Story ...... URITHI WA BIBI EP. 5
Author..............Steven Morgan
📞..................... +255 659 115 223
🌷 TULIPOISHIA 🌷
Basi nikiwa bado nipo chumbani na Bibi huku nikikiweka kioo alicho nipa kwenye begi langu la kusafiria. Baada ya hapo kwakua ilikua tayari ni usiku Sana ,tukatoka nje kichawi,yani tulitoka bila ya kufungua milango,moja kwa moja tulienda kwa Bibi zubeda ambae yule mgeni Foya ndipo alipo fikia,ilikua ni usiku Sana ,wote ndani walishalala fofofo, Mimi na Bibi tuliruka na kutua kwenye paa la nyumba la Bibi zubeda.Tulipotua juu ya bati,hapakua na kelele wala kishindo zaidi Kama aliekua ndani Kama hajalala basi anaweza akasikia Kama mchanga au vimawe mawe vinamiminika kwenye bati!!
Ndugu msomaji ukisikia Hari hiyo,ujue wanga wamesha tua na Kama hujalala basi utalala kwa lazima .unachotakiwa kufanya baada ya kuona Hari hiyo ni kumwomba Mungu Sana akunusuru na ibirisi huyo.
Basi tukatua kwenye lile bati la bibi zubeda ,japo bati zake zili oza lakini hatuwezi kuanguka kwani tunakuaga wepesi sana . Tulimwaga madawa yetu ili asie lala kwa muda huo ,alale kwa lazima ili sisi tuendelee na kazi yetu.
Tulitazama kwa kupitia jicho la tatu la kichawi tulimwona yule bosi Foya anaye taka kesho juma tatu twende wote dares salaam amelala fofofo huku simu yake ya tachi ikiwa chini. Tulirukaruka huko juu ya bati huku tukiimba nyimbo za kichawi kwa sauti. Hata Kama hujalala huwezi kutusikia. zaidi, utahisi wimbo flani unao ufahamu ume play katika kichwa chako ,ukiona hivyo ujue wazee wa kiza wapo nje au ndani wanacheza na kuimba. Basi tukacheza Sana Mimi na Bibi baadae tukaingia ndani chumbani kwa yule mgeni Foya . Taa ilikua inawaka tukaizima Kisha tukaanza kumsotea kwa makalio ,muda mwingine tulimjambia mdomoni akawa anashtuka na kukohoa sana. Bibi aliniambia kua nimkalie tumboni kwa makalio yangu Kisha nimsotee sotee !! Nami nikafanya hivyo tena kwa haraka . Lakini ghafla yule mzee Foya alishtuka usingizini kwa haraka na akanikamata nikiwa palepale juu ya tumbo lake!!! Huwezi amini Bibi aliondoka na kuniacha nimekwama juu ya tumbo la mzee Foya ambae ni bosi wangu mtarajiwa huku nikiwa uchi wa mnyama na makalio yangu makubwa yaliyojaziana minyama yakiwa juu ya tumbo la mzee Foya.
******* ***** ENDELEA 👇 ************
Nikiwa bado nipo juu ya tumbo la mzee Foya ,sikua na ujanja kwani mzee Foya alinikamata kisawa sawa!! Nikajua sasa leo ndio mwisho wangu wa maisha ,nikahisi huwenda mzee Foya akanidhuru . " Ahaaa! Kumbe ulijua Mimi ni mtu wa mchezo mchezo! Sasa Leo nakuua yani nakuchinja kabisa!!". Aliongea mzee Foya kwa kujiamini zaidi huku Mimi nikitetemeka kwa hofu nisijue Cha kufanya. Nilihofia zaidi kwamba je,nitafanyaje endapo mzee Foya atanibahini? Maana mpaka muda huo bado alikua hajanitambua kua ndio Mimi binti Chuma anaye taka kunichukua nikamfanyie kazi. Kulikua na giza nene pale chumbani sababu chemli iliyokua inawaka ,tuliizima mwanzoni kipindi tunaingia na Bibi . " Alafu unaonekana wewe ni binti mdogo kabisa kwanini Sasa unakua shetani namna hii? Ngoja kwanza nifanye mpango wa kuwasha taa ili nikuone vizuri!" Duh! Nilishtuka Sana kwani nilijua muda wa kumbuka umekaribia. Lakini kabla mzee Foya hajafanya chochote ,ghafla tu akatokea mkuu wetu, yule aliyetuhapisha uchawi. Akampiga kofi mzee foya la paji la uso,Foya akazimia Kisha akanichukua na kupotea ghafla,mara tu nikajikuta nipo juu ya kibeku yani ndege ya kichawi aina ya Air fagio plane( Broom air plane ) huku mkuu akiwa ndio dereva na Mimi nilikaa nyuma nikiwa kwenye umbo la nyau. Usafiri huu huwa ni wa haraka Sana Kama nilivyo elekeza hapo mwanzo. Hivyo mkuu alinifikisha mpaka mlangoni nyumbani kwa Bibi.Bibi alitoka nje haraka Wakati sisi tukiwa tunakaribia kutua.
" Bibi Chuma mnatakiwa kuwa makini Sana ,hata hivyo umefanya la maana Sana kunipa taarifa mapema. Raha sivyo leo Chuma angeumbuka."
Hayo yalikua ni maneno ya mkuu akimwambia Bibi, kumbe Bibi baada ya kukimbia na kuniacha alitoa taarifa kwa mkuu ndio akaja kunipa msaada.
" Na wewe chuma inabidi utulize akili ,ujitambue ! Wewe una nguvu Sana ila hujui kuzitumia,uwezo ulio nao wewe, chocho te waweza fanya , Chuma bila Shaka kesho ndio unakwenda kufanya kazi kwa huyo mzee Foya huko dar es salaam. Hakikisha unakua makini Sana usije ukakosea chochote. Yule mzee mpaka asubuhi akiamka hakuna chochote atakacho kikumbuka zaidi tu atakufuata ili muondoke,Mimi nakutakia safari njema pia ukatanye kazi yetu kwa weredi na umakini zaidi. Kwaherini!"
Mkuu baada ya kuongea maneno hayo,alituaga na akaondoka kwa usafiri wake wa haraka. Tukabakia Mimi na Bibi
Kwakua ilikua ni USIKU Sana, hatukuzungumza mengi ,tukaenda kulala ili kesho niwahi kuamka kwaajiri ya safari.
Kama wasemavyo waswahiri kua ,awike asiwike ni lazima kuche, Ndivyo ilivyokua , asubuhi ilifika ,nikajiandaa vya kutosha ,ninaposema nimejiandaa vya kutosha namaanisha nilifungasha Kila kitu kinacho nihusu haswa dhana za kichawi. Kumbuka hiyo ilikua ni siku ya juma tatu na ilipofika saa kumi na mbili asubuhi ,mzee Foya alikuja alinikuta nje na Bibi tukimngoja yeye tu!
" Karibu Sana mzee foya ,mfanyakazi wako ndo huyu yuko tayari kwa Safari." Bibi alimwambia mzee Foya kwa msisitizo. " Asante Sana Bibi mbokeleni, Chuma..tusipoteze Sana muda wacha tuwahi gari la kwanza"
Foya akatoa shilingi elfu 30 akampa Bibi Kisha sisi tukaondoka. Bibi alinipungia mkono Kila nilipogeuka kumtazama.
Tulifika msamvu mapema tukapata basi ,safari ilisonga mida ya saa kumi tukafika kwa mzee Foya maeneo ya Tabata shuleni. Tulimkuta mkeo na watoto wawili wa umri wa miaka 6 na miaka minne. " Karibuni wageni , karibuni sana,lete huo mzigo wako binti nikupokee!" Nilimpa begi langu mama mwenye nyumba ambalo lilikua zito Sana . " Heee! Mbona begi lako zito Sana,umeweka mawe nini?" Aliongea mama mwenye nyumba. " Kaweke huo mzigo bana mbona unataka kuchunguza mzigo usio kuhusu?" Alidakia baba mwenye nyumba Foya. Basi yule mama Akaniambia nimfuate,akaenda kunionesha ,chumba changu Cha kulala nikaingia nikaweka mzigo wangu. Kisha tukatoka akanitembeza nyumba nzima ,nikaona mazingira yote.akanielekeza na majukumu yangu ya kazi . " Hivi dada unaitwa nani?" " Naitwa Chuma." ( "Aahaa,sasa dada Chuma,Mimi na baba yako wote ni wafanya kazi ,na asubuhi wote tunaondoka ,Mimi huwa narudi mida ya saa kumi,baba yako huwa anarudi saa kumi na moja na kuelekea. Watoto hawa wanasoma chekechea,huwa kuna gari mida ya saa moja linawapitiaga kwahiyo uhakikishe unawapikia asubuhi na mapema wale,waoge kisha uwaandae kwaajiri ya shule. Ukisiki honi ya gari unawatoa nje wapande gari la shule ,sawa Dada Chuma?" "Sawa mama nimekuelewa." "Nashukuru Kama umenielewa lakini pia ,unatakiwa inapofika saa Saba mchana una andaa chakula . Mambo mengine ni kujitahidi usafi wa mwili na mazingira ,sawa Chuma?" " Sawa mama nimekuelewa". Basi Kama umenielewa unaweza kwenda kuoga bafu ni lile pale chumba Cha tatu pembeni na kinacho fuata ni choo."
Mama mwenye nyumba alinielekeza mambo mengi haswa majukumu ya kazi. Nikaingia chumbani kwangu nikabadirisha nguo,Kisha nikatoka nikiwa na kanga moja ambayo imenichora umbo langu la mwili haswa makalioni ambapo sio siri ,sijisifii kweli Mungu amenibariki minyama ya makario.
Nikakatiza pale sebureni ambapo alikaa baba mwenye. Nyumba na mkewe . Nilijisahau nilijua kua bafu na choo vipo nje hivyo, nilitaka kutoka nje. " Wewe binti vipi! Mbona hivyo?" " Naenda kuoga mama!" " Wewe si nilikwambia kua bafu na choo vipo chumba Cha tatu pembeni? Sasa huko nje unaenda wapi! Au umeshazoea huko kwenu vijijini milimani huko?
" Nilijisahau tu mama samahani!" " Sawa Chuma tumekuelewa nenda tu kaoge mama!!"
Aliongea mzee Foya huku akinitazama kwelikweli. Basi nikageuka na kuelekea huko bafuni . " We baba Maria vipi? Mbona unamtazama Sana yule binti kwa nini?"
Nilimsikia mama mwenye nyumba akimsema mmewe kua alikua akinishangaa Sana. Nafikiri ni kwa sababu ya ile kanga niliyovaa na umbo langu ,lilimpa shida Sana.
Basi nikaelekea bafuni ,ile nafungua mlango tu!
Namwona bibi yuko kule bafuni,kiukweli nilishtuka Sana ,ilibaki kidogo tu ,nipige kelele.
" Tulia Chuma, nimekuja tu kuona unapokaa ,ni pazuri Sana, nafikiri tutaonana baadae ,mida ya kazi,kuna kazi ya kufanya leo". "sawa bibi"
Bibi alitoweka Kisha nami nilioga na kuondoka chumbani kwangu.
Ile naingia chumbani tu! Nakuta kioo kipo kitandani kwangu. Kioo hiko hakikua kigeni kwangu kwani nilikitambua vizuri tu ,kua ndio kile alichonipa Bibi na nilikiweka kwenye begi langu ,Sasa sijui kilitoka vipi kukaa pale kitandani.!! Nikakisogelea Kisha nikakitazama ,nilichokiona ni tofauti na nilicho kitarajia! Nilijua nitajiona Mimi mwenyewe,lakini, huwezi amini,nilimwona Bibi zubeda wa kule kwetu morogoro, ambae ana undugu na mzee Foya, na mzee Foya ndipo alipofikia kwa Bibi zubeda ambapo siku moja kabla ya kuja huku dar tulienda na Bibi kumwangia mzee Foya na ndipo nilipo kwama kwenye tumbo la mzee Foya.
Sasa tuachane na hayo,turudi pale ndani chumbani kwangu ,nilizidi kukitazama kile kioo,nikamwona Bibi zubeda akiniteta na jirani yetu mmoja wa kulekule nyumbani . Huyo jirani alikua anaitwa mama majuto ,alimpelekea umbea Bibi zubeda kua eti Mimi na Bibi yangu ni wachawi Sana na pia ikiwezekana, wamwambie mzee Foya kua Mimi ni mchawi anifukuze. Kama nilivyo eleza hapo mwanzo kua ,kioo ni msaada mkubwa Sana kwa wachawi,nimeweza kumwona Bibi zubeda kwenye kioo changu Cha kichawi kwa sababu yule Bibi zubeda na mwenzake walikua wakizungumza sehemu ambayo kulikua na kioo kilichokua wazi yani hakikufunikwa. Kwa hiyo kwetu sisi inakua ni Kama CCTV camera.
Basi baada ya hapo Sura ya Bibi zubeda na mwenzake zikapotea Kisha ikaja sura ya mkuu wetu wa uchawi, mkuu alinikazia macho Kisha akasema ," Chuma nadhani unajua Cha kufanya" Kisha mkuu akapotea.
Nikamwita Bibi zubeda kwenye kioo akatokea tena. Nikachukua begi langu Kisha nikatoa mdori wa kike, nikaanza kuukaba kwenye shingo ule mdori huku nikinuiza maneno ya ufundi. Mara nikaanza kumwona Bibi zubeda kwenye Koo akijishika shingo huku akitoa macho ,kuhashiria maumivu makari. Alihangaika mpaka alianguka chini ,huku Mimi nikiwa bado naendelea kumkaba yule mdori ,mwishoni nikamnyonga shingo ya Yule mdori ,na Bibi Zubeda nae alijinyoosha palepale. Yani nimuua kabisa asije akaniharibia kwa bosi wangu Foya.
Nikachukua kile kioo na kukirudisha kwenye begi, nikikabadili nguo Kisha nikatulia kitandani. Mara nikasikia mama Maria yani mama mwenye nyumba ananiita, " Chuma , Chuma toka uje tule " kumbe mama alikua amesha pika ,nikatoka kuelekea sebuleni, ile nafika tu sebuleni, mara namwona ..................................
ITAENDELEA.................
Je, Chuma ameona nini pale sebuleni? Usikose sehemu ya 6 . Uhondo ndio kwanza unaanza ukiwa na maarifa kibao. Mambo mengi muda mchache.Mungu akijaaria tutakutana tena sehemu ijayo.Asante.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni