Story :.................... URITHI WA BIBI . EP.3
Author................... Steven Morgan
📞 : .......................+255 659 115 223
Email : ................. stevennemes2k@gmail.com
Karibu tena ndugu msomaji katika mwendelezo wa story yetu.Kabla ya kusonga mbele, ngoja tukumbushane kidogo..
TULIPOISHIA:
Ndugu msomaji, sehemu iliyopita tumeona kua chuma mashaka na bibi yake mbokeleni,wakiwa kwenye harakati za kishirikina za kuruka kwa usafiri wa air kibeku aina ya " ungo natural air plane" ambayo safari yao iliwapeleka mpaka Nairobi Kenya. Ambako huko ,mambo yaliwaendea hovyo,walipokatiza kwenye anga la kanisa moja la Kenya Assemblies of God . Ambapo wali anguka na ndege yao kwenye uwanja wa kanisa nyakati hizo za usiku,ila bibi alifanikiwa kukimbia na kumwacha mjukuu wake Chuma akiwa amekwama.Ambapo baadae alikuja kuokolewa na mmama mmoja mchawi wa hukohuko Kenya na kutoweka nae.Chuma akiwa kwenye mikono ya yule mama mwenyeji wa kenya mambo ya kichawi yaliendelea Kama kawaida.Kwani tumeona kua chuma kwakua alikua na njaa aliweza kula supu ya kichawi yani supu ya nyama ya mtu ikiwa na mchuzi mwingi wa damu.Majanga kwa chuma yaliendelea ambapo walipata misukosuko pia walipokwenda kuwachawia watu mtaani. Mwishoni tuliona Chuma akinusurika kubakwa akiwa amekwama kwenye nyumba ya kijana mmoja huku yule mama akiwa amekimbia na kumwacha na alipojipanga tena ,alirudi kumwokoa tena Chuma .Ambapo baaadae kwa kutumia usafiri wa ndege ya kichawi aina ya "fagio natural Air Plane" , Chuma akiwa na yule mama bila kupoteza muda walisafiri kwa haraka na kuwasiri nchini Tanzania nyumbani kwa kina chuma.Ambapo walimkuta bibi yake na chuma akiwasubiri ,kisha baada ya chuma kupokelewa na bibi yake,yule mmama mchawi wa Kenya akaondoka zake bila kusubiri.
ENDELEA..
Bibi alinipokea usiku ule ,kwakua nilichoka Sana sikuweza kuongea mengi bali nili muomba bibi niende nikalale afu mambo mengine tutazungumza asubuhi. Bibi aliniruhusu Kisha nikaenda chumbani kwangu kulala . Nilipokuja kushtuka ilikua tayari kumesha kucha,kwani nilisikia ndege wakilia huku nje bibi aliendelea kufagia uwanja. Niliamka na kuchukua ndoo yenye maji ya kuoga ya baridi ,nikaenda kuyaoga ili niondoe uchovu. Kiukweli nilichoka Sana tena Sana!! Nilipomaliza kuoga , tayari bibi alisha ivisha chai na futari yenye mchanganyiko wa magimbi,miogo ,ndizi na vigonzo. Futari iliungwa kwa nazi . Bibi alitandika jamvi dogo na aliandaa chai Kisha wote tukaketi jamvini na kunywa chai kwa pamoja. "Pole Sana mjukuu wangu ndio ukubwa huo". " Asante bibi ila namshukuru Sana mungu ameniepusha na mengi". " Mh! Mungu tena katokea wapi? Wewe umshukuru tu yule mama mchawi wa Kenya ,ndie alie kusaidia sana." "Nikweli bibi napaswa pia kumshukuru yule mama mungu ambariki Sana."
"Mungu ambariki kwa kazi gani nzuri aliyoifanya? Hebu wacha kumtaja taja huyo mungu wako kwenye haya mambo!"
"Sawa bibi ila hii kazi Mimi siitaki tena !"
"Wee! Tena funga huo mdomo wako,hivyo unavyosema wiki hii tu! Natakiwa nikukabidhi mikoba rasmi ,na wala huwezi kupinga wamesha kuchagua wakubwa, hahaha haahaa haahaa!"
Kiukweli mtoto wa nyoka ni nyoka , sikuweza kulipinga hilo . Sijui bibi aliniroga!! Maana siku zilikwenda hatimaye wiki ikafikia ,alilolisema bibi ndilo lililokua . Na kiukweli sikuweza kupinga . Nakumbuka ilikua siku ya juma nne nyakati za usiku sana,waswahili wanaita mida ya wanga! Tukiwa nyumbani ,bibi alinipaka dawa na kunichanja chale nyingi za kichawi mwilini na kunielekeza baadhi ya mambo makubwa. Kisha baada ya hapo ,tukaenda kwenye sherehe ya kukaribishwa mwanachama mpya wa kichawi. Tukaenda kwa kuruka kwa kupiga guu la kushoto chini na kupotea kwa ghafla Kisha tukaenda kutokea kwenye uwanja wa mpira wa miguu,ukiwa umefurika watu kibao ,wakubwa kwa watoto ,vijana kwa wazee!! Uwanja huo pembeni kuna makaburi mengi sana . Kiukweli niliogopa Sana ! Japo Mimi mwenyewe nilikua natisha ukinitazama lakini,na Mimi pia niliwaogopa wenzangu nilipo watazama ! Walikua wanatisha Sana.!
