STORY............ URITHI WA BIBI EP. 7
MTUNZI........ STEVEN MORGAN
SIMU........ +255659115223
Naaam,Kwa mara nyingine tena, tumshukuru Mungu kwa kukutana tena ,katika episode ya 7, karibu tena katika muendelezo wetu wa URITHI WA BIBI. Bila kupoteza muda ,
TULIPOISHIA ndipo tunapo anziaππ
ππππππππππππππ
Mzee foya baada ya kuria kwa muda mrefu kutokana na taarifa ya kifo cha bibi zubeda wa morogoro,alinyamaza Kisha akamwambia mkewe aketi chini wazungumze kua itakuaje?
" Mke wangu kesho inabidi niwatangulize huko morogoro kwenye msiba mapema,lakini Mimi nitakuja jioni sababu kuna sehemu nitapitia kutafuta ukweli wa kifo cha ndugu yangu bibi zubeda. Na nikimjua hadui alie husika ,hama zake ,hama zangu." Mzee foya aliongea kwa hasira sana,huku Mimi na mama Maria tukiwa tumetulia kama tumezubaa vile. Basi kwa kua muda ulikua umeshaenda,Kila mtu aliingia chumbani kulala............. ............ .................. ....
ENDELEA...
Basi ,kwakua muda ulikua umeshaenda,kila mtu aliingia ndani kulala. Usiku huo chuma Mimi sikuweza kupata usingizi,kwani niliwaza mengi sana ,ikiwemo suala la bosi wangu mzee foya kutaka kuchunguza kifo Cha ndugu yake bibi zubeda wa morogoro. Nilijiuliza je,akinibahini kua ni Mimi mfanyakazi wake Chuma ndie niliye husika je ,itakuaje?
Ndugu msomaji katika vitu ambavyo ukivifanya basi ,ni lazima utaandamwa na wachawi sana, ikiwa ni pamoja na kufuatilia ishu za kishirikina zilizofanywa na wachawi, maana wachawi wanapofanya Jambo huwa hawataki mtu mwingine ajue chanzo Cha tukio,na endapo wakigundua kua Kuna mtu anataka kufuatilia ukweli wa Jambo Fulani ambalo lilifanywa na wao ,basi hapo vita itakua imeanza .
Niliwaza na kuwazua bila kupata jibu ,usingizi sikupata kabisa ,lakini mwishowe nikatoa kioo changu Cha kichawi,Kisha nikamuita mkuu wetu wa uchawi . Mkuu alitokea palepale ndani ya kioo , " Chuma unashida gani ,naona umeniita" mkuu aliongea, " nikweli mkuu nimekuita Kuna Jambo linanitatiza sana,tulifanya mauaji, lakini bosi wangu anataka kuchunguza ukweli wa kifo Cha ndugu yake,nina hofu endapo akinibahini itakuaje? Nisaidie mkuu". Nilimueleza mkuu kinacho nisibu. " Chuma hilo mbona ni Jambo dogo sana,lakini pia usipokua makini huwa ni Jambo kubwa sana. Sasa,chakufanya unakijua chukua kioo chako hiko baada ya Mimi kuondoka ,muite bosi wako humo,Kisha umuhoji kua atakwenda kwa mganga gani,Kisha umfuate huyo mganga na umpe rushwa yoyote ile iwe ya pesa au ya mwili ilimradi tu aupindishe ukweli kwa mteja wake,hapo utakua umeokoka. Hahaha hahahaha hahahahaaaaaaa!!! Kwa heri!"
Mkuu baada ya kunipa maelekezo ,alicheka sana ,Tena cheko nzito mpaka nilitaka kuogopa!
