sina raha kiukweli.


Mara tukafika baada ya kusafiru kwa gari kwa umbali fulani, tukatembea kidogo tukaingia kwenye nyumba moja kubwa ya kisasa, tulikaribishwa na mdada alionekana kua ni mdada wa kazi .Akatuitia bosi, na bosi akatoka akiwa na mkewe na watoto zao wakubwa wawili ,wa like na wa kiume,tukasalimiana Kisha mama mwenye nyumba akarudi ndani na wanae,  Bosi akatuchukua na kutupeleka nyuma ya nyumba yake .


Akatuonesha eneo la kazi ,vifaa na kila kitu,tukapatana being ya kujenga Banda lile ni laki mbili. Bosi akachukua kiti na gazeti akakaa pembeni akituangalia sisi tunavyoendelea na kazi.


Tukapima ,Kisha nikaaanza kuchimba mashimo kwaajili ya nguzo. Mara Mwambe akaanza kuongea.

" Eheee!, Sasa jamaa yangu ,wakati tutaendelea na kazi ,wacha nikwambie kile ulichonikela, hakuna kugombana hapa tuwe Kama tunaongea tu hapa" 

"Sawa mwambe letter habari!" Wakati huo huku kaz zinaendelea.


" Hivi Sadiki! Katika maisha yako ulishawahi kua mchawi,au unaujua uchawi?"

"Mh! Kwakweli siujui huo uchawi na Wala sikuwahi kua mchawi na sitarajii kua mchawi, sijui kwanini umeniuliza hivyo Mwambe?"

*Sadiki nimekuuliza hivyo kwa makusudi na Kama nilivyokwambia sitaki hapa tugombane ,tunaelekezana ili tujue nini kinaendelea"

"Nakusikiliza Mwambe endelea!"

" Sadiki bana wewe ni mchawi!! Na sijui huo uchawi umeuanza lini! Na Jana Usiku nilikuona kwa macho YANGU ,ndani kwangu ulikuja kuniwangia,na Mimi hua napenda kumweleza mtu ukweli.samahani Kama nitakua nimekukasirisha!!"


Mwambe aliongea kwa sauti kubwa tu ,kiasi ambacho yule bosi alikua akitusikia tukiongea.


" Mwambe Mimi sikupingi mawazo na maono yako,ila kiukweli Mimi si mchawi Kama unavyo fikiri labda kutakua Kuna namna ,Yani Kuna mtu ananichezea.Maana kiukweli rafiki yangu Mimi mwenyewe wakati mwingine nashindwa kuelewa hata shemeji yako nyumbani,nashindwa kumuelewa ,Yani ana Mambo ya hajabu Sana."


" Sadiki Kama ni hivyo Basi huenda ikawa shemeji akawa ndio mchawi"

"Hilo sikupingi ndugu yangu kwa asilimia 99% shemeji yako ni mchawi,Sasa nitafanyaje ndugu yangu?"


" Hapo bana Sadiki ni kua makini ,raha sivyo na wewe utakuja kua mchawi kweli au atakuja kukutoa sadaka" 


" Kwani shemeji anaitwa nani! Na ametokea wapi? Maana wewe nawe kwa kuokota okota wanawake siku utaokota jini!"

" Usintishe bana Sadi! Shemeji yako anaitwa Chuma ,ni African beaut hivi ,anatokea pande za morogoro huko sijui Kijiji gani lakini ni mtu wa milimani huko kwenye safu za milima ya ulugulu.!"

 

Ghafla bosi akaniita Mimi!"

" We kijana Samahani,nakuomba ! Kuna kitu umeongea hapo kidogo umenishtua"


Sijajua ni nini bosi alichoniitia  mpaka nilipoenda kumsikiliza.

"Naaam bosi"

"Ndio kijana ,Mimi naitwa foya au mzee foya Kama watu walivyo zoea kuniita. Nimewasikiliza vizuri mazungumzo yenu,lakini Kuna jina la mtu mmoja umelitaja na mahari alipotoka, umenishtua mno!!"


"Mh! Jina gani hilo mzee wangu! Na kwanini likushtue hivyo?"

" Kijana wangu hilo jina ni lilikua ni la mfanya kazi wanting wa ndani,lakini kwa Sasa huyo mtu NI hadui yangu mkubwa,najua huko aliko Chuma wa morogoro Ndolelo, anataka alipe kisasi kwangu na familia yangu .Chuma ni mchawi Yani ni binti hatari Sana.!!!!"


" Mzee Foya, samahani kidogo ,unajua Chuma Mimi ni mke wangu,Na nilishaona  Mambo ya hajabu pale nyumbani,nahisi huenda akawa ndio huyohuyo binti unaye mzungumzia."


" Ndio huyo huyo bila Shaka,kijana,unatakiwa ujiongeze,japo Mungu yupo lakini unatakiwa ujiongeze raha sivyo utapotea."

" Sasa mzee wangu Mimi sielewi chochote Cha kufanya,nilishawahi kumshilikisha mchungaji ,lakini mchungaji alinishauli kumwomba mungu tu zaidi."

" Kijana mchungaji yupo sahihi kabisa , Mungu kwanza lazima umtangulize Kisha mengine ndio yanafuatia. Kama hutojari tafuta siku moja  baada au kabla ya kumaliza kazi yangu,nikupeleke kwa mtaaaramu mmoja yupo huko huko morogoro vijijini mgeta ,huyo anaitwa "Mganga Alumbile Kalumba" kiboko ya vibwengo wote,atakucheki na atakukinga dhidi ya hadui yako. Mimi mwenyewe mpaka Leo niko salama ,ni kwa  ajili yake japo Mungu ndio mkuu katika hayo.Nadhani umenielewa?"


"Nimekuelewa bosi wangu ,wacha nikafanye kazi tutaendelea kuwasiliana"


................ Ita endelea..........................

Je, nini kitaendelea? Usikose kufuatilia story yetu nzuri yenye utamu mpaka tindini au tebwetani yani full shuga sukari.


Nashukuru kwa wote mnao nisaport kufuatilia story za Morgan wa Madola.

Saport zenu zisi ishie hapo, ukipenda unaweza pia kunisaport kwa kikombe 🥃 kimoja Cha kahawa 🍷 na kashata.

Pia ningependa kupata zaidi maoni yenu,Kama Kuna Jambo haliko sawa kwa upande wangu au wenu, tuwekane sawa. Asante sana ndugu msomaji ,nakutakia siku njema.✏️

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

URITHI wa Bibi 15

 Story... URITHI WA BIBI EP.15. Mwisho. Mtunzi....Steven Morgan 📲......... 0659115223 Naam kwa Mara nyingine tena ndugu msomaji tumekutana ...