Uwanja huo siku ufahamu kwa haraka kwani sikua mtu wa kutembea tembea sana maeneo.
Basi kwakua watu walijaa Sana uwanjani,na sisi pia tukatafuta siti na kuketi. Tukawa tuna sikiliza kinacho zungumzwa na mkuu pale katikati ya uwanja. " Karibuni Sana wanachama wenzangu,katika utangulizi wa sherehe yetu ya kuwakaribisha wanachama wapya katika utawala wetu"
Watu walishangilia Sana kwa sauti zenye milio tofauti za wanyama ,yani wengine walilia Kama paka , wengine Kama farasi ,Simba ,bundi yani kila mtu alikua na mlio wake ! Niliogopa Sana kwani hata bibi nilie kaa karibu nae ,pia nae alishangilia kwa kulia Kama paka shume " nng'aaaaaaaaaauuuuuuuuuuu!"
Haisee! Muda mwingine nilitamani hata kumkimbia bibi lakini sikua na jeuri hiyo.
" Bila kupoteza muda,tunawaomba watu wafuatao waje hapa kati, aje binti nuru,aje kijana Lazaki,aje binti Chuma,pia aje na mwana dada Maria ."
Nilishtuka sana nilipo lisikia jina langu lakini Cha kushangaza nilijikuta nakwenda pale kati bila mwenyewe kujielewa . Wote tulio tajwa tulienda pale katikati ya uwanja kwa mkuu ambae alionekana kutisha zaidi ya wengine. Mkuu akanyosha msinga wenye manyoya ya mnyama was hajabu Kisha akatupiga piga nao usoni Kisha akanyosha mkono wa kushoto likaja kapo kubwa lililojaa vibuyu tofauti tofauti. Akatoa dawa ya mgando katika kila kibuyu akazichanganya Kisha akatuchanja chale za kutosha na kutupaka ile dawa .Alipo maliza akasema karibuni Sana ,nasi nasi kwa pamoja tukajibu Asante sana mkuu.
" Ndugu zangu Sasa mmekua mafundi,hakuna mtu wa kuwasumbua duniani hapa ,labda mbinguni! Zoezi la kuwapa mikoba limekwisha,kilichobakia ni kuwaapisha ambapo zoezi hilo litafanyika kesho juma tano kuanzia saa kumi jioni.Leo tutashangilia kwa pamoja kwa kuimba na kucheza pia tutakula na kunywa.hivyo kila kamati ijiandae kwa majukumu yake . Kamati ya mapishi naomba mchangamshe mikono Wakati tunaendelea kuburudika kwa ngoma na kucheza baada ya hapo tunataka kula "
Mkuu aliongea hivyo Kisha ngoma zikaanza kupigwa lakini nilishangaa Sana baada ya kuona ngoma zinazopigwa haziku ngoma Kama unavyo fikiria,bali walikua watu wakipigwa vichwa na wengine walipigwa makalio na kutoa mlio Kama ngoma iliyo wambwa kwa ngozi!!
Tulicheza Sana kwa kuimba kwa sauti kubwa yani endapo watu wangetusikia majumbani basi ni lazima wangetoka kututazama.
Mkuu alinyoosha msinga wake juu ,ngoma ikazima na wale watu waliofanywa kua ngoma walionekana kuchoka Sana. Mkuu aliwanyoshea msinga wake ,wale watu wakatoweka!!
Sijui walipokwenda ila nafikiri walirudishwa makwao.
"Ndugu washirika wenzangu,baada ya kucheza vya kutosha ,na kuimba vya kutosha ,Sasa ni muda muhimu wa kula chakula chetu pendwa . Chakula kipo tayari ,bakia hapo hapo ulipo utaletewa chakula chako"
Mkuu baada ya kumaliza maneno hayo,mara watu wa hajabu wakaanza kugawa chakula kwenye mabakuli makubwa Sana yakiwa yamejaa mapande makubwa ya nyama huku yakiwa na mchuzi mwekundu wa kutosha. Chakula kiligawiwa kwa haraka ,muda huo sisi pia tukiwa katikati ya uwanja Kama wanawali,pia tuliletewa msosi wetu kwenye mabakuli makubwa . Tukala na kunywa bila kuhofia msosi ulikua mtamu Sana kwani ulikua unafanana kabisa na utamu wa supu niliyo kunywa kule Kenya. Nilikunywa na kula bila hofu kwani niliufurahia msosi ule, kiukweli ilikua ni damu mbichi ya mtu pamoja na minyama nyama ya mwili wa mwana damu.