Ndugu zangu hapa ngoja kidogo tujifunze kitu,wakati mwingine waganga sio wa kuwaamini sana. Haswa pale unapoona kua tatizo lako kila unapotibiwa hauponi ,anakubadirishia kila dawa lakini hauponi. Ukiona hivyo maranyingi huwa ,huyo mganga wako unaye mtegemea kutatua matatizo yako kila wakati,tayari amesha anza kupotoshwa na wachawi ,anakula rushwa na badala ya kukutibu anakuongezea maumivu kwa dawa anazopewa na wachawi .
Tuachane na hayo, turejee pale chumbani nilipokua ,baada ya kupokea muongozo kwa mkuu, nikachukua kioo changu tena,hua nakiamini sana,ni kioo ambacho alinipaga bibi.
Nikakikazia macho kile kioo Kisha nikamuita bosi wangu mzee foya kwa sauti ya mamraka isiyo pingika. Palepale mzee foya bosi wangu,akatokea ndani ya kioo changu. Nikaanza kumuhoji maswari kwa maneno ya mamlaka yasio pingika naye alinijibu vile vyote anavyo vikusudia kuvifanya kutoka moyoni.
Hapo nilijua kua mzee foya kesho anatarajia kwenda kwa mganga gani,hivyo kabla yeye hajafika nilazima nifike Mimi Kwanza ili nimrubuni yule mganga wake ili bosi asije akaujua ukweli.
Basi ,Kama waswahili wasemavyo ,kua awike asiwike ni lazima kuche na Usiku wa deni haukawii kuisha. Ndivyo ilivyo kua ,nilishtuka asubuhi ya saa kumi na mbili na nusu baada ya mke wa bosi kunigongea mlango na kunitaka nijiandae kwa safari ya kurudi morogoro kwenye msiba.
Kiukweli sikujua usingizi ulinikamata muda gani lakini ndo ikawa hivyo nimeshtuliwa kumesha kucha. Bila kupoteza muda Kwanza nikachukua kioo Tena nikamuita Bibi chapu Kisha nikampa maelekezo ,kua bosi wangu mzee foya leo anataka aende kwa mganga mmoja anayeitwa " Aumbile kalumba" anayepatikana mgeta. Kwa hiyo nilimpa maelekezo Bibi kua amfuate yule mganga asubuhi ileile amrubuni na ampe rushwa ya pesa ili aupindishe ukweli wa kifo Cha Bibi zubeda. Bibi alinielewa Kisha akatoweka . Nami nikaenda kuoga Kisha nikawaogesha na watoto nikawavalisha ,nami nikajiandaa vyema ,tayari kwa Safari.
"Chuma toka twende maana muda umeenda sana" alikua ni mke wa bosi akiniita ili tuondoke,muda huo nami nilishabeba begi langu nikatoka chumbani kwangu na kuelekea sebuleni,ambako nilimkuta mke wa bosi na bosi mwenyewe mzee foya .
"Safari njema mke wangu,muende salama nami jioni au Usiku nitakua nishafika huko msibani" aliongea mzee foya Kisha akatusindikiza hadi ubungo stendi ya mabasi .Tukapanda Basi la abood la saa mbili ,tukaagana na mzee foya Kisha yeye akageuza akarudi nyumbani baada ya gari kuanza kuondoka. Mipango ya mzee foya nilishaijua na tayari nimeshaitafutia korokwini ,sikua na wasiwasi tena kwani nilijua tu kwamba Bibi ameshaenda kuvuruga mitambo. Safari iliendelea huku njaa zikiwa zinauma kutokana na kutokula asubuhi. Wakati mwingine nilitapika ndani ya gari,sijui kwanini ila nafikiri ni kutokana na kutokula au kutokua na mazoea na Safari ndefu za mara kwa mara. Baadhi ya sehemu gari lilidimama ,tulichimba dawa na kupata chakula kidogo Kisha Safari iliendelea.
Hatimaye tulifika Msamvu stendi ya mabasi ya morogoro saa Saba mchana.Tukachukua usafiri wa taxi ukatupeleka milimani kwetu huko Ndolelo kwenye safu za milima ya ulugulu. Baada dakika Kama kumi na tano tulifika sehemu tulishuka kwenye gari,Mama alimlipa dereva Kisha sisi tuliendelea na Safari yetu kwa miguu kwani gari lilishindwa kusonga mbele kutokana na ufinyu wa barabara. Tukapandisha vilima huku Mimi nikiwa nimembeba mtoto mmoja na Mama nae amembeba mtoto mmoja. Jasho zilituvuja wakati mwingine tulipumzika Kwanza kwani mama Maria mke wa bosi hakuzoea Safari za vilima na miteremko mikali.
Tuliendelea na Safari ,hatimaye yapata saa Tisa na nusu ,tunafika msibani kwa marehemu Bibi zubeda. Tulikuta watu wengi sana wakiwemo majirani na ndugu wengi sana na watoto wa bibi zubeda,walikuja watu kutupokea mizigo yetu lakini Mimi niligoma kupokelewa begi langu nililibeba mwenyewe.Tukapelekwa ndani sebuleni kupumzika jamvini kwani tulikua tumechoka sana.
Tuachane Sasa na habari za Chuma huko msibani ngoja tumuone sasa Bibi yake Chuma na Safari yake ya uvurugaji wa mitambo.
Bibi Chuma au Bibi Mbokeleni bila kuchelewa baada ya kupewa taarifa na mjukuu wake Chuma ,alifunga Safari ya kichawi kwenda kwa huyo mganga Alumbile Kalumba huko mgeta. Ninaposema alifunga Safari ya kichawi namaanisha sio Safari ya kawaida bari ni Safari ya MWENDO KASI Yani ni Safari ya kufumba na kufumbua Yani ni chapu kwa haraka.
Ghafla! Tayari Bibi Mbokeleni amejikuta ametua kwa kishindo kikari sana ,nje ya nyumba ya mganga Alumbile,mpaka mganga akashtuka na akatoka nje ya kibanda chake cha msonge kilicho ezekwa kwa nyasi. Uso kwa uso na Bibi Mbokeleni, " Mbona umekuja kwa kitisho ,umekuja kwa Shari au kwa heri?" Aliuliza mganga Alumbile. " Ha ha haaa haaaa haaa! Nimekuja kwa heri kabisa,wala sina Shari na wewe, ila Kuna mtu atakuja mchana wa leo ,anaitwa Foya,huyo ndio nina shari nae. Kuna ndugu yake tumemuua Mimi na mjukuu wangu anaitwa Chuma,Sasa huyu mzee foya atakuja kwako kupata ukweli kuhusu kifo cha ndugu yake."
" Sawa hiyo ni kazi yangu na huyo atakua ni mteja wangu wa siku nyingi, Sasa wewe mchawi unataka nikusaidie nini? "
" Naomba sana mganga,uufiche ukweli wa Jambo hili ,nitakulipa kiasi Cha pesa kikubwa mara mbili na kile atakacho kupa mteja wako. Na ukilikataa ombi langu ,utakua umeitangaza vita Kali isiyoweza kumalizika ."
" Kwa hiyo umekuja hapa kwa mganga Alumbile Kalumba,kuja kunitisha na kunitangazia vita?, Mimi sijawahi kutishwa na kigagura wala mchawi yoyote yule,Kama wewe ni mchawi kwa nini usi zuie kuumbuka kwenu? Nafikiri wewe Bibi hunijui vizuri, labda ngoja nijitambulishe kwako vizuri maaana naona umekuja kwa Shari. Mimi ndio mganga Alumbile Kalumba,kiboko ya majini na wachawi wakubwa na wadogo Kama wewe na timu yako. Sitoi wala sipokei rushwa kutoka kwa kiumbe hai yeyote yule. Sipindishagi ukweli kua uongo hata siku moja,pia simuogopagi kiumbe hai yeyote yule na ukitangaza vita na Mimi,hakikisha unajiandalia kabuli lako Kwanza.Nadhani mpaka hapo utakua umenielewa Bibi unaweza ukaondoka kwa amani huwa sitaki mzaha."
Bibi Chuma jitihada zinaonekana kugonga mwamba baada ya mganga Alumbile kumkatalia ombi lake la kupotosha ukweli.
" Hahaha! Hayo ni maneno tu mganga,huna lolote wewe,Mimi ndio Bibi Mbokeleni au Bibi Chuma ,mchawi niliye kubuu nisie wezekana,kwa kua hutaki kunifanyia kazi yangu ,umesha tangaza vita na kamati ya ufundi jiandae kuiyaga Dunia mganga raha sivyo kubaliana na Mimi kunifanyia kazi yangu."
"Bibi Chuma Kama nilivyo kueleza Mimi huwa sitishiki kwa lolote na huwa nangoja hadui anianze na Mimi namaliza kabisa,kwa hiyo nakupa muda Kwanza kajiandalie kaburi lako kabisa na Kama Kuna URITHI wowote nenda kauache kabisa maana ukipambana na Mimi Sasa hivi hutopata bahati ya kua hai ndani ya lisaa limoja lijalo Mimi ndio Alumbile kiboko ya wachawi Sina muda Tena wa kuzungumza na wewe ondoka haraka hapa kabla sijakudhuru!" Aliongea mganga kwa hasira sana.
Bibi Chuma akajifanya mwamba hakutaka kuondoka akataka kuujaribu uwezo wa mganga Alumbile,bila kujua kua Alumbile huwa hajaribiwi! Bibi Chuma akarusha uchawi mzito wa maangamizi lakini hakufua dafu kwa mganga Alumbile,alitulizwa kiwepesi Kama pasi ya mpira wa miguu. Alumbile bila huruma akapiga pigo moja takatifu linalo itwa mwana ukome,Bibi Chuma alirushwa juu Kisha akajipigiza chini kwa kishindo na habari yake ikawa imeisha, alikufa palepale!!
" Nilikwambia wewe Bibi lakini ulikua mbishi Sasa habari yako imeisha nenda kwako sitaki mzoga hapa" aliongea mganga Kisha akaupoteza mwili wa Bibi Chuma kimiujiza na kuurejesha nyumbani kwake ili waje wamshtukie ndani kwake akiwa maiti.
Baada ya masaaa machache mbeleni Mzee Foya aliwasiri kwa mganga Alumbile Kalumba ,alikuta Kuna watu wanne wakingoja kuhudumiwa, alisubiri mpaka ilipofika zamu yake na yeye akaingia kibandani.
" Karibu sana mzee Foya ,pole sana na Safari pia pole sana kwa msiba na pole sana kwa matatizo."
" Asante sana mganga Alumbile sijui umejuaje Kama Nina msiba na hayo matatizo?"
" Mimi ni mganga wa kweli ,kabla ya wewe kufika hapa,hadui yako tayari alishafika hapa maana alijua kua wewe utakuja hapa."
" Hadui yangu ni nani ,na alikuja hapa kufanya nini?"
" Kua mpole bwana Foya wanasemaga waswahili kua kikuracho ki nguoni mwako.Hadui yako unaishi nae wewe mwenyewe tena nyumba moja! Ila hadui namba moja nimesha ndio alie kuja hapa leo. Kunirubuni kua nisikwambie ukweli wa kifo cha ndugu yako ,na akataka kunidhuru baada ya kumkatalia lakini hakuweza nikamdhuru yeye na kumuua kabisa.!"
" Duh! Unaweza kuniambia huyo ni nani alikuja na ukamuua?" " Usiwe na haraka foya kila kitu Kiko wazi utajua tu mwenyewe taratibu. Sina Cha kufanya kwako kwa Sasa sababu kinga nilisha kupatia na familia yako yote zaidi muombe sana mungu akusaidie zaidi. Lakini kumbuka kua hadui yako unaishi nae nyumba moja ila sikwambii ni nani,sababu unaonekana kua una hasira sana ,kua mpole Leo au kesho utamjua hadui yako .Nenda tu msibani na ukifika huko Kuna msiba mwingine utausikia ,huyo aliekufa ndio hadui namba moja na hadui mwingine aliye bakia ndio unashi nae nyumba moja,ila usije ukachukua sheria mkononi utafungwa haya mambo yataisha kimya kimya."
"Sawa mganga Alumbile Mimi nimekuelewa sana na nitakua mpole Kama ulivyo sema wacha niende niwahi msibani."
Mzee foya alia aga Kisha akaanza Safari ya kurudi Ndolelo msibani .
Tuachane na mzee Foya,turudi kule msibani kwa marehemu Bibi zubeda.
Chuma akiwa na Mama Maria na watu wengine kibao wakiwa wametulia pale ndani sebuleni kwenye jamvi au mkeka, Chuma Kuna kitu kilimshtua sana,machale yakamcheza Kisha akamwambia mama Maria mke wa mzee Foya, " Mama samahani naomba niende nyumbani mara moja kwa Bibi yangu sio mbali sana ni hapo tu Kijiji Cha pili."
"Sawa Chuma nenda ila usichelewe kurudi maana si unaona hawa watoto wanavyo sumbua?" " Sawa mama nitawahi sana kurudi Wala sita chelewa."
Binti Chuma alitoka ndani na kuondoka kuelekea kwao kwa Bibi yake Mbokeleni,Chuma akiwa na begi lake mgongoni Safari inaendelea kupanda na kushuka vilima Chuma alishazoea. Chuma alikua Kama amechanganyikiwa flani hivi! Japo kinacho mchanganya hakukijua kabisa ila ,alikua na hamu kubwa ya kufika nyumbani kwa Bibi yake Mbokeleni. Masikini Chuma bila kujua kilichomkuta Bibi yake ni kipi aliendelea na Safari yake.
Hatimaye Chuma anafika nyumbani kwa Bibi yake Mbokeleni akiwa na presha bila kujua sababu ni nini?
Nyumbani palikua kimya sana ,nikaangalia mlango wa nyumba ya Bibi ,ulikua umefungwa kwa komeo,nikafungua komeo nikausukuma mlango lakini,haukufunguka. Unaonekana ulifungwa kwa ndani .nikatazama huku na kule hakuna aliye niona nikaingia ndani kichawi .
Ghafla ! Namwona Bibi yupo kitandani amejinyoosha huku macho yamemtoka kweli kweli Yani ukimtazama kwa mbali,unaweza ukamwona Kama amevaa miwani kumbe ni macho yamemtoka bibi yangu! Nilishtuka sana kwani nilianza kuziona dalili za hatari kubwa .Nikamsogelea Bibi nikawa namwamsha lakini hakuamka,ndipo nilipo gundua kua Bibi yangu Mbokeleni ameshafariki.!! Nilichanganyikiwa sana nikaanza kulia huku machozi yakinivuja Kama maji lakini nikajikaza,nikaanza kukusanya vitu vyote muhimu haswa dhana za uchawi na nikaenda kuzificha nje mbali kidogo na nyumbani,niliondoka kichawi na nikarudi kichawi. Nikatuma meseji ya kichawi yenye taarifa ya msiba wa Bibi , wachawi wote wa hapa kijijini wao ndio watu wa Kwanza kupata taarifa .
Kisha nikaaanza kulia kwa sauti mpaka majirani wakanisikia wakaanza kuja nikawaeleza nilicho kikuta ndio hicho ila sijui chanzo. Baada ya muda watu walijaa kwa wingi ,walitoa vitu vyote nje, vijana walifunga maturubai na baadhi ya watu walipeleka taarifa mpaka Kijiji Cha pili.
Nilishangaa sana kwani baada ya muda mchache ,baadhi ya watu nilio waona kule kwenye msiba wa Bibi zubeda wamekuja pale nyumbani na kunipa pole wengine waliuliza kilichotokea lakini niliwaeleza hari harisi niliyo ikuta. Ndipo nilipo amini kua taarifa za msiba zimesha fika mpaka Kijiji Cha pili. Mipango ya msiba ikapangika kua kesho yake ndio maziko yatafanyika sawa na msiba wa kule Kijiji Cha pili.
Tumuache Chuma kidogo na majanga yake , ngoja tukaone kinachoendelea kule msibani Kijiji cha pili kwa marehemu Bibi zubeda. Maana Mzee Foya amesha anza kupanda na kushuka vilima karibia atafika msibani.
Msibani kwa Bibi zubeda kulitawaliwa na vilio vya kila aina ,Yani ni kelele tu ndizo zilizo tawala.
Mara ghafla! Mzee Foya aliwasiri msibani alianza kuwasalimia watua alio wakuta pale nje huku wakipeana pole ya msiba. Aliingia ndani alikutana na mkewe huku watoto wake wakiwa wanacheza na watoto wenzao. Alimchukua mke wake na kwenda kukaa chemba ili waongee kidogo.
" Mama Maria mke wangu,kifo Cha ndugu yangu ,sio Cha heri za mwenye enzi Mungu,kimesababishwa na mwana wa adamu,na nikimgundua ,hakika sita muacha mzima na Leo mganga wangu ameniambia kua nitajua hilo,Kuna ishara nitaziona "
"Sawa baba Maria lakini pia Kuna msiba mwingine umetokea kule Kijiji Cha pili..!"
"Eheee! Sasa hiyo ndio ishara yenyewe ya Kwanza niliyo ambiwa na mganga Alumbile Kalumba,na huyo aliekufa ndio hadui yetu namba moja na mwingine..... Mwi..ngine!" "Sawa baba maria lakini unajua aliye kufa huko ni nani? Na hujiulizi kua Chuma Yuko wapi hapa?"
" Eheee ni kweli alafu nilitaka kukuuliza tangia mwanzao kua Chuma Yuko wapi? Na aliye kufa huko ni nani?"
" Mme wangu Chuma aliniaga kua anakwenda kumsalimia Bibi yake huko Kijiji Cha pili lakini inasemekana ,alipofika huko, alimkuta Bibi yake amefariki na haijulikani kilicho sababisha kifo Cha Bibi Chuma."
"Duuuh! Mke wangu,tunavita kubwa na tusipo kua makini tunaweza tukaangamia mmoja mmoja maana Bibi yake chuma ndio alikua hadui yetu namba moja ,na mganga aliniambia kua hadui namba mbili tunaishi nae nyumba moja,bila Shaka atakua ni Chuma!! Chuma ama zako ama zangu na kuanzia Sasa simtaki Tena Chuma katika familia yangu"
Mzee Foya aliongea kwa uchungu huku akimsisitizia mke wake kua Chuma hamtaki tena maana ni hadui yao mkubwa sana hawatakiwi kuishi nae nyumba moja....
Kesho yake ikafika mazishi yakafanyika pande zote mbili watu walilala matanga kisha tarehe za kupanda msalaba zilitajwa pande zote mbili ,kule kwa Chuma msalaba utakua 15/08/20..
Na kule kwa bibi zubeda ni 14/08/20..
Shughuli za mazishi kwa ujumla zilikwisha.
Je, unafikiri nini Kita endelea? Je, Chuma ataenda kuungana na mzee Foya na kurudi Tena dar es salaam? Je, Chuma atabaini nini kuhusu kifo Cha Bibi yake? Je,vita vikali vitakua kati ya Chuma na mganga Alumbile Kalumba! Au kati ya Chuma na mzee Foya? Usikose kufuatilia sehemu ya 8 ya URITHI WA BIBI, utapata majibu ya maswari yote. Vita ndio inaanza vita vikali vya kiroho na kimwili.