Tulipomaliza kula na kunywa mkuu akasimama na kutupongeza wote tuliojiunga na uchawi siku hiyo na kusema kua kesho juma tano tusisahau ,saa kumi kamili jioni tukutane kwenye pori la kusimikwa .
"Ndugu zangu sherehe yetu imeisha ,ila kesho juma tano chonde Sana,walengwa wote tukutane kwenye pori la kusimikwa kwa haraka kwa muda uliotajwa, kwa Sasa hakuna Cha zaidi ,kusanya kilichochako kila mtu arudi nyumbani ila msikose kuwanga japo nyumba moja kabla hamjaenda kulala makwenu"
"Sawa mkuu" watu wote tuliitikia kwa pamoja Kisha tukapiga miguu chini na kutoweka kwa ghafla .Mimi na bibi tukakutana kwenye njia panda moja karibu na makazi ya watu ,ikiwa kunakaribia kupambazuka kabisa,bila hofu tuliingia kwenye nyumba moja ya mchungaji Boniface ,tuliwanga kwa kusota sota kwa makalio kuanzia sebuleni mpaka vyumbani walimo lala. Kiukweli mchungaji Boniface alikua mwepesi Sana ,alikua anamwongopea mungu hakua mchungaji kweli alikua tapeli yani ni nabii wa uwongo. Tulimchezea Sana mwisho tulimbeba na kumlaza nje ya nyumba yake Kisha sisi tukaondoka zetu nyumbani. Tukalala kidogo asubuhi na mapema ikawadia . Bibi aliniambia kua nijiandae mapema kwani saa kumi kamili inatakiwa niondoke ili nikasimikwe.
Siku hiyo nilichoka kiasi nikaenda kuoga Kisha nika andaa chai Kama kawaida Mimi na Bibi yangu tukanywa huku story nyingine zikiendelea. Muda ulisonga mbele hatimaye saa kumi kasoro dakika tano,nilishtuka bibi akiniamsha kumbe nilipitiwa na usingizi,Bibi alishapika Cha mchana Lakini sijala tukaingia ndani na kuvaa mavazi yetu ya kazi. Tukapiga miguu chini na kuibukia kwenye msitu mkubwa ambapo tuliwakuta wenzetu walishafika nilikua nasubiriwa Mimi tu!
"Afadhari bibi mbokeleni na chuma kwa kufika maaana mlikua mnatuchelewesha"
Aliongea mkuu mwenye sura ya kutisha.
"Bila ya kupoteza muda walengwa wote njoeni mkae chini ya mti huu" ulikua ni mti mkubwa sana ,tulikaa pale chini tukiwa uchi ,mkuu alitambika kwa lugha yake tusio ielewa ,mara ghafla ikanyesha mvu kubwa japo kulikua na jua kari la saa kumi.Yani kulikua na mvua na jua kwa pamoja. Waswahili wanasemaga eti,simba anazaa!!!! Dhana hii imeenea Sana mtaani kwamba jua likiwaka na mvua ikinyesha kwa pamoja eti,Simba ana zaa, ukweli ni kwamba ukiona jua linawaka na mvua inanyesha kwa pamoja, ujue kuna wachawi wapya wana hapishwa na wamekubariwa kupokea nguvu kutoka kwa shetani wa kichawi.
Basi,mvua ikaendelea kunyesha na jua likaendelea kuwaka ,mara ghafla mvua ikakata na likabakia jua Kama kawaida. Mkuu wetu alicheka Sana , akasema kwamba " vijana wangu mmepokea nguvu kubwa Sana za kuusumbua ulimwengu, natumaini mtakua mawakala wazuri Sana wa shetani katika kuleta ubovu ulio kidhiri katika Dunia . Mbarikiwe Sana na lusifa ,na mkafanikiwe katika kutenda dhambi zenu zilizobarikiwa na shetani".
Mkuu alipomaliza kusema hayo Mimi nikajihisi mwenye nguvu Sana na nikajikuta naweza kufikiria na kufanya mambo makubwa bila ya kufundishwa. Macho yaliniwiva kama nyanya ya utunguja. Mkuu alinitazama Kisha akasema " Chuma ,wewe unaonekana kua na nguvu nyingi sana ,kafanye kazi ,jamii ikutambue na kukuogopa ,hakuna kiumbe atakae weza kukudondosha , ulimwengu ni wako chuma , chochote unaweza kufanya kuanzia Sasa,umesha pewa nguvu ya mamlaka!" Hayo yalikua maneno ya mkuu akinisifu,baada ya hapo tukanyanyuka na kurudi nyumbani baada ya kuruhusiwa na mkuu.
********************************************
ITAENDELEA.
JE,nini kitafuatia? Sasa chuma amesha kua kamili ,unafikiri nini kitaendelea? Usikose kufuatilia sehemu ya 4,ya URITHI WA BIBI. UHONDO NDIO KWANZA UNAANZA. Fanya ku LIKE PAGE, NA KU SHARE,Ili wengine waone na kuburudika.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni