Ijumaa, 8 Novemba 2024

URITHI wa Bibi 15

 Story... URITHI WA BIBI EP.15. Mwisho.

Mtunzi....Steven Morgan

πŸ“²......... 0659115223


Naam kwa Mara nyingine tena ndugu msomaji tumekutana tena katika kufunga ukurasa wa mwisho wa story yetu ya URITHI WA BIBI.  Wacha tumalizie story yetu kabla hatujaanza kigongo kingine.


Kama kawaida pale tulipoishia ndipo tunapo anzia.


Ilipoishia ep.14

Chuma msalaba huu wa kulipiza kisasi Cha Bibi yako utakua peke yako mwenyewe,sitaki uwaponze wengine kwaajiri ya nafsi yako.Jipange vya kutosha Kisha Anza kumdondosha mganga Alumbile Kalumba Kisha mmalizie mzee Foya ,sawa?"


Mkuu alinisisitizia.

"Sawa mkuu" 

Nilimjibu.


"Basi Kama tume elewana kila mtu atoweke mahara hapa Mara moja na muende mkaendelee na shughuri zenu nyumbani."


Mkuu alituruhusu Kisha kila mtu alitoweka kwa stahili yake,kurudi nyumbani. Wengine walitoweka Kama radi,wengine walitoweka Kama upepo ,Yani zilikua ni mbwembwe tu za kichawi katika kuonesha uwezo.


 ENDELEA...

Basi Mimi nilirudi nyumbani ,nilipofika sikua na chakufanya zaidi ya kuniweka Safi katika hari ya kiubinadamu kamili.Nilikaa na kuwaza Sana kwamba ni kwa namna gani nitaweza kumuangusha mganga Alumbile Kalumba!!

Siku hiyo sikupata usingizi kabisa .


Wazo likanijia , nikachukua kioo alicho niachiaga bibi Kisha nikapiga ndumba nikiwa nimerudi Sasa kwenye hari ya kikazi. Alitokea palepale yule mganga kwenye kioo. Alikua ni mtu wa makamo kidogo. Nilimwangalia kwa makini nikagundua kua yule alikua si mganga wa mchezo mchezo.


Nikaamua kulitengeneza pembe ili nimtume aende akamchunguze yule mganga. 

Ndugu msomaji bila Shaka katika jamii yako iliyo kuzunguuka ,ulishawahi kusikia kua flani ni mchawi na ana miliki  mapembe .

Je,unajua pembe ama mapembe ni nini katika imani za kichawi?

Najua wengine mnafahamu vizuri zaidi yangu ila wengine pia hawajui kabisa kua pembe ni nini!!!

Kwa tafsiri nyepesi kwa mtu asiye fahamu ,atakwambia kua pembe ni,kitu chenye mfano wa pembe za ng'ombe ,au unapozungumzia habari za mapembe unazungumzia mapembe ya wanyama .


Wenye mawazo hayo,wako sahihi kwa uelewa wao lakini, katika imani za kichawi pembe ni jina tu ila halifananii hata kidogo na pembe ya mnyama.


Ndugu msomaji,niliposema kua nilitengeneza pembe na kumtuma akamchunguze yule mganga,unaweza ukajiuliza kua ,pembe ni kiumbe wa namna gani na anatengenezwaje?


Ndugu msomaji pembe hutengenezwa kwa kutumia Mara nyingi Midori ya kuchezea watoto. Mdori huo hufanyiwa ndumba za kichawi na kua kiumbe chenye uhai Kama mtu kamili akiwa kwenye kimo kilekile Cha mdori.Lakini pia pembe huyo anakua na uwezo wa kubadirika kua kiumbe mwingine yeyote yule mfano;

Pembe anaweza akabadirika kua panya na akaja kwako kufanya Lile alilotumwa Kama kubukua unga wa ugali au Mchele. Ndugu msomaji labda ulikua ukidhani kuwa watu wabaya huwa wanabukua pesa tu peke yake. Hapana watu wabaya huwa wanabukua hata mazao yanapokua shambani au nyumbani.

Wakati mwingine ndugu msomaji umeshawahi kusikia au kuona panya wanasumbua Sana ndani ya nyumba na unapoweka sumu ,wapo watakao kufa lakini,Kuna wengine wasumbufu zaidi bado wataendelea kusumbua hata ukiweka tena sumu kwenye chakula,watakila mpaka watasafisha lakini hawafi!! Ukiona hivyo panya hao sio wa kawaida bali ni mapembe. Kua makini na vyakula vyako ndani, maana Kama ulinunua kilo 20 za unga na kilo 30 za Mchele,ujue mtakula wote yaani utakuja kushangaa vyakula hivyo vitakuja kuisha muda usio utarajia. Kama uritarajia kua msosi wako utakaa wiki mbili,ujue utashangaa ndani ya wiki na siku mbili msosi umekatika.


Pia pembe,ana uwezo wa kujigeuza paka au nyau ,na hutumwa kazi mbalimbali Kama za upelelezi ,Yani wakati mwingine mnaweza mkakaa sehemu mkawa mnapiga story,lakini baadae akatokea paka na kuketi karibu yenu,nyie bila kujua mnaanza kuteta kua flani mbaya Sana na yule jirani yetu nae ni mtu mbaya Sana.Kumbe yule paka ni pembe atawasikiliza mwanzo mwisho na atarekodi kila kitu na kupeleka ujumbe huo kwa aliye mtuma.


Ndugu msomaji ngoja turudi kwenye story yetu,basi nilitengeneza yule pembe na kumtuma kwa yule mganga akachunguze ulinzi wake ukoje kabla sijaenda Mimi moja kwa moja.


Nilikaa na kutulia ,nilikua nikisubili pembe alete majibu sahihi. Ndugu msomaji kumbuka pembe ni Kama kifaa kinacho tumwa na opareta wake alikua ni Mimi. 

Na akipatwa na tatizo lolote ni lazima nijue hata Kama nipo mbali nae .


Haisee! Muda mchache baadae ,nilihisi kichwa kuuma Sana baadae mwili mzima ulikua na maumivu. Hii ilikua ni ishara tosha kua pembe wangu amehangamizwa !!


Baadae alirudi pembe wangu akiwa tayari mfu au kifaa kisicho faa tena. 

"Mh! Inaonekana huyu mganga si wa mchezo." Nilijisemea moyoni  Kisha nikaamua kulala maana ilikua ni Usiku Sana na siku hiyo sikua na hamu hata ya kwenda kuwanga.

Asubuhi ikafika nikaamka mapema Kama kawaida ,nikaoga Kisha nikawa naendelea na shughuri zangu za nyumbani za kawaida.


Nilipomaliza shughuri zangu zote za kufua na kujipikilisha, nikala Kisha nikajifungia ndani ,niakaanza kuandaa mkakati mzito wa kumshinda yule mganga. Mbinu niliyoitumia kuandaa bomu zito lenye kafara nzito ya manuizi yaliyoambatana na kufunga kwa siku 30.

Baada ya kuandaa lile bomu ,nikaliweka na ili lile bomu lipate nguvu zaidi ni lazima nijinyime Yani nifunge kwa siku 30.


Ndugu msomaji hakuna rahana kubwa Kama kumrahani mtu kwa maneno na kwa kufunga haswa kwa mtu ambae sio mchawi ,akifanyiwa mabaya ,Kisha yeye akaamua kumwomba Mungu kwa kufunga ili, Mungu amripize mbaya wake ,haisee dua hii ya maombi na kufunga ni hatari Sana.


Haswa kwa wewe ambae sio mchawi ,unaweza ukamrahani mbaya wako kwa kufunga siku 30 na kumnuizia maneno mabaya kila siku. Mfano wa maneno ya rahana ya kumnenea mbaya wako kila siku yanapatikana katika BIBLIA TAKATIFU  katika kitabu Cha ZABURI ya 109: 1- ........


Ila kwa sisi wachawi,kwetu ni tofauti huwa hatutumii biblia sababu inatudhuru,na wakati mwingine dua zetu huwa zinagoma pia.


Basi,siku zilizidi kwenda na hatimae ikafika siku ya ishirini na tisa. Nikajiandaa vya kutosha ili kesho yake mapema niende nikamlipue mganga Alumbile Kalumba. Niliamini kabisa kua nitashinda vita hiii,japo nilijua kua naenda kupambana na mtu hatari lakini nilijiamini na kujipa moyo.


Usiku ukafikia giza lilitawala kila kona.kama ilivyo kawaida,Usiku wa deni haukawii kucha. Kulikucha hasubui na mapema siku ya 30 ya mfungo wangu,nikajiandaa kichawi na kubeba kila aina ya dawa. Nikacheki kwenye rada yangu na kuona kua mazingira yanaruhusu kuondoka. Nikapotea Kama mware wa radi. Fyaaaaaaaaaa!!!!!


Nikaenda kuibukia nje ya nyumba ya yule mganga Alumbile Kalumba. Nikawa naangaza macho huku na kule kutazama usalama . Lakini kabla sijafanya chochote ,nikasikia sauti ya kiume ikinikaribisha ,kwa kua mbele sikuona mtu,nikageuka nyuma kutazama Kama kutakua na yeyote.lakini nyuma pia sikuona mtu.! Lakini pia ile narudisha shingo mbele ,nakutana uso kwa uso na Mganga Alumbile Kalumba akiwa na uso wa mnyama mbogo.


"Haa haa haaaa hahaha!"

Mganga alicheka Sana Mimi nikiwa namtazama.

" Karibu Sana Chuma, ujio wako ni Kama marehemu Bibi yako alivyo nijiaga. Na mwisho alifia hapa hapa. Wewe ni binti mdogo Sana halafu pia ni mzuri Sana ,hakika unafaa kua hata mke wangu. Hahaha hahaha!"


"Usinichekee mjinga wewe! Sikuja kwa masihara hapa ,leo ndio mwisho wako babangu huna pa kutokea."


"Chuma wacha kujidanganya na hako kasiraha chako ulicho kihandaa,huwezi kunihangamiza Mimi kirahisi hivyo! Bibi yako alishindwa akapotea na mama yako mkenya alishindwa akapotea. Sasa wewe bado mdogo Sana harafu ni mrembo Sana, hutakiwi kupotea na utamu wako. Cha msingi wacha hiyo tabia ya uchawi Kisha nikuoe tuishi maisha mazuri ya kiganga ."


Mganga alikua akiongea huku akinitamani maana nilikua uchi kabisa hivyo aliniona mwili na shepu na utupu wangu wote. Sijisifii lakini kiukweli nilikua Niko vizuri kwenye shepu japo sura si Sana. Yule mganga hakua na mke ndo maana ananirubuni lakini Mimi sikua na masihara hayo kwani nilienda kikazi kwani nilishafunga siku30 kwa ajili yake.


"We mbwa sikiliza Sina muda wa kupoteza,kabla hakujapambazuka vizuri,ngoja nikuoneshe."


" Hapana Chuma usifanye hiko unachotaka  kukifanya ,ni hatari Sana kwako nami napenda uishi I'll uwe wangu."


Mganga aliendelea kuongea lakini Mimi sikutaka kupoteza muda tena, nikamrushia kombora zito ,nililo liandaa . Mganga alilia Sana baada ya kukutana na pigo zito la mauaji. Alianguka chini na kupoteza fahamu.

Nikajua kua nimesha maliza kazi ,nikawa namsogelea ili kumkagua, lakini kilichonikuta baada ya kufika pale alipoanguka ilikua ni hatari zaidi kwangu.


Nilimkaribia pale alipoanguka nikainama ili nimguse au nimtingishe nione Kama ata amka. Nikamtingisha mwili wake,ghafla aka amka kwa kucheka Sana  mpaka nikahisi woga lakini pia nilijishangaa maana sikua na uwezo wa kufanya chochote kile. Niligundua kua hata miguu yangu ilishindwa kunyanyuka kabisa. Sikua na ujanja sijui ni nini alicho nitendea huyu mpuuzi.


" Hahaha , Chuma nilikwambia kua wewe bado mtoto Sana kwenye sekta hii, ona Sasa ,muda si mrefu nawe unakwenda kufa Kama wenzako walio tangulia. Nakuonea huruma maana bado binti huna hata mtoto mmoja. Kwaheri Chuma."


"Hapana mganga naomba Sana unisamee ,sitaki kufa mie ,nipe adhabu yoyote ile nitaifanya."


" Chuma huwezi tena kunipangia Cha kukufanya,ila una machaguo mawili tu na si vinginevyo, chagua moja,kufa au nikutoe uchawi Kisha nikuoe uwe mke wangu!"

 

Mganga alinipa sharti zito ambalo sikuwahi kutarajia kukutana nalo. Kiukweli alinitaiti kweli kweli,nami sikua tayari kufa Yani ni bora kuolewa ni Jambo la heri kuliko kufa kizembe wakati chansi ya kuishi ipo. 


" Nipo tayari mganga kuacha uchawi na kuolewa na wewe"


" Safi Sana Chuma karibu kwenye ulimwengu Safi wa maisha mapya."


Basi ndugu msomaji kuanzia siku hiyo niliacha uchawi na nikawa mke bora kwa mume wangu Alumbile Kalumba. Tuliishi vizuri na tulikuja kuzaa  watoto watatu. 


Kwa Sasa nipo Safi ,nimemrudia Mungu. Ndugu msomaji Uchawi ni mbaya Sana usije kushawishiwa kuingia kwenye chama hicho.  Asanteni πŸ™ na karibuni tena nyumbani kwetu kumenoga.

URITHI wa Bibi 14

 Story.......... URITHI WA BIBI EP.14


Author........ $teven Morgan.


πŸ“².............. 0659115223


ILIPOISHIA episode 13.

Tuliendelea kusubiri Kisha tukaroga ili mzee foya ajisikie kwenda chooni,mida ileile tulisikia sauti ya binti akilia kilio Cha ukweli na sio Cha mahaba ,yule binti akatoka mbio akatupita pale sebuleni bila kutuona akatoka nje huku akiwa amejifunga kanga moja ,akaondoka zake ,nasi tulienda hadi chooni kwa mzee foya na kumkuta ametoa macho huku damu zikimtoka puani. Tukajua kua tumesha maliza mchezo ,tulicheka Sana Kisha tukatoweka kurudi nyumbani.


.............. ENDELEA...................


Baada ya kurudi nyumbani nikiwa Mimi na mama mkenya,tulijipongenza kwa kazi nzuri tuliyo ifanya.

Baada ya hapo , nikachukua kioo changu Cha urithi alicho niachiaga bibi. Nikapiga Rada zangu ili nihakikishe kwa Mara nyingine Kama mzee Foya atakua amekufa kweli au lah?


Nikatazama kwa makini Sana ,lakini huwezi amini,mzee Foya nilimwona akiwa mzima wa afya kabisa !!! 


"Mzee Foya mzima! Inawezekanaje?"

Nilizungumza kwa sauti ya unyonge Sana.


"Mzima!!!"

Alishtuka mama mkenya.


Ndugu msomaji kiukweli wachawi wanapokutumia jini la mauaji chooni ,huwa kupona kwako kutategemeana na ukaribu wako na mwenye enzi Mungu.


Pia ndugu msomaji kiukweli amini usiamini ,kua Kuna watu hapahapa Duniani hawarogeki hata ufanyaje au hata uwe mchawi mkubwa kiasi gani utachemka tu!!

Kutorogeka kwao haina maana kwamba wamejikinga Sana kwa Waganga! Raha Sha! Bali watu hawa wasio rogeka huwa wanakua na urinzi maarumu walio wekewa na Mungu mwenyewe kabla hawajazaliwa au kutoka kwenye matumbo ya Mama zao . Huwa hawarogeki kabisa ,na ndo maana mchawi anaposhindwa kumuua mtu wa dizaini hii, hutumia majambazi ili kumuondoa mtu huyo Duniani.


Basi , ndugu msomaji,Mimi na mama yangu ,tulishangaa Sana kwa tukio like la mzee Foya kuendelea kubaki hai. Lakini pia kiukweli mzee Foya pia alikua ni miongoni mwa watu walio barikiwa na Mungu mwenyewe kuwekewa ulinzi maarumu,japo mwenyewe alikua hajijui,alikua akihisi kwamba dawa za mganga wake ndipo zinazo fanya kazi zaidi.


"Chuma naomba unipe muda wa lisaa limoja baada ya kutoweka hapa ,Kisha nitakupa mrejesho. Naenda kuandaa bomu la kushiba kutokea Kenya lililoundwa kwa uchawi wa kizamani,naamini mzee Foya hatoweza kuishi tena."


Mama mkenya aliongea kwa kumaanisha kwelikweli!! Kisha akaondoka kwa kutoweka ghafla . Nami nilikua nasikilizia huo muda wa mrejesho alio niambia mama mkenya niusubili.


Sikuamini Sana akilini mwwngu Kama mbinu na siraha ya Mama mkenya itatosha kumuangamiza mzee Foya,maana kiukweli nilisha gundua kua mzee Foya hawezi kurogeka hata kidogo.


Muda ulizidi kwenda masaa ya kutosha yalipita! Nilishangaa kutopata ripoti yoyote kutoka kwa Mama mkenya!! 


Nilihisi kua huenda kukawa na tatizo,nikampigia simu ya kichawi,lakini hakupatikana,nikampigia simu ya kawaida pia , hakupatikana!!


Na muda ulikua umeenda kweli,ilikua imeshafika saa kumi na mbili jioni. Bado sikuelewa kilichotokea au kumkuta Mama yangu mkenya!


Lakini kipindi nafikiria hayo,Mara ghafla nikapata ujumbe wa kichawi,kwamba muda huohuo nahitajika maari flani Kuna tatizo la kujadiri kwa dharula!


Ndugu msomaji,wachawi huwa wapo monitored Yani kwa lugha nyepesi unaweza kusema kua wachawi huwa wanaonganishwa kulingana na kamati zao ama kikundi Chao,na hupeana taarifa za haraka kupitia ishara maarumu . Ishara hiyo inaweza ikawa mlio maarumu wa ngoma au filimbi, nadhani wale walio pitia mgambo au skauti au jeshi ,watakua wananielewa vizuri hapa. Yaani huwa jeshini Kuna milio tofauti ya filimbi, na ukilia mlio fulani Basi ujue kuna watu flani wanna hitajika eneo flani ,huenda ikawa viongozi pekee ndio wanao hitajika,au wanajeshi wote wa kambini wanajitajika eneo flani kulingana na tafsiri ya filimbi. 


Basi ,hata sisi wachawi tupo hivyo pia. Kina mlio flani wa ngoma nilimsikia, ninaposema niliusikia ndungu msomaji, namaanisha kwamba hata Kama ningekua kwenye kundi la watu Mia,mlio huo ningeusikia Mimi tu,labda Kama kutakua na mchawi mwingine Kati yetu nae pia anaweza akasikia.


Baada ya hapo ,sikutaka kupoteza muda, nilijiandaa Kisha nikatoweka Kama nuru iliyo zidiwa na kiza kinene.


Ndugu msomaji wachawi huwa hukutana popote pale palipo pendekezwa kwa muda huo,huenda ikawa barabarani,au chini ya mti,au pembezoni mwa mto au makaburini au njia panda. Kokote pale wachawi huweka mkutano wao na muda wowote ule huenda ikawa asubuhi,mchana,jioni au usiku.


Ndugu msomaji ngoja nikupe faida ndogo, unapotembea barabarani Kisha ukapita sehemu flani na ukasimama  barabarani au chini ya mti ukapumzika,lakini baada ya muda ukaanza kuhisi Kama Kuna kundi la watu limekuzunguuka na nywele zako za mwili haswa kichwani zinasisimka,au jicho likaanza kukucheza bila lidhaa yako,ujue wazi kua ,eneo hilo ulilo kuwepo,kina kundi la watu wabaya wanafanya Yao, na unachotakiwa hapo ni kuondoka Mara moja eneo hilo Kisha muombe Mungu kwa ulinzi zaidi.


Basi,baaada ya Mimi kutoweka ,Kama kawaida nikaenda kuibukia kwenye kilinge chetu tunacho kutanaga siku zote.Nilikuta wachawi kibao wameshafika Yani Kama walikua wakiningoja Mimi tu!


"Karibu Chuma,tulikua tunakusubilia wewe tu! Najua kila mtu hapa anataka kujua nini nilicho wahitia ."


Aliongea mkuu. Lakini Mimi nolizidi kushangaza Jambo moja ambalo nilikua sielewi kbisa! Nilikua nikiangaza macho huku na kule lakini yule Mama mkenya,sikumuona kabisa.Nilikua na hofu Sana. Mara ghafla mkuu akaonge.


"  Chuma pole Sana kwa kumpoteza rafiki pia Kama Mama yako mkenya,hatupo nae Tena hapa Duniani!!! Na hivi Ninavyo zungumza,tayari ndugu zake huko Kenya wamesha mshtukia kua amefariki na wanaendelea na taratibu zao za msiba.!!


Kila mtu alishangaa Sana pia nami nililia Sana kwani iliniuma Sana na amekufa kwa ajiri yangu.Mkuu alizidi kuongea.


"Baada ya hapo,Chuma naomba nikushahuri Jambo moja kwamba,kwanza achana na mzee Foya kwanza,Kisha muanze kumuua mganga wake Alumbile Kalumba Kisha mzee Foya atakua mwepesi tu!"


Mkuu alionge bila kujua kua mzee Foya harogeki hata kidogo.


" Chuma msalaba huu wa kulipiza kisasi Cha Bibi yako utakua peke yako mwenyewe,sitaki uwaponze wengine kwaajiri ya nafsi yako.Jipange vya kutosha Kisha Anza kumdondosha mganga Alumbile Kalumba Kisha mmalizie mzee Foya ,sawa?"


Mkuu alinisisitizia.

"Sawa mkuu" 

Nilimjibu.


"Basi Kama tume elewana kila mtu atoweke mahara hapa Mara moja na muende mkaendelee na shughuri zenu nyumbani."


Mkuu alituruhusu Kisha kila mtu alitoweka kwa stahili yake,kurudi nyumbani. Wengine walitoweka Kama radi,wengine walitoweka Kama upepo ,Yani zilikua ni mbwembwe tu za kichawi katika kuonesha uwezo.


xxxxxxxxxxx Itaendele xxxxxxxxxxxx


Je,Chuma atawezaje kumuua mganga Alumbile Kalumba? Ikiwa Bibi yake alikua bingwa lakini aliuawa na Mganga Alumbile Kalumba!!!

Je , Chuma atawezaje kumuua mzee Foya? Ikiwa mbinu zao zimeshindikana mpaka mama mkenya amefariki!  Na Chuma amesha gundua kua mzee Foya harogeki,je atatumia njia gani?


USIKOSE KUFUATILIA SEHEMU YA MWISHO KABISA YA STORY YETU YA URITHI WA BIBI EP.15. [ MWISHO ]πŸ”Œ

URITHI wa Bibi 13

 Story........ URITHI WA BIBI EP. 13


Mtunzi........ Steven Morgan


πŸ“².............. +255 659 115 223


Karibu ndugu msomaji katika mwendelezo wetu wa story yetu tamu,ikiwa tunaelekea elekea mwisho kabisa.

Basi,Kama kawaida pale tulipoishia ndipo tunapo anzia.


ILIPOISHIA episode 12..


Mume wangu Sadiki alikurupuka bila kudai chochote kisha akachukua begi lake akalibeba mgongoni bila kunawa uso akaondoka. 

Alipokua barabarani nami nilimfuatilia nyumanyuma nikiwa kwenye hari ya kichawi ya kuto onekana na mtu wa kawaida. Niliona gari ndogo likija kwa Kasi upande ule ambao Sadi alikuwepo ,nilimzubaishasadi kichawi na kumpa kizunguzungu Cha ghafla,akajiingiza mwenyewe barabarani kwenye kumi na nane ,dereva alishindwa kumkwepa Wala hakupiga bleki ,alimgonga Sadi kwa Kasi ileile aliyo kua anakuja nayo!! 

Sadi alipezwa juu Kama karatasi akatua chini kwa kujipigiza kwenye Rami,alipasuka vibaya Sana !!!!   Kisha Mimi nikaenda kwenye mwili wa Sadi nikafanya yangu Kisha nikaondoka bila kuonekana na mtu.

Nilirudia nyumbani na kuendelea na shughuri zangu. Baada ya masaaa kadhaa ,taarifa zilinifikia na kila mtu alikua kua Sadi amepata hajari amefariki.mwili wa Sadi uliifadhiwa mochwari na ulichukuliwa na ndugu yake mmoja kesho yake Kisha ukasafirishwa kwenda kwao,Mimi sikutaka kwenda sababu sikutambulika na ndugu yake yoyote hivyo waliniona Kama  awala tu!


.............. Endelea.......πŸ”‹πŸ‘‡πŸ‘‡ep.13


Basi ndugu msomaji kiukweli Sadi  mpenzi wangu ,ndio tayari nimesha muweka ndondocha au Msukule kwa muda kabla ya kifo chake Cha ukweli.


Ndugu msomaji labda ulikua hujui tu,ila kiukweli mtu kabla ya kuchukuliwa Msukule huwa wachawi Kwanza wana andaa kisa ambacho baadae hugeuka mkasa kamili wenye ushahidi kamili machoni pa watu. 

Mfano Kama mpenzi wangu Sadi alivyo patwa na mkasa wa kugongwa na gari ,na watu walimuona  alivyo gongwa,hivyo kisa Cha Sadi kufa ni gari . Labda Kama utataka kujua ukweli harisi wa kifo Cha utata Kuna baadhi ya ishara mbalimbali unaweza kuziona eneo la tukio au kwenye mwili wa marehemu. Au una weza kwenda kwa mganga kuchunguza 

zaidi.

Sadiki nilimficha mvunguni mwa kitanda changu mpaka ule mwili wake wa uongo utakapo zikwa ndipo na sisi tunaanza kuutumia ule mwili wa ukweli ukiwa na nafsi yake iliyo hai.

Ndugu wasomaji ninaposema Sadiki nimemficha chumbani kwangu mvunguni, haina maana kwamba ,ukija kuingia chumbani kwangu na kupekua mvunguni ndio utaona chochote Cha kushangaza, kiukweli ukija na macho yako mawili ya wazi huwezi kuona chochote zaidi ya kuona kweupe tu!!! Labda uwe umechanjia dawa au uwe umepata upako  wa maono kutoka kwa Mungu mwenyewe zaidi ya hapo huwezi kuona chochote. Na unaweza kukaa na mtu mchawi chumba kimoja kwa muda mrefu na usione chochote kile ndani zaidi ya kuhisi .


Basi,siku moja hasubui nilitulia zangu nyumbani,Mara ghafla akatokea yule Mama yangu mkenya, alikuja kuniambia kua Usiku  wa siku hiyo natakiwa kumpeleka Sadi kilingeni maana siku zilishaenda Sana na miezi kadhaa ilipita .Hivyo , wanachama wenzangu walikua wanahitaji kula  nyama ya zamu yangu..

"Chuma leo ndio siku ambayo mkuu amenituma nije kwako kukupa habari kua umpeleke Sadiki leo akawe chakula chetu,maana kila mtu katika jamii anajua kua Sadi alisha kufaga muda"

Aliongea yule Mama mkenya.


"Sawa mamangu basi naomba leo tushinde wote hapa kwangu Kisha Usiku tuondoke wote."

"Usijari Chuma tupo pamoja ,ndomana nilichaguliwa kukusaidia."


Basi tulishinda wote nyumbani kwangu ,tulipika tukala , story nyingine ziliendelea.

Atimae Usiku uliingia tulikula kisha tukaanza kujiandaa mida ya saa mbili Usiku, 

Ndugu msomaji Mara nyingi mchawi huwa hujiandaa na Safari yake kuanzia saa mbili kamili usiku, na mchawi hana muda maarumu wa kuwanga  au kumchezea mtu,hata asubuhi au mchana mchawi anaweza kukuwangia au kukuchezea.

Basi tulijiandaa vya kutosha na yule Mama mkenya Kisha mida ilipofika ya Usiku wa wachawi tukaondoka kuelekea kilingeni,tuliwakuta wachawi wengi Sana walioanza kufika wakiendelea na utaratibu.

"Chuma bila kupoteza muda naomba tuletee mnyama wetu hapa , tuendelee na utaratibu wetu hapa."


Aliongea mkuu kwa kumaanisha kua nimlete Sadiki pale kwa kutolewa sadaka.Nami kwa kutumia maneno ya kichawi ya mamraka,nikamwita Sadiki kutoka kule chumbani kwangu mvunguni. Huwezi amini ndugu msomaji,ila kilichotokea ni Sadiki alitokea palepale kilingeni akiwa Kama zuzu.


Mkuu akanyoosha kidole chini πŸ‘‡ Mara ghafla! Akatokea mbuzi mkubwa wa kiume ( beberu) Kisha akaja mchinjaji akiwa ameshika bisu kubwa lenye makari Kama nyembe . Yule mchinjaji akamlaza mbuzi chali na kumshika miguu ya mbele,Mar ghafla! Sadiki pale aliposimama nae alianguka ,Kisha mchinjaji akaanza kumchinja yule mbuzi, mbuzi alilia Sana! Lakini pia nae Sadiki,alilia Sana huku mikono yake miwili ikishikilia shingo yake ili isidondoke au isidhurike kwa maumivu aliyo kua akiyapata.


Ndugu msomaji hakuna urogi mbaya Kama urogi wa mbuzi,Yani unapoona mbuzi anatolewa sadaka ujue,kuna Jambo zito linaenda kutokea .


Basi, mbuzi alichinjwa mpaka akafa,huku ulimi ukiwa nje,pia Sadiki nae ,alikufa huku ulimi upo nje na macho yalimtoka Kama fundi saa. 

 

Kamati ya chakula iliandaa msosi Yani nyama ya Sadi ,tukala na tulikunywa pia damu yake iliyo kingwa.


Ndugu msomaji najua unaweza kujiuliza swali moja ,kwamba ,kwa nini wachawi wanakunywa damu za kila mtu hata kama mtu akiwa na maambukizi ya virusi vya ukimwi ila mchawi anakunywa damu ya mgonjwa huyo na yeye hapati maambukizi yoyote,zaidi ya kuwa salama !!!!!!

Ndugu msomaji kiukweli, wachawi wanapokua katika maumbile yao ya kichawi huwa Kama wanyama na si watu,na ndomana huweza kula hata nyama mbichi kitu ambacho mwana Adamu wa kawaida hawezi. Kiukweli kile anachokula mchawi ,hari yeye bali mchawi hutumika Kama njia ya kuwashibisha mapepo au mashetani wanayo yaabudu.  Japo wanapokula radha ya chakula huisikia lakini wanao Shiba ni viumbe wengine. Hata chakula kingekua na sumu mchawi ana uwezo wa kula bila kudhurika .


Basi ,tulikula nyama na kunywa damu Kisha tukacheza ngoma za kikwetu kwetu. Baadae mkuu alionge.


" Ndugu zangu shughuri yetu imeisha kilichobaki Sasa,kila mtu apotee hapa arudi kwake akalale au Kama utataka kwenda kuwanga kidogo ruksa, ila naomba Chuma na mama mkenya mbaki hapa Kuna kazi nataka kuwapa."


Mkuu alipomaliza kutoa maagizo kila mtu,alitoweka isipokua Mimi ,mama mkenya na mkuu tulibakia kwa mazungumzo kidogo.


" Chuma ukisaidiwa na mama hapo, kesho mida ya saa Saba mchana,naomba muende kwa bosi wako mzee foya mkamroge ili afe ,ili ulipe kisasi Cha Bibi yako Mbokeleni ila mke na watoto wake msiwaguse hawana hatia. Baada ya kazi hiyo,kuna kazi ya mwisho kabisa ya kwenda kukabiriana na yele Mganga wa morogoro mgeta anae itwa Alumbile Kalumba."

"Sawa mkuu tumekuelewa"


Tulimuaga mkuu Kisha tukatoweka,ninaposema tulitoweka nadhani unaelewa ndugu msomaji Yani tulifutika Kama mwanga wa radi na kuibukia kwenye chumba changu,ilikua ni Usiku Sana bado. Tililala kuitafuta asubuhi.


Asubuhi ilifika ,tulioga Kisha tuka andaa chai tukanywa Kisha tukaanza kujiandaa na Safari iliyopo mbele yetu.

Mida ilizidi kwenda,tulishajiandaa kikazi, hatimaye saa Saba ikaingia! 


Bila kupoteza muda tukapotea na kwenda kuibukia kwa mzee foya nje ya nyumba yake,tukaangalia usalama ,tukagundua kua mke na watoto wa mzee foya pamoja na mfanya kazi wao hawakuwepo pale nyumbani ,walienda kula likizo nyumbani kwa mke wa mzee foya ila tulihisi kwa muda ule Kuna watu Kama wawili ndani chumbani kwa mzee foya.


Ndugu msomaji, tulitoweka tena na kuibukia sebuleni kwa mzee Foya,tulitulia kimya Mara tu ! Tukaanza kusikia miguno na sauti za mahaba kutoka chumbani kwa mzee foya ,nikatazama kiganja changu ,nikamwona mzee foya akiwa ana mla uroda binti mdogo Sana Kama wa kidato Cha nne hivi!!!


"Kumbe huyu mzee mshenzi namna hii?"

Aliongea yule Mama mkenya.


Baada ya hapo tukatoweka andaa mtego wa jini makata chooni kwa mzee foya  ambacho kilikuwepo kulekule ndani kwa mzee Foya Yani chumba chake kilikua ni masta. Tulilituma lile jini chooni kwake . Kisha tulitulia pale sebuleni kusikilizia mtego, mzee foya aliendelea kumgeuza mtoto wa watu Kama chapati huku binti akaendelea kutoa kilio Cha furaha kilicho changanyika na sukari ya zuchu.


Tuliendelea kusubiri Kisha tukaroga ili mzee foya ajisikie kwenda chooni,mida ileile tulisikia sauti ya binti akilia kilio Cha ukweli na sio Cha mahaba ,yule binti akatoka mbio akatupita pale sebuleni bila kutuona akatoka nje huku akiwa amejifunga kanga moja ,akaondoka zake ,nasi tulienda hadi chooni kwa mzee foya na kumkuta ametoa macho huku damu zikimtoka puani. Tukajua kua tumesha maliza mchezo ,tulicheka Sana Kisha tukatoweka kurudi nyumbani.


..............Itaendelea...................


Je,mzee foya atakua amekufa kweli?

Je,mganga Alumbile Kalumba wa Moro mgeta atawezekana? Usikose kufuatilia sehemu ya 14 ya URITHI WA BIBI.

URITHI wa Bibi 12

 Story....... URITHI WA BIBI EP.12 

Mtunzi..........Steven Morgan


WhatsApp..............+255659115223


Karibu tena kwenye mwendelezo wetu wa story yetu ya URITHI WA BIBI sehemu ya12. Najua nipo slow Sana ,Mambo ni mengi muda mchache . Watu wanataka kuburudika na kuelimika kwa kupata ufahamu wa Mambo mbalimbali kupitia story. Mambo mazuri hayahitaji haraka,Usinichoke , endelea kunifuatilia ili upate kuyajua Yale ambayo hukutarajia kuyajua kamwe.

 

Kama kawaida pale tulipoishia ndipo tunapo anzia:


ILIPOISHIA.....πŸ–‹️


"Mh! Jina gani hilo mzee wangu! Na kwanini likushtue hivyo?"

" Kijana wangu hilo jina ni lilikua ni la mfanya kazi wangu wa ndani,lakini kwa Sasa huyo mtu NI hadui yangu mkubwa,najua huko aliko Chuma wa morogoro Ndolelo, anataka alipe kisasi kwangu na familia yangu .Chuma ni mchawi Yani ni binti hatari Sana.!!!!"


" Mzee Foya, samahani kidogo ,unajua Chuma Mimi ni mke wangu,Na nilishaona  Mambo ya hajabu pale nyumbani,nahisi huenda akawa ndio huyohuyo binti unaye mzungumzia."


" Ndio huyo huyo bila Shaka,kijana,unatakiwa ujiongeze,japo Mungu yupo lakini unatakiwa ujiongeze raha sivyo utapotea."

" Sasa mzee wangu Mimi sielewi chochote Cha kufanya,nilishawahi kumshilikisha mchungaji ,lakini mchungaji alinishauli kumwomba mungu tu zaidi."

" Kijana mchungaji yupo sahihi kabisa , Mungu kwanza lazima umtangulize Kisha mengine ndio yanafuatia. Kama hutojari tafuta siku moja  baada au kabla ya kumaliza kazi yangu,nikupeleke kwa mtaaaramu mmoja yupo huko huko morogoro vijijini mgeta ,huyo anaitwa "Mganga Alumbile Kalumba" kiboko ya vibwengo wote,atakucheki na atakukinga dhidi ya hadui yako. Mimi mwenyewe mpaka Leo niko salama ,ni kwa  ajili yake japo Mungu ndio mkuu katika hayo.Nadhani umenielewa?"


"Nimekuelewa bosi wangu ,wacha nikafanye kazi tutaendelea kuwasiliana"


Endelea πŸ‘‡.

Basi , tukaendelea kufanya kazi na jamaa yangu Mwambe. Lakini nilikua na mawazo Sana juu ya Mke wangu Chuma.

Tulifanya kazi mpaka jioni,tulibakiza sehemu ndogo Sana ya kazi, bosi mzee foya alitugea nusu ya pesa ,tuligawana na jamaa yangu Mwambe Kisha tukaondoka.


Mimi nilishika njia yangu baada ya kuagana na Mwambe ,nilitembea kwa miguu kwa muda mrefu kwani , nilijisahau  hata kupanda gari,kutokana na wimbi zito la mawazo juu ya Mke wangu Chuma.Nilipokuja kushtuka nilijihisi maumivu ya miguu,ndipo nilipopanda gari ili niwahi nyumbani maana giza lilishaanza kutanda.


" Hodi hodi mke wangu!"

Kimya.

"Hodi hodi mke wangu Chuma!"

Kimya.

"Uuuwiiii! Jamani! Kuna mtu ndani huku?"

 

Nilipiga Sana hodi lakini sikuona dalili yoyote ya mke wangu Chuma kuitika au kufunga mlango maana nilishika kitasa na kugundua kua mlango ulikua umefungwa .

Nilishangaa lakini dakika ileile nikiwa nipo pale nje mlangoni mwa chumba changu,nilianza kuhisi kizunguzungu kikali Sana,mpaka kichwa kikaanza kuuma,nilianguka pale pale mlangoni kwangu chini puuuuu! Nilipoteza fahamu sikujua Tena kilicho endelea muda huo.


"Hahaha hahaha hahaha aaaa!, Ongera Sana Chuma, unatakiwa kua makini Sana na vita iliyopo mbele yako."

"Asante Sana mamangu kwa msaada wako wa kua bega kwa bega na Mimi."

"Usijari Chuma tupo pa moja ,kwa Sasa ngoja nikuache najua unajua nini Cha kufanya ."

Mama yangu yule mkenya aliniaga Kisha akapotea Kama mwale wa radi. Muda huo tulikua tupo palepale chumbani,hata mume wangu Sadi alipokua akigonga hodi tulimsikia,ila sikutaka kumfungulia sababu tulikua kwenye Mambo yetu ya Siri. Hivyo niliamua kumroga na kumzima ufahamu.

Nilimchukua mume wangu kichawi kutoka pale nje alipoanguka na kuja ndani mpaka kwenye Kochi bila ya yeye kujijua.

Muda huo nipo kwenye gwanda la kichawi,nilijua mipango yote aliyo panga mume wangu Sadi kupitia kiganja chake,nilitambua kua alionana na hadui yangu mzee foya na kupanga kwenda kwa mganga Alumbile Kalumba ambaye ndie Alie muua Bibi yangu Mbokeleni,au Bibi Chuma. 

Ndugu msomaji kumsoma mtu na kujua dhamira yake na mipango yake ya baadae ni elimu ndogo Sana ambayo si uchawi bali ni utaaramu ambao hutumiwa hata na wanajimu au watabiri wa nyota. 

Ningependa kuelekeza hapa lakini hii ni ishu nyingine ila nitamwomba ndugu mwandishi siku moja baada ya kumaliza story hii,nitakuja na somo la fomula maaarumu kwaajili ya kusovu Mambo madogo madogo bila kwenda hata kwa mganga. Na nitamwomba afungue group la WhatsApp kwa ajiri ya somo hilo.


Basi turejee ,kwenye story yetu, mume wangu alionekana kulala usingizi kabisa,ilikua imeshafika saa mbili kasoro Usiku. Nikatenga chakula mezani maana nilijua kua mume wangu ana njaa Sana.

Nilipomaliza kutenga chakula ,nilimuamsha . 

"Mume wangu amka kutoka kwenye usingizi batiri!"

Nilimuamsha mume wangu kwa sauti ya mamraka ya Lusifa. Nae aka amka kwa kushtuka ghafla huku akivuta pumzi Kama mtu Alie kua amekabwa.

" Nipo wapi hapa?"

"Jamani mume wangu si upo nyumbani hapa kwa mke wako Chuma?"

"Mbona sikumbuki niliingia muda gani humu ndani mke wangu! Nini kimenitokea?"

Mume wangu aliendelea kuniuliza maswari! Lengo langu la kumrudishia ufahamu ,ili aweze kula chakula kwa raha.Lakini naona mwenzangu anazidi kuniuliza maswari ya kushangaza.

Ndugu msomaji ngoja nikupe ufahamu kidogo ,siku zote mtu alie tolewa ufahamu kichawi, hata akila chakula hawezi kukiona kitamu Kama wewe unavyo kiona. Mtu alie tolewa ufahamu hawezi kuhisi kichefuchefu Wala hawezi kuhisi uzuri au ubaya wa chakula . Aliye tolewa ufahamu ana uwezo wa kula hata mavi bila kinyaa,lakini wewe mwenye ufahamu wako huwezi kula hivyo. Mfano mtu Alie wekwa Msukule au ndondocha ,huyu nae ametolewa ufahamu ,ana uwezo wa kula chochote kibichi au kimewiva,kichafu au kisafi,pia wanakula mpaka unga wa ugal au pumba za maindi Kama nguruwe bila kujisikia kichefuchefu.  Hi yote ni kutokana na kuzimwa kwa ufahamu ambao umebeba sensa muhimu za mwili.


Ok,tuendelee Sasa na story yetu, kiukweli sikutaka mume wangu Sadi ale chakula akiwa kwenye hari ya kutokua na ufahamu sababu najua madhara yake Kama hayo niliyo yaeleza hapo juu.


" Mke wangu nini kimenitokea Mimi au ndio unaniletea ...... unaniletea.....!!!" Mume wangu Sadi kwakua fahamu zake zimerudia ameanza kuhisi Mambo flani kwangi.

"Nakuletea nini tena mume wangu hebu kula kwanza."

"Si unaniletea uchawi wako siwezi kula hiko chakula chako mchawi mkubwa wewe!!"

Duh! Mume wangu akaanza kunisanukia kua Mimi ni mchawi. Lakini kabla sijamjibu chochote mara ghafla akaja mkuu wetu wa uchawi akiwa katika umbo la kutisha Sana,na akajionesha kwa kila mtu pale ndani ,Yani jinsi alivyokuja hakujiweka paswadi za kuto onekana na mtu wa kawaida,hivyo hata mume wangu Sadi alimuona pia mkuu wangu kwa urahisi.

" Chuma kwa nini unamlembea mtu mwenye kiburi? Maliza kazi Sasa hivi!"


Wakati mkuu anaongea hayo,. Sadiki mume wangu alishazimiaga muda,kwani hakuweza kudumu kumtazama mkuu Alie kua anatisha Sana. Hata wewe ndugu msomaji ungekuwepo nadhani,ungekua wa Kwanza kuzimia au kufa kabisa.


Ndugu msomaji unajua kua mwili wa mwanadamu umeumbwa na kuwekewa mipaka maarumu katika utendaji wake wa kazi mfano kutazama na kuona,mwanadamu kawekewa mipaka , unaweza ukawa na uwezo wa kuona na kutazama vitu vidogovidogo vya kutisha lakini siku moja ukikumbana na kitu kinachotisha zaidi ,mafaili na system ya ubongo hushindwa kufanya kazi hatimaye mtu huyo anaweza kupoteza fahamu au kufa kabisa! Ili uweze kuona vitu vya kutisha zaidi bila kudhurika inakubidi uwe na utukufu zaidi au inakubidi uwe na Roho ngumu Sana na uji update vya kutosha.


Mume wangu alikua na Roho nyepesi Sana ,alizimia!!,

Kwakua mkuu ameniamuru kumaliza kazi bila kulemba muda uleule ,sikulaza damu nilimkata Sadi kichawi,kwa ajili ya kafara .Namaanisha nilimchukua Msukule Sadiki kwaajili ya kafara.

Mkuu alifurahi Sana.

" Chuma hongera , nadhani unajua nini kinacho fuatia ,kwaheli tuonane badae kidogo kilingeni."

Mkuu aliniaga Kisha akaondoka . Mimi nilimchukua Sadi nikawafanya wakawa wawili Kama mapacha Yani nafsi iliyo hai niliichukua na mwili wa kufoji niliuweka kitandani ukiwa hai Ila ulikua haujielewi.

Nilingoja ifike hasubui ili nitengeneze kisa kabla ya mkasa. Mida ilizidi kwenda ,Usiku ukakomaaa,nilienda kilingeni kuonana na mkuu,ndugu msomaji kilingeni ni sehemu yoyote ambayo watu wowote wanaweza kukutana kwa pamoja na kufanya wanayo fanyaga Kama kucheza draft,kucheza usoro au karata au kupiga story. Lakini sisi wachawi kilingenikwetu,tunakutana pia kwa ajiri ya Mambo yetu na dharula.


Basi ,mkuu aliniamuru nitengeneze kisa ambacho kila mtu katika jamii ataamini kua Sadi kafariki kihalari ! Au bahati mbaya.

Nikatengeneza ajari ya kichawi ili kesho nimbabatize Sadi akiwa kwenye mwili wenye nafsi mfu. Baada ya kumaliza nikaondoka kurudi nyumbani,nilimkuta Sadi amelala fofofo.

Asubuhi ilipowadia rafiki yake Sadi walio enda kufanya kazi wote Jana alipiga simu. Simu iliita niliitazama nikaona jina la Mwambe, mara ghafla Sadiki mume wangu akashtuka usingizini na akachukua simu na kuipokea .

" Halloo mwambe,haisee nakuja Sasa hivi rafiki yangu,nimechelewa Sana kuamka,nakuja Sasa hivi!"


Mume wangu Sadiki alikurupuka bila kudai chochote kisha akachukua begi lake akalibeba mgongoni bila kunawa uso akaondoka. 

Alipokua barabarani nami nilimfuatilia nyumanyuma nikiwa kwenye hari ya kichawi ya kuto onekana na mtu wa kawaida. Niliona gari ndogo likija kwa Kasi upande ule ambao Sadi alikuwepo ,nilimzubaishasadi kichawi na kumpa kizunguzungu Cha ghafla,akajiingiza mwenyewe barabarani kwenye kumi na nane ,dereva alishindwa kumkwepa Wala hakupiga bleki ,alimgonga Sadi kwa Kasi ileile aliyo kua anakuja nayo!! 

Sadi alipezwa juu Kama karatasi akatua chini kwa kujipigiza kwenye Rami,alipasuka vibaya Sana !!!!   Kisha Mimi nikaenda kwenye mwili wa Sadi nikafanya yangu Kisha nikaondoka bila kuonekana na mtu.

Nilirudia nyumbani na kuendelea na shughuri zangu. Baada ya masaaa kadhaa ,taarifa zilinifikia na kila mtu alikua kua Sadi amepata hajari amefariki.mwili wa Sadi uliifadhiwa mochwari na ulichukuliwa na ndugu yake mmoja kesho yake Kisha ukasafirishwa kwenda kwao,Mimi sikutaka kwenda sababu sikutambulika na ndugu yake yoyote hivyo waliniona Kama  awala tu!


.............. Itaendelea..............

............... .................. ..............

................ ................ ...............

URITHI wa Bibi 11

 Story............ URITHI WA BIBI EP. 11

Mtunzi ........Steven Morgan.

Contact......................+255659115223


Naam kwa mara nyingine tena Mungu yu mwema, tumekutana tena ndani ya story za Morgan, bila Shaka ndugu wasomaji wangu mu Wazima wa afya!!

Bila kupoteza Muda tunasonga mbele na hiki kigongo chetu Cha URITHI WA BIBI EP. 11 . Tukiwa tuna karibia mwishoni mwishoni . Staki nikuchoshe na story ndefu zisizo julikana zitaisha lini!!


Basi Kama kawaida, pale tulipoishia,ndipo tunapoanzia.                            


ILIPOISHIA EP.10

IKaribu ndugu Sadiki,unaweza kuketi hapo, mmhmm! Bila Shaka nakumbuka nilikutana na wewe kule barabarani na nikakosakosa kukugonga na gari langu ,si ndio?"

"Bila Shaka mchungaji!"

"Sawa kabisa na ulinielezeaga tatizo lako na mkewe kuhusu uzazi vipi ! Uliishia wapi ? 

" Tulienda hospital na mke wangu tulipima ,lakini Cha hajabu! Wote tukaonekana hatuna tatizo,Yani wote ni wazima,ila dokta ametushahuri tu tumwombe Mungu tu maana yeye ndie anae toa!!

"Mh!  Sawa ndugu sadii,Mungu pekee ndie anaye toa na ndie anaye twaa,umekuja sehemu sahihi tatizo lenu litakwisha "

"Amen mchungaji! Lakini ukiachana na hilo mchungaji, Kuna Jambo lingine linanitatiza Sana"


Nilimuelezea mchungaji kila kitu kuhusiana na ile ndoto na ile siku narudi nyumbani na kusikia mke wangu anaongea na mtu Kisha baadae baada ya kuingia ndani anasema alikua ni yeye tu na tv pekee.

" Sadiki upo kwenye hatari kubwa sana,tena ni hatari ya kufa,inaonekana Kuna hadui anakufuatilia,na ameshaanza kukushambulia, na hadui huyo hayupo mbali ,yupo ndani kwako."...................


          ENDELEA...............

Sadiki upo kwenye hatari kubwa sana,tena ni hatari ya kufa,inaonekana Kuna hadui anakufuatilia,na ameshaanza kukushambulia, na hadui huyo hayupo mbali ,yupo ndani kwako."...................


Nilishtuka Sana ! Baada ya mchungaji kuniambia kua nipo kwenye hatari kubwa!


" Sasa ,wacha tusali Kwanza ili tulikemee Jambo hili baya linalotarajia kukudhuru"


"Sawa mchungaji!" Nilimjibu mchungaji kua niko tayari kwa maombi muda huo.


"Baba katika jina la Yesu Kristo,namkabidhi kwako kijana  Sadiki, umuwekee ulinzi ulio imara,malaika wote wenye nguvu wamzunguuke kila aendapo , Roho zote Safi ziwe upande wake ,zimlinde dhidi ya hadui anae mkabili. Ee ,Mungu baba ,jidhihirishe kwa kijana huyu ili apate kuamini uwepo wako na aweze kuokoka na kulitangaza jina lako. Baba tunaomba na kushukuru katika jina la Yesu Kristo.Amen."


"Amen." Niliitikia baada ya mchungaji kuniombea. 

" Sadiki Sasa upo salama,ila Jambo la msingi ,usiache kulitaja jina la Mungu baba na Yesu kristo katika kila Jambo haswa unapohisi hari ya hatari."

"Sawa mchungaji nimekuelewa"

" Karibu Sana Sadiki ,juma pili unaweza ukaja kwa ajiri ya ibada ya pamoja ,lakini pia unaweza ukaja na mke wako ,pia unaweza kuniharika nyumbani kwako kwa ajili ya ibada."

"Sawa mchungaji,nitakuharika siku moja uje nyumbani"

" Asante Sadiki karibu tena! "


Niliagana na mchungaji Kisha niliondoka kuelekea nyumbani. Lakini kipindi nipo njiani nilijiuliza maswali mengi Sana ! Wakati mwingine nilihisi kua huenda mpenzi wangu Chuma akawa sio mtu wa kawaida. Kibaya zaidi nikakumbuka kipindi kile Cha mwanzo nilipokutana na Chuma kule baa ,alinileteaga masihara kwa kusema eti yeye ni jini!! Nilijua ananidanganya kwani jini hawezi kula chakula Kama kile alichokua anakula yeye pale! Lakini kauli yake ya kusema kua yeye ni jini! Wakati mwingine nikilinganisha na haya Mambo ninayo yaona ,nahisi kabisa Kama Chuma sio jini,basi atakua ni mchawi!!!


Nilikua bado nipo barabarani nikiongea peke yangu Kama chizi,nimesahau kabisa hata kupanda gari ,nikawa natembea tu kwa mguu kutoka segelea kuelekea buguruni!!!  Nilipokuja kushtuka! Nilishafika mbali Sana,kwakua nilichoka Sana kutembea,ilibidi tu nipande gari.


Nilifika nyumbani nyakati za saa kumi jioni .

" Karibu mume wangu,Mbona umechelewa Sana ! Ulikua wapi?"

"Swali gani Tena hilo mke wangu? Si nimetoka mihangaikoni? Mimi kazi zangu ni za kutafuta Yani day worker. Kwa hiyo kurudi nyumbani mapema inategemeana na muda nilioanza kufanya kazi."

"Sawa mme wangu lakini Mimi nimeuliza tu! Wala si ugomvi!"

"Usijari mke wangu,"

"Sawa ,haya Nenda ukaoge Kwanza maji tayari yapo hukohuko bafuni ,sawa mume wangu?"

"Nashukuru mke wangu wacha niende nikaoge Kisha niandalie msosi kabisa maana Nina njaa Sana"


Sadiki alienda kuoga bafuni. Bila kupoteza muda,nikahisi Kuna Jambo linaendelea ambacho Mimi silijui. Nikaenda chumbani nikachukua kile kioo changu Cha kichawi,nikaanza kumfuatilia mume wangu tangia anatoka nyumbani ,watu alio ongea nao barabarani , maongezi yao waliokua wakiongea, mwisho wa Safari yake niliona kua alienda kanisani kwa mchungaji, maongezi yao waliokua ,wakiongea yote niliyasikia.Hivyo nikahisi kabisa kua huenda mume wangu ameanza kunishtukia ila sio Sana. Nikarudisha kioo changu. Mara ghafla!!

Mume wangu Sadi aliingia ndani!

" Haaa! Yani Mimi nilifikiri ,umeshanitengea msosi mezani,sijui ulikua unafanya nini Sasa!!!"

"Mume wangu ,si ubadilishe hizo nguo Kwanza? Wacha gubu bana msosi upo kabatini nakuekea Sasa hivi"


Mume wangu alibadilisha nguo Kisha akaja pale mezani ,akataka tule wore chakula huwa hapendi kula peke yake,hata Kama Mimi nimeshiba atanifosi nile nae tu! Tukawa tunakula huku story za hapa na pale zikiendelea.

Mara simu ya mume wangu ikaanza kuita  kwenye mfuko wa kushoto wa suruali yake. Akaitoa na akapokea simu.


"Halloo mwambe! Mambo vip rafiki yangu,naona Sasa hivi dili zako unapiga mwenyewe hatushtuani kabisa!!"

"Sasa si ndio maana nimekupigia simu rafiki yangu ili nikujulishe kua Kuna dili nimelipata la kujenga mabanda ya kuku kwa mzee mmoja wa kichaga hapahapa dar es salaam. Kama una nafasi kesho uje ili twende "   

" Sawa mwambe Mambo si ndio hayo Sasa,kesho mapema tu ntakupigia simu"


Mume wangu alimaliza kuongea na simu Kisha akakata Kama alipiga yeye vile! Kisha akaendelea kula.

" Mke wangu dili hili tayari ,kesho mapema naenda kuanza nalo" 

"Safi Mungu ni mwema"

Tulimaliza kula Kisha ,tukawa tunaangalia filamu za kibongo , mpaka Usiku uliingia ,tulikula Cha Usiku tukawa tutaendelea kuweka CD na kuangalia muvi.

Ilishafika saa tatu na nusu Usiku, mume wangu akachukua CD moja ambayo haijajulikana ni cd ya aina gani,akaiweka ili tuitazame,kumbe ! Ilikua ni CD ya kibongo pia ! Lakini ilikua ni ya kichawi! Ilikua inaitwa " Mkoba wa babu"  inatisha Sana wakati mwingine niliogopa!!

" Aaah! Bana kumbe hata wewe unaogopa Mambo haya?"


Mume wangu aliniuliza.

"Ndio ,kwani nisiogope Mimi nimekua nani?" Nilimjibu.

"Si unakumbuka mwanzoni kipindi kile tulivyokutana kule baa,uliniambiaga kua wewe ni jini,Sasa Mbona unaogopa kutazama Mambo haya tu,ya kuigiza?


Aliendelea kuniuliza mume wangu Sadi ,sijui alikua na maana gani .

"Nilikudanganya tu! Ili usinisumbue uniogope ukae mbali nami! Sema tu ulikua king'ang'anizi Sana wewe! Eti ,ulikua unantaka hivyo hivyo hata Kama ningekua jini!! Shauri yako siku utakuja kulitongoza jini kweli litakuua!"

Nilimjibu mume wangu.

"Thubutuuuu!!! Kuniua haiwezekani labda hilo jini lipate ruksa kwa Mungu zaidi ya hapo atakufa yeye!!"

"Mmh! We mume wangu nawe kwa kujigamba sijui unachoringia ni nini! Mpaka jini akushindwe wewe kukuua?"

"Wee! Mimi naringia kuwa karibu kabisa na Mungu wangu pamoja na Yesu kristo wa Nazareth.Hakuna wa kunisumbua"


Basi ile sinema ilikua ikiendelea ,mume wangu aliitazama kwa umakini lakini Mimi nilikua nakwepesha macho kwenye vipande vilivyokua vinatisha. Story zikiendelea lakini wakati mwingine nilikua  naingiwa na hasira pindi tu ! Mume wangu anapolitaja jina Yesu Na Mungu baba. Ndugu msomaji jina la Yesu ni dawa na kinga ya kweli kwa wenye imani nalo.Ni kweli jina la Yesu lina nguvu kushinda majina yote unayoyajua wewe . Hili ndilo jina pekee la uponyaji. Nadhani Kama wewe ni mlokole tutakua tunaelewana vizuri hapo! 


Basi Usiku ulizidi kukolea Kama chumvi ya mawe, mume wangu akapitiwa na usingizi akalala palepale kwenye Kochi,sikutaka kumwamsha nilimwacha palepale! Mara ghafla! Nikasikia kishindo kikubwa juu ya bati " kwapuuuu!!!" Nilishtuka kiubinadamu lakini nilijua kua ni nini, kinachoendelea.

Mara , akatokea yule mmama mkenya ,pale chumbani akasema ," Mbona unachelewa Sana kujiandaa wewe! Muda ndio huu twende zetu " 

"Nilikua na mume wangu muda mwingi nilijisahau kwa kweli ,samahani ila,tumfanyize mtu wa bandia abaki hapa kitandani badala yangu ili mume wangu akija huku chumbani ajue kua nipo nimelala asishtuke."


Basi,tukamfanyiza mtu wa bandia Alie fanana na Mimi ili alale pale kitandani badala yangu kipindi ambacho Mimi sipo pale kitandani.Tukamlaza yule mtu pale kitandani.  Hapa naomba nieleweke hivi,nikwamba mchawi anapotaka kuondoka Usiku Kama yupo na mumewe au mtoto, Basi mchawi huamua kutengeneza kopi yamwili wake ubaki pale kitandani ili mume au mtoto akiamka ,asijikute kua yupo peke yake na kujiuliza maswali, ndo maana huacha ile kopi ili aonekane yupo kumbe hayupo.

Na ule mwili wa bandia unao bakia pale kitandani,hata uutingishe kiasi gani hauwezi kuamka Wala kuongea,japo unaweza ukauona Kama mtu tu ,amelala na anapumua ila ukiuamsha hauwezi kuamka kabisa Wala kuongea kutokana na kwamba ule sio mwili wa kweli kiukweli, ule mwili unaweza kua ni mgomba,mchi au kinu!!!!


Basi , tuachane na hayo ,mimi na yule Mama mkenya, tukafanya yetu Kisha tukatoka nje kichawi,Kwanza tuliwachawia wapangaji wenzangu wa pale ,haswa wale wanao jifanya kula wali nyama,samaki kila siku,niliwasotea kweli kweli. Ndugu msomaji kwa wale mnao ishi nyumba za kupanga ,jaribuni kua wastaarabu ,wakati mwingine usitake kila mtu ajue umepika nini,pia usiwe mwema Sana sababu kwa wema wako huohuo, Kuna watu wanateseka!! Na si kila unae msaidia ni mwema kwako wengine ni wabaya Sana japo unawasaidia lakini bado watakuona Kama unaringa na watautumia wema wako Kama sampo ya kukushusha. Yani Kama ulikua unatoa Sasa utapokea! Yani Kama ulikua unasaidia masikini Sasa wewe ndo utakua ombaomba. Na hii ndio ubaya wa uchawi Yani watu wema na wazuri wasio kua na hatia ndio wanao andamwa bila sababu za msingi,ni ujingaujinga tu!!!


Basi tuliendelea kuwachawia wapangaji Kisha tukapotea Kama upepo unaovuma na kutulia ghafla, tukajikuta tupo kilingeni Yani kwenye makutano ya wachawi .Tulikuta wachawi wengi Sana kilingeni, wakiendelea na shughuri zao za kichawi .mkuu akaniambia kua ni kwanini bado sijakamilisha suala la utoaji wa sadaka.?

Lakini Mimi nilimjibu kua ,nimeshaweka mtego na tayari mhusika yupo kwenye kalenda ya kifo!

" Sawa Chuma kua makini Mambo yasije kua tofauti!". "sawa mkuu" nilijibu.

" Lakini Chuma unatakiwa Sasa ,umuite huyo mhusika kwanza hapa kilingeni ,umpige ndumba Tena Kisha leo umtangulize mbele kwenye kuwanga kwako huko mtaani haswa kwa jamaa zake huyo mhusika ."

Kama kawaida kwa maneno ya mamraka yasio pingika nikamuamuru Sadiki wangu atokee pale kilingeni , akatokea akiwa anashangaa shangaa! Lakini hakuna anachokielewa, nikampiga ndumba tena kwa kumnuwia mabaya mikosi na nuksi zote zikawa upande wake.


Basi,baada ya hapo,nilimwacha yule Mama mkenya pale kilingeni Mimi nilimchukua Sadi ,nikamtanguliza mbele ,yeye ndio akawa dereva anaye jua njia. Nikamuamuru twende kwa yule rafiki yake Mwambe aliye mpigia simu kua kesho Kuna dili la kujenga ,mabanda ya kuku . Tukaenda mpaka kwake tukaingia ndani , Sadiki akiwa mbele hajitambui kua anawanga kwa niaba yangu. Tulimwangia Sana Mwambe lakini kibaya zaidi Mwambe alishtuka ghafla usingizini na akamwona Sadiki.


"Sadiki!,Mbona si hamini macho yangu,kumbe wewe ni mwanga ?"


Mwambe alijiuliza maswali lakini hakuna wa kumjibu Wala kumthibitishia hilo Jambo aliloliona kua ni ndoto au ni kweli?

 Wakati anajiuliza hayo maswali Mwambe ,sisi tulipotea chapu na kuibukia nje ya nyumba,nikacheka Sana tena sana Yani Kama vile ninavyo fanya ni vizuri kumbe ni ujinga tu!! Sauti ya kicheko ilikua ni kubwa sana lakini kwa mwanadamu wa kawaida huwezi kuisikia sauti hiyo katika uharisia wake. labda,Kama utaisikia sauti hiyo,basi utahisi ni sauti ya ndege wa hajabu,au mnyama wa hajabu,au unaweza kusikia wimbo unao ujua unapiga katika kichwa chako Yani ni Kama unaimba kimoyomoyo.  Ujue hapo Kuna mtu mbaya anapiga kelele ,Kama sio cheko  basi anaimba nyimbo ya kichawi.


Baada ya hapo tukatoweka ,tukarudi nyumbani,Sadi nilimlaza kitandani,Kisha nikaupoteza ule mwili wangu wa bandia pale kitandani. Nikajiweka sawa Kisha nami nikalala.

⛅ Asubuhi ikafika ,nikaamka mapema Kama mwanamke ,nikaandaa chai , nikaandaa maji ya kuoga pia. Mume wangu alichelewa Sana kuamka ,aliamka saa mbili na robo .

"Dah! Mke wangu ,kwa nini hukuniamsha mapema wakati unajua wazi kua leo ,Kuna dili natakiwa niende nikafanye nipaye pesa?"

"Mimi mwenyewe nilijisahau mme wangu , samahani" nilikua mnyenyekevu Sana kwa mume wangu.

"Sawa wacha nkaoge niondoke zangu"

Sadi alienda kuoga Kisha akarudi nikamtengea chai akanywa . 

"Asante mke wangu kwa chai,wacha niende kibaruani,japo leo najihisi nimechoka kweli sijui naumwa?"

"Hapana mume wangu ,huo ni uchovu tu, umelala Sana umechelewa kuamka ."

" Sawa Chuma wacha niende"

Mume wangu aliniita kwa jina langu, mara ghafla simu yake ikaita. ( Tilililii, tilililii, tililililiiiiiix2 )

"Halloo mwambe,nakuja Sasa hivi mtu wangu"

" Wahi rafiki yangu ,muda umeenda sana bosi amenipigia simu,alafu Kuna Jambo lingine nataka nikueleze ukweli maana naona umeanza kunipanda kichwani,najua nikikukaushia siku nyingine utanipanda hata matakoni wewe!"

" Mwambe Mbona sielewi unachokiongea? Hebu ngoja nije Kwanza utanielezea vizuri"

 Mume wangu sadi nilimsikia akikwaruzana kidogo na jamaa yake Mwambe ,Mimi nilijua kinachoendelea.Basi mume wangu akaondoka. 


Hodi hodi!  " Nanii?" " 

Nani ugomvi bana ! Njoo nje huku ,Mimi Sadi.

"Aaah! Ngoja nije "

Mwambe akatoka nje na vifaa vya kazi ,nikavichukua na kuvibeba ,bila kupoteza muda tuliondoka kazini.Tukiwa njiani .." eheee rafiki yangu Mwambe, vipi Mbona sijakuelewa ulicho kizungumza kwenye simu kwa ukali ,kwani Kuna nini?" 

" Sadiki sijui nianzie wapi lakini wacha twende kazini Kwanza nitakueleza hukohuko"

"Ok sawa "

Mwambe hakutaka kuniweka wazi kabisa , kiukweli aliniweka kwenye mawazo kua hiyo ishu inayomkwaza yeye ni ipi? Na maimi Sadi nahusika vipi ? Nikawa Sina raha kiukweli.


Mara tukafika baada ya kusafiru kwa gari kwa umbali fulani, tukatembea kidogo tukaingia kwenye nyumba moja kubwa ya kisasa, tulikaribishwa na mdada alionekana kua ni mdada wa kazi .Akatuitia bosi, na bosi akatoka akiwa na mkewe na watoto zao wakubwa wawili ,wa like na wa kiume,tukasalimiana Kisha mama mwenye nyumba akarudi ndani na wanae,  Bosi akatuchukua na kutupeleka nyuma ya nyumba yake .


Akatuonesha eneo la kazi ,vifaa na kila kitu,tukapatana being ya kujenga Banda lile ni laki mbili. Bosi akachukua kiti na gazeti akakaa pembeni akituangalia sisi tunavyoendelea na kazi.


Tukapima ,Kisha nikaaanza kuchimba mashimo kwaajili ya nguzo. Mara Mwambe akaanza kuongea.

" Eheee!, Sasa jamaa yangu ,wakati tutaendelea na kazi ,wacha nikwambie kile ulichonikela, hakuna kugombana hapa tuwe Kama tunaongea tu hapa" 

"Sawa mwambe letter habari!" Wakati huo huku kaz zinaendelea.


" Hivi Sadiki! Katika maisha yako ulishawahi kua mchawi,au unaujua uchawi?"

"Mh! Kwakweli siujui huo uchawi na Wala sikuwahi kua mchawi na sitarajii kua mchawi, sijui kwanini umeniuliza hivyo Mwambe?"

*Sadiki nimekuuliza hivyo kwa makusudi na Kama nilivyokwambia sitaki hapa tugombane ,tunaelekezana ili tujue nini kinaendelea"

"Nakusikiliza Mwambe endelea!"

" Sadiki bana wewe ni mchawi!! Na sijui huo uchawi umeuanza lini! Na Jana Usiku nilikuona kwa macho YANGU ,ndani kwangu ulikuja kuniwangia,na Mimi hua napenda kumweleza mtu ukweli.samahani Kama nitakua nimekukasirisha!!"


Mwambe aliongea kwa sauti kubwa tu ,kiasi ambacho yule bosi alikua akitusikia tukiongea.


" Mwambe Mimi sikupingi mawazo na maono yako,ila kiukweli Mimi si mchawi Kama unavyo fikiri labda kutakua Kuna namna ,Yani Kuna mtu ananichezea.Maana kiukweli rafiki yangu Mimi mwenyewe wakati mwingine nashindwa kuelewa hata shemeji yako nyumbani,nashindwa kumuelewa ,Yani ana Mambo ya hajabu Sana."


" Sadiki Kama ni hivyo Basi huenda ikawa shemeji akawa ndio mchawi"

"Hilo sikupingi ndugu yangu kwa asilimia 99% shemeji yako ni mchawi,Sasa nitafanyaje ndugu yangu?"


" Hapo bana Sadiki ni kua makini ,raha sivyo na wewe utakuja kua mchawi kweli au atakuja kukutoa sadaka" 


" Kwani shemeji anaitwa nani! Na ametokea wapi? Maana wewe nawe kwa kuokota okota wanawake siku utaokota jini!"

" Usintishe bana Sadi! Shemeji yako anaitwa Chuma ,ni African beaut hivi ,anatokea pande za morogoro huko sijui Kijiji gani lakini ni mtu wa milimani huko kwenye safu za milima ya ulugulu.!"

 

Ghafla bosi akaniita Mimi!"

" We kijana Samahani,nakuomba ! Kuna kitu umeongea hapo kidogo umenishtua"


Sijajua ni nini bosi alichoniitia  mpaka nilipoenda kumsikiliza.

"Naaam bosi"

"Ndio kijana ,Mimi naitwa foya au mzee foya Kama watu walivyo zoea kuniita. Nimewasikiliza vizuri mazungumzo yenu,lakini Kuna jina la mtu mmoja umelitaja na mahari alipotoka, umenishtua mno!!"


"Mh! Jina gani hilo mzee wangu! Na kwanini likushtue hivyo?"

" Kijana wangu hilo jina ni lilikua ni la mfanya kazi wanting wa ndani,lakini kwa Sasa huyo mtu NI hadui yangu mkubwa,najua huko aliko Chuma wa morogoro Ndolelo, anataka alipe kisasi kwangu na familia yangu .Chuma ni mchawi Yani ni binti hatari Sana.!!!!"


" Mzee Foya, samahani kidogo ,unajua Chuma Mimi ni mke wangu,Na nilishaona  Mambo ya hajabu pale nyumbani,nahisi huenda akawa ndio huyohuyo binti unaye mzungumzia."


" Ndio huyo huyo bila Shaka,kijana,unatakiwa ujiongeze,japo Mungu yupo lakini unatakiwa ujiongeze raha sivyo utapotea."

" Sasa mzee wangu Mimi sielewi chochote Cha kufanya,nilishawahi kumshilikisha mchungaji ,lakini mchungaji alinishauli kumwomba mungu tu zaidi."

" Kijana mchungaji yupo sahihi kabisa , Mungu kwanza lazima umtangulize Kisha mengine ndio yanafuatia. Kama hutojari tafuta siku moja  baada au kabla ya kumaliza kazi yangu,nikupeleke kwa mtaaaramu mmoja yupo huko huko morogoro vijijini mgeta ,huyo anaitwa "Mganga Alumbile Kalumba" kiboko ya vibwengo wote,atakucheki na atakukinga dhidi ya hadui yako. Mimi mwenyewe mpaka Leo niko salama ,ni kwa  ajili yake japo Mungu ndio mkuu katika hayo.Nadhani umenielewa?"


"Nimekuelewa bosi wangu ,wacha nikafanye kazi tutaendelea kuwasiliana"


................ Ita endelea..........................

Je, nini kitaendelea? Usikose kufuatilia story yetu nzuri yenye utamu mpaka tindini au tebwetani yani full shuga sukari.


Nashukuru kwa wote mnao nisaport kufuatilia story za Morgan wa Madola.

Saport zenu zisi ishie hapo, ukipenda unaweza pia kunisaport kwa kikombe πŸ₯ƒ kimoja Cha kahawa 🍷 na kashata.

Pia ningependa kupata zaidi maoni yenu,Kama Kuna Jambo haliko sawa kwa upande wangu au wenu, tuwekane sawa. Asante sana ndugu msomaji ,nakutakia siku njema.✏️

URITHI wa Bibi 10

 Story......... URITHI WA BIBI EP . 10


Mtunzi : Steven Morgan


Contact : +255659115223


Naam, ndugu wasomaji karibuni Tena katika muendelezo wa story yetu . Japo mwendo wa kinyonga lakini tutafika. Pia unaweza kunipiga teke, kwa kunichangia kikombe Cha kahawa 🍷Cha Mia tano tu! Ili mniongezee meendo wa kuwaletea Mambo mazuri . Sio lazima ila ukijisikia kwa moyo ..... +255659115223 tigo pesa.


Tuachane na hayo ,Sasa turudi kwenye story yetu.Kama kawaida tulipoishia ndipo,tunapoanzia.


ILIPOISHIA EP9...


Sadi nikikupa nafasi ya kuchagua ,kua Mimi niwe ,rafiki yako tu,au ndugu yako ,au Dada yako,au jirani yako! Au mpenzi wako! Je,wewe utachagua nafasi ipi kati ya hizo?"

"Duh ! Kwa kweli kabisa kutoka moyoni ,Mimi nitachagua uwe mpenzi wangu wa pekee! "

"Basi karibu moyoni mwangu Sadi,nimeamua kukukabidhi moyo wangu mwepesi Kama karatasi, tafadhari usije ukanisariti Sadi."

" Chuma wacha kunitania bana ! Hivi ni wewe unae ongea hivyo au!"

"Sadi sijachanganyikiwa naongea nikiwa namaanisha au hunipendi, Kama hutaki Basi wacha niondoke!"

"Hapana Chuma ,unajua siamini kabisa lakini Kama unaniaminisha hivyo! Basi na Mimi nasema kua , nakupenda kweli na ikiwezekana hata leo amisha mizigo yako hapa tuanze maisha yetu.

    

Sadi bila kujua kua anamkaribisha shetani ndani,na pia ana mkaribisha ezraeli mtoa raho yake,ana amua kumchukua Chuma na kwenda nae mpaka kule gesti alipo panga,atamsaidia kubeba mizigo yake ,na Chuma Sasa  rasmi ameamia kwa Sadi Kama kuishi Kama mke na mume huku Chuma akiwa na  mipango yake ya maangamizi........................


Endelea..

Basi ,maisha yaliendelea kati ya Chuma na Sadiki au Sadi. Imeshapita Sasa takribani mwaka mmoja. Lakini Chuma hakupata mtoto bado ! 

Siku moja hasubui na mapema Sadi aliamka mapema ili ajiandae kwenda mihangaikoni,alimwamsha mkewe Chuma.

"Mke wangu Chuma ..!"  "Ndio mpenzi nambie"     " unajua Chuma huu ni mwaka Sasa lakini !"  " Lakini nini?" Alidakia Chuma kwa ukari.

" Lakini sioni dalili zozote za wewe kua ni mjamzito,nimejitahidi kweli lakini sielewi tatizo ni nini!?"

" Kwa hiyo una maana gani?". " Maana yangu ni kutafuta suruhisho la tatizo hili ili nasi tuwe na watoto wetu Kama wengine. Baadae nikitoka mihangaikoni , nitakuja kukuchukua twende tukapime afya zetu za uzazi ili atakae bainika na kasoro, apate tiba ,sawa mke wangu?"

"Sawa Sadi kipenzi ni Jambo jema hilo"


Nilimkubalia mume wangu Sadi,kwa kile anacho kitaka. Lakini kiukweli Mimi ndie nilikua na sababisha Sadi asiwe na uwezo wa nguvu za kiume ili asizae na Mimi maana ,sikutaka mwanangu akose baba maana nilijua kua siku za Sadi za kuishi zilikua zinahesabika. Nilikua na hakika kabisa kua Sadi hawezi kuumaliza mwaka huu. Basi , niliendelea na shughuri za pale nyumbani ,nilipomaliza nikapumzika nikawa naangalia tv. Mara ghafla upepo mkali ulivuma pale ndani vitu vilivyokua vyepesi vilipeperuka huku na kule . Sikuelewa ile hari ni nini? Nilibaki nimeduwaa Kama zoba! Nilikuja kushtuliwa na kofi zito na mtu nisie mjua kwa haraka,mpaka akili zilipokuja kukaa sawa,ndipo nilipojua kua alie kuja pale kwangu alikua ni mkuu amenijia kwa hasira kubwa sana.


" Chuma umejisahau Sana,tunahitaji sadaka yako Sasa,wenzako wote wametoa kasoro wewe Chuma!"   

"Sawa mkuu nitatoa naomba nipeni muda kidogo" " Chuma huna Tena muda was kutosha ila kwa heshima ya Bibi yako Mbokeleni nakupa muda wa kutosha ,kuanzia Sasa anza kazi ya kumwandaa mhusika ,sawa Chuma?"

"Ndio mkuu"

Mara ghafla mkuu akapotea ! Nikavuta pumzi Kisha nikaishusha taratibu ,nikawa nahema kwa hofu.  

Mtu pekee wa kumtoa sadaka ni Sadiki na si mwingine,nilikataa kumbebea ujauzito sababu nilijua yeye ni marehemu mtarajiwa siwezi kuishi na mtoto asie kua na baba. 

Bila kupoteza muda nikaanza maandalizi ya kumdhuru Sadi mume wangu. Nikachukua nguo yake  na kuanza kuichawia,Kisha akaja yule Mama wa Kenya palepale . " Naona unaandaa mtego wa kumnasa mnyama wako" "ndio mama lakini hata hivyo nimepungukiwa na sanda ambayo ndio ingekamilisha mtego huu!" 

"Usijari Chuma Mimi sanda ninayo ipo nyumbani Kenya,ila ngoja nikuletee ukamilishe mtego wako."  

Huwezi amini lakini ndivyo ilivyo kua, sanda ikaja palepale! Baada ya yule Mama mkenya kuiita pale kwa mamraka ya kichawi.

Ndugu msomaji nilipokua naandaa mtego wa kumnasa mtu wangu,si masihara huu ni mtego hatari Sana. Ukiponyeka katika mtego huu ,Basi huwezi kuja kufa kwa kurogwa tena ,utakuja kufa kwa amri ya Mungu tu!!


Nikachukua ile sanda,nikashona suruali kwa sindano na uzi wa mkono. Kisha nikakata upande mwingine wa sanda, nikashona tisheti Kisha tukazipigia ndumba nyingine nikisaidiwa na yule mamangu mkenya.  Kisha nikachukua nguo za mume wangu anazo pendaga Sana kuzivaa mara kwa mara. Tukazichawia kisha tukazipoteza kichawi! Zilizo baki pale Sasa ,ni zile nguo za sanda nilimuwekea kabatini mume wangu ili akirudi azivae ,hatoshtuka maana yeye na watu wengine wa kawaida wataziona Kama ni nguo tu za kawaida za siku zote lakini nyuma ya pazia ni sanda.

Baada ya kuweka zile nguo kabatini ,hatua iliyo fuata ni kupanga tarehe na mwezi wa kufa mtu yule katika mwaka huu.Na aina gani ya kifo atakufa mtu huyo?

Ndugu msomaji Duniani Kuna mambo,! 

Huu mtego nilio uhandaa,sio Kama namuua moja kwa moja! Bali katika ulimwengu wa kimwili ataonekana amekufa kweli, lakini kiroho na mwili wa kweli tutakua tumeuteka na kuuficha kichawi,mpaka itakapobainika wazi katika jamii kua yule mtu amekufa na amezikwa ndipo sisi tunapoanza kumtumia mtu wetu katika uharisia wake harisi akiwa Kama Msukule. 


Basi tukapanga tarehe fulani na mwezi fulani ndio itakapokua mwisho wa Sadiki kuishi Duniani. Zile nguo tulizozitengeneza kwa sanda ,atatakiwa kuzivaa mara40 ,na sisi tutalala matanga siku arobaini ingari yeye bado yupo hai.


Basi mtego ulikamilika ,tukaweka kila kitu sawa. Kwakua muda ulishaenda ,nikapika chakula Cha mchana ,nikamwekea mume wangu Kisha nami nikala na mshirka mwenzangu. Baada ya hapo tukaendelea kupiga story za hapa na pale.


Sasa tuachane na Chuma pale nyumbani ngoja tumwone Sadi katika harakati zake.


Sadiki akiwa na mawazo makubwa huku akitembea barabarani kwa mwendo wa kinyonga,mara ghafla.. ..honi ya gari! Piiii! Piiiiiiii! Piiiipiiipiiiii !!

Nikashtuka Sana maana kiukweli Sadiki Mimi nilisha jisahau Kama nipo barabarani ,mawazo yalini zonga Sana. Mara akashuka mtu mmoja kwenye lile gari lililo paki pembeni baada ya kunikosakosa kunigongea. Alikua ni mbaba mtu mzima ,alivalia suti nyeusi ,akiwa na mwonekano wa kichungaji.


" Kijana habari! Naitwa mchungaji Nelson ,kanisa langu lipo kule maeneo ya segelea."

" Mimi naitwa Sadi au Sadiki naishi kule buguruni na mke wangu."

"Sawa kijana ila unaonekana haupo sawa kabisa je,ni nini shida?"

"Mchungaji, ni kweli Nina shida kubwa sana, Mimi na mpenzi wangu Chuma tumeishi takribani mwaka mmoja Sasa! Lakini mke wangu hata dalili za uja uzito Hana ,nami nataka watoto mchungaji sijui nini shida"

"Usijari kijana hakuna kinachoshindikana Kama tu uta mshirikisha mwenye ezi Mungu!   Je, baada ya hapo wewe umepanga kulimaliza tatizo hilo kwa njia gani?"

"Mchungaji,nimepanga hivi ninaporudi nyumbani nimchukue mke wangu niende nae hospitali tukapime ili, atakae bainika na kasoro,atibiwe."

" Sawa kijana,fanya hivyo mara moja ila,mkiona hamjafanikiwa, Basi ,chukua hizi namba zangu zasimu 07xxxxxxxxx. Utanipigia ili kulimaliza tatizo lenu maana hakuna kinacho shindikana Kama ukijikabidhi kwa Yesu kristu awe bwana na mwokozi wako."

" Asante mchungaji ,namba nimeshazisevu nitakutafuta nitakapo kuhitaji ,wacha Sasa nirudi nyumbani."

"Sawa kijana ila punguza mawazo usije ukapata hajari ! Safari njema.


Basi,nika agana na mchungaji Kisha nikapanda bajaji nikarudi zangu nyumbani.

Lakini nilipofika nje ya mlango wa chumba changu nilisikia sauti ya mke wangu na sauti nyingine ya mmama mtu mzima akiongea ,walikua wanazungumza mazungumzo ya kawaida huku sauti ya tv ikisikika kwa mbali.Nilijua mke wanting yupo na jirani yake anapiga stori.

Nikabisha hodi kwa kugonga mlango na  kunena kwa sauti.

" Hodi hodi mke wangu,nimerudi mumeo"  

"Karibu mume wangu"

Sauti ya mke wangu ilisikika Kisha kimya kingi kilitanda Kisha ghafla nikahisi kichwa kuuma kwa ghafla Kisha nikarudi kwenye hari yangu.

Mara mlango ukafunguliwa na mke wangu nikaingia ndani, kiukweli ndani kulikua kuzito Sana ,nywele zilikua zina nisisimka,lakini pia nilishangaa Sana kutoona mtu mwingine ndani wakati nilimsikia mke wangu akipiga story na mtu mwingine,nikabaki nimeduwaa!!

"Mume wangu vipi ! Mbona upo hivyo?"

"Nashangaa mke wangu,niliwasikia mkiongea huku ndani na mwenzio ,Sasa nashangaa ninavyoona kua upo mwenyewe humu,je ulie kua unaongea nae Yuko wapi? Au umemficha mvunguni?"


"Mume wangu nawe kwa wivu! Humu Wala hakuna mtu labda tv ndio uliyo isikia ! "

" Sawa mke wangu tuachane na hayo,niandalie maji ya kuoga Kwanza mamana nahisi joto Kali Sana."


Nilimwandalia mume wangu maji ya kuoga ,Kisha akaenda kuoga . Nilikua nahofu kumbe mume wangu alitusikia tukiwa tunaongea ,na alipogonga hodi yule mmama mkenya akapotea kichawi ghafla ! Ndo maana mume wangu alihisi kichwa kuuma na kizunguzungu kwa sababu pale ndani kulitawaliwa na nguvu za kiza .

Mume wangu alitoka bafuni Kisha akaja ndani.

" Mke wangu nimeshamaliza kuoga hebu niandalie nguo nzuri za kuvaa na kupendeza"

 Kichaa kapewa rungu ,nikafungua kabati na kuchukua tisheti na jinsi, kwa macho zinaonekana hivyo lakini kiukweli ndio zile nguo nilizo zishona kwa sanda !! Nilimpa zile nguo mume wangu,akazivaa Kisha nika mwandalia chakula tukala wote pia japo Mimi tayari nilisha kula. Mimi nikimwangalia mume wangu nilimwona amevaa sanda kabisa juu na chini lakini kwa wewe ndungu msomaji mwenye macho mawili ,ukimwangalia mume wangu utamuona amevalia tisheti na jinsi, hata yeye mwenyewe mume wangu akijitazama ,anajiona amevaa tisheti na jinsi,nguo zake anazozipendaga.

  

Tukamaliza kula ,nami nilijiandaa ,nikabadili nguo Kisha tukatoka na kufunga mlango wetu, Safari ilikua ni kwenda hospitali kwenda kupima  afya za vizazi vyetu.

Nikiwa na mume wangu kwa mguu tulitembea kwenda kwenye hospitali moja ya Aghakhan ,tulipofika tulionana na  dokta . Tukajieleza Kisha dokta akachukua vipimo vyake ,tukasubili kwa nusu saa, dokta alitupati majibu kua ,wote sisi vizazi vyetu viko sawa Wala hakuna tatizo lolote la kutibika kibaolojia. Cha msingi ni kumwomba mungu zaidi maana yeye ndie anaye toa.


"Tunashukuru Sana dokta kwa majibu na ushahuri wako!"

"Asanteni karibuni Tena!"

"Tunashukuru dokta"


Baada ya hapo nikamchukua mke wangu Tukapanda bajaji tukarudi nyumbani. Nilipofika nyumbani nilikua sijielewi elewi kwa kweli nilikua nahisi Kama wenge ,sikutaka kwenda kokote pale ,niliwasha tv nikawa naangalia ,mpaka Usiku ukaingia .

Sijui Kama nilikula chakula Cha Usiku maana nilipokuja kushtuka nilikua tayari nipo kitandani chumbani nimelala. Pembeni alikua mke wangu nae amelala pia. Sikutaka kumwamsha maana na Mimi mwenyewe macho yalikua mazito ,ishara ya usingizi mzito ukininyemelea, sikua na ujanja nililala Kama fofofo!! 

Mara nikajikuta nipo mtaani kwetu nyakati za usiku Sana ,huku nikikimbizwa na watu wa hajabu nisio wajua wameshika mapanga,wengine wameshika mikuki , wengine walibeba mawe makubwa lakini walipokua wananirushia Yale mawe yalikua yanakuja kwa spidi kubwa utadhani yalikua hayana uzito. Lakini yalinikosa kosa na kuangukia pembeni ,yalichimba ardhi Kama pango yalipotua chini. 

Nililia Sana😭😭😭  huku nikiendelea kulia na kuita kuomba msahada lakini hakuna alie nisikia hata kidogo mtaa mzima ulikua kimya . Mikuki ilinikosakosa  nikazidi kukimbia ,jasho zilinivuja na nguvu  ziliniishia kabisa ,nikaanguka chini ,huku wale watu na siraha zao tofauti wakiwa wanakuja taratibu,mmoja wao alinikaribia na akanioneshea ishara ya kunichinja shingo yangu na damu yangu kuinywe.  Jamaa lile likanyanyua panga lake juu akijiandaa kuniua. Mwili wangu haukua na nguvu ,nikaita mpaka ni kachoka,mwishoni namwona lile lijamaa limejikinya kushusha panga lake kwa Kasi ili anikate shingo yangu,nilinena kwa kumwomba mungu wangu.. "Ee Mungu wangu uniokoe ,Kama hii ni ndoto ,unihamshe nitoke katika usingizi huu nikiwa salama,Mungu wangu niokoe"

  Lile panga lilipokua linashuka ,na kukaribia  kwenye shingo yangu nilipiga kelele kubwa  mpaka nikashtuka usingizini!!! 

Kumbe kulikua tayari kumeshakucha, mke wangu alishtuka nae kwa kelele nilizopiga .

Mwili wangu wote uliloa jasho ,mapigo ya moyo yalikua yanaenda mbio sana,. 


"Vipi mme wangu Mbona hivyo" nilimuuliza mume wangu kwa unafki kwani nilikua najua vizuri Sana kilichomkuta.

Ndugu msomaji ndoto ni ujumbe mzuri Sana Kama utajua maana yake. Ndoto inaweza kukupa ujumbe mzito juu ya hadui anaye kufuatilia maisha yako.


Kwakua mume wangu Sadi,nilisha muweka kwenye tageti zangu ,hiyo ndoto aliyo iota ni ishara kwamba Kuna hadui mwenye Roho mbaya na lengo baya Sana katika maisha yake na hadui ameshaanza mashambulizi makali dhidi yake,hivyo anatakiwa kua makini, raha sivyo anaweza kupotea kwa kufa na kuchukuliwa Msukule.


"Mke wangu nimeota ndoto mbaya Sana ,mpaka moyoni nimekosa amani kabisa"

" Mme wangu hiyo ni ndoto tu Wala usiwe na wasiwasi,ngoja nikakuandalie maji ya kuoga utoe uchovu.


Nilienda kumwandalia maji mme wangu ,tulienda kuoga wote tukarudi ,nikaandaa chai tukanywa Kisha akaniaga kwenda kwenye mizunguuko yake ya kujitafutia ridhiki.

  

" Mke wangu tutaonana badae kidogo "

Nilimuaga mke wangu Kisha nikaondoka . lakini kiukweli moyoni nilikua na hofu Sana kutokana na ile ndoto ya Jana Usiku. Nikakumbuka kua nina namba ya mchungaji Nelson wa segelea. Nikampigia simu ,akasema kua yeye Yuko kanisani ila ,ingekua vizuri Mimi niende huko kuliko kuongea kwenye simu.

 

Nikapanda gari moja kwa moja segelea kanisani.

Ilikua ni siku ya juma tatu,mchungaji nilimwona akiwa anakagua ujenzi wa kanisa jipya. 

 

" Karibu Sana Sadiki,twende ofisini kwa mazungumzo zaidi"

Tulienda ofisini na mchungaji Nelson.

 

"Karibu ndugu Sadiki,unaweza kuketi hapo, mmhmm! Bila Shaka nakumbuka nilikutana na wewe kule barabarani na nikakosakosa kukugonga na gari langu ,si ndio?"

"Bila Shaka mchungaji!"

"Sawa kabisa na ulinielezeaga tatizo lako na mkewe kuhusu uzazi vipi ! Uliishia wapi ? 

" Tulienda hospital na mke wangu tulipima ,lakini Cha hajabu! Wote tukaonekana hatuna tatizo,Yani wote ni wazima,ila dokta ametushahuri tu tumwombe Mungu tu maana yeye ndie anae to.!!"

"Mh!  Sawa ndugu sadii,Mungu pekee ndie anaye toa na ndie anaye twaa,umekuja sehemu sahihi tatizo lenu litakwisha "

"Amen mchungaji! Lakini ukiachana na hilo mchungaji, Kuna Jambo lingine linanitatiza Sana"


Nilimuelezea mchungaji kila kitu kuhusiana na ile ndoto na ile siku narudi nyumbani na kusikia mke wangu anaongea na mtu Kisha baadae baada ya kuingia ndani anasema alikua ni yeye tu na tv pekee.

" Sadiki upo kwenye hatari kubwa sana,tena ni hatari ya kufa,inaonekana Kuna hadui anakufuatilia,na ameshaanza kukushambulia, na hadui huyo hayupo mbali ,yupo ndani kwako."...................


          Itaendelea...............

Je,Binti Chuma atafanikiwa kumtoa sadaka Sadiki?

Je,vipi maisha ya mzee Foya yanaendeleaje?

Je,Chuma ataweza kulipiza kisasi kwa mganga Alumbile Kalumba Alie muua Bibi yake?

Hayo na mengine mengi ya hajabu utayajua zaidi kwenye episode zijazo.



URITHI wa Bibi 9

 Story........ URITHI WA BIBI EP.9

Mtunzi........ Steven Morgan


Contact.....+255659115223


Ilipoishia....πŸ‘‡


"Sawa karibu" nilimjibu yule kijana kwa urahisi kabisa bila usumbufu.

"Asante sana mrembo Chuma naomba nipe dakika 3 tu nikachukua vinywaji vyangu kule kwenye meza yangu nihamishie hapa."

"Sawa nenda." Nilimjibu. Sasa wakati anaenda kuchukua vinywaji vyake yule kijana ,Mimi Kuna kitu kikanishtua au naweza sema nilipata message ya kichawi,nikanyanyuka haraka na kwenda chumbani kuangalia vizuri huo ujumbe.............. ...............


Endelea πŸ‘‡

Nikanyanyuka haraka kwenda chumbani kuangalia huo ujumbe vizuri.Nikaingia kwenye kile chumba nilicho Kodi, nikafungua begi langu kubwa na kutoa kioo changu ndipo nilipo mwona mkuu aliniambia kua ,kutakua na kikao Usiku huo kwa hiyo nisikose. Nikafanya maandalizi ya haraka kwaajili ya kikao .Kisha nikarudi pale baa kwenye kile chakula changu, muda ulikua umeshaenda kidogo ilikua ni saa4 Usiku. Nikamkuta yule kijana Sadi bado yupo pale kwenye meza yangu ananisubiri,huku akiwa anaendelea kula chakula chake taratibu.

"Chuma Mbona umenitoroka ghafla sijakukuta lakini nikajipa moyo nikahisi labda ulienda msalani (chooni). Vipi kwema lakini? Mbona unaonekana Kama haupo sawa?"

Sadi aliniuliza ,sijui alinionaje lakini nahisi nilikua tofauti kutokana na maandalizi ya kichawi niliyo yafanya. Hapa naomba niwape Siri moja ndugu wasomaji, uchawi siku zote huwa ni Kama vazi,hivyo nilipoenda kujiandaa maana yake nilisha vaa vazi la uchawi,na pale nilipokaa na Sadi,naweza kufanya chochote kile kinacho husiana na uchawi,na Kama ulisha wahi kumwangalia mtu usoni afu ukamwona Yuko tofauti kuliko siku zote ulivyo mzoea yaani anatisha sana na huwezi kumtazama mara mbilimbili ujue,huyo mtu sio wa kawaida kwa mda huo,lazima atakua amevaa kikoti Cha uchawi na amejiandaa na Jambo fulani hata Kama mchana kaa nae mbali.


Basi tuachane na hayo ,turudi pale mezani ,nikiwa bado nipo na yule kijana Sadi,nikawa naendelea kula chakula changu bila kuhofia chochote. Akili yangu haikua pale kabisa,hata Sadi alipokua akiniongelesha nilimwona Kama inzi anae nisumbua.

"Chuma sio Siri nimevumilia nimechoka ,wacha tu nikwambie ukweli,Mimi nahisi kukupenda kweli,na Kama utanihafiki ,nitakuoa tuishi Kama mke na mume!"

"Unajua Sadi unaniletea utani sana hapa!"

"Hapana Chuma Mimi nakupenda kweli na sio masihara!"

"Sasa wewe kijana Yani umeniona leo tu,alafu unaniambia unanipenda! Hivi unanijua vizuri kweli wewe?"

" Haijarishi Chuma ,kwa Sasa ninachokijua Mimi ni kukupenda wewe tu,suala la kukujua vizuri,nitakujua baadae."

" Sadi wacha kujifanya shujaa,endapo ukinijua hata kwa dakika moja huto tamani Tena kukaa karibu yangu"

"Mh! Wacha kunitisha Chuma wewe ni mrembo sana nitawezaje kukaa mbali nawe?"

"Sadi hivi kweli unaweza ukaishi na jini?"

"Kwanini unaniuliza hivyo Chuma! Inamaana wewe pia ni jini?"

"Ndio Sadi Mimi ni jini" nilimdanganya yule kijana ili asinizoee.

" Hahahaha! Wacha uongo Chuma jini hawezi kula vyakula Kama unavyo kula wewe ,labda utakua hunitaki tu , ila Mimi nakupenda tu hata Kama wewe ni jini"


"Sawa Sadi ila ni vyema ukakaa mbali nami ili nisije nikakudhuru."

 "Chuma naomba nikuachie namba yangu ya simu ili siku nyingine ukipenda unitafute tuongee zaidi"

" Sadi Sina haja ya namba zako kwa sababu hata hiyo simu yenyewe Sina"

"Chuma sikia hapa Nina simu mbili chukua hi simu moja Kuna laini yangu humo ya Vodacom pia Kuna namba yangu humo imeandikwa jina la Sadi,nafikiri tutawasiliana Chuma"


"Asante Sadi ila kwa Sasa naomba uniache mwenyewe nitakupigia kesho sawa?"

" Sawa Chuma Basi nikutakie Usiku mwema mpendwa."

"Nawe pia Sadi "


Tuliagana na Sadi Kisha akaondoka na kuniacha Mimi mwenyewe pale mezani.

Nikalipa bili ya chakula Kisha nikarudi ndani kwenye chumba changu. Kwakua muda ulikua umeshaenda ,nikatoka nje ya ile gesti kichawi Kisha Kuna ndege ilinipitia palepale tukaondoka kwenye kikao. Kikao kilifanyika mlandizi ,tulipofika tukashuka tukiwa wengi sana Kama vile tulikua tumepanda Basi la mwendo Kasi. Kila mtu akakaa kwenye siti yake kasoro Mimi tu ndio nilikosa siti.

Ndugu msomaji ninaposema nimekosa siti simaanishi siti unayoijua wewe Kama stuli,kigoda au Kochi. Bali siti zetu sisi huwa ni watu harisi ndio huwa tuna wakalia Kama siti, Kama ulishawahi kulala Usiku na uka amka asubuhi ukiwa umechoka sana na mwili unauma  baadhi ya sehemu,ujue ulibebwa Usiku na mchawi na ulienda kutumika Kama siti.


Basi ,baada ya Mimi kukosa siti ,nikaamua na Mimi kutafuta siti yangu.Nikatumia maneno ya mamraka yasio pingika,labda Mungu pekee ndio wa kuzuia. Nikamwita yule kijana Sadi kwa mamraka ya kichawi.

Hapa naomba nielezee kidogo ,ndugu msomaji . Kama ulishawahi kusikia sauti ikikuita kwa jina lako haswa  nyakati za Usiku alafu ukashtuka usingizini na kuitika kwa sauti,bila kujua anaye kuita ni nani! Wakati mwingine unaweza ukatoka nje kuangalia anayekuita usimwone yeyote. Ujue kua hiyo ni sauti ya mamraka ya kichawi inayokuita kwa dharula ili ukatumike na sio kurogwa. Sasa unapo ona hari hiyo inakupasa ukemee kwa jina la Mungu baba na  Yesu kristu ili kujinusuru katika janga hilo la kutumika.


Basi turudi pale kwenye kikao mlandizi,niliendelea kumwita yule kijana Sadi kwa majina yake mawili ,japo jina lake la pili sikulijua nilitumia jina la Adamu Kama ndo jina la baba yake ,kwa hiyo nilimwita "Sadiki Adamu njooooo", "Sadiki Adamu njooooo" x3 .

Nilirudia rudia kumwita kwa jina hilo mara tatu.  Huwezi amini ila ndivyo ilivyo kua ,yule kijana akatokea palepale nilipo huku akiwa amepiga goti. Nika muinamisha akawa anatembea kwa mikono na miguu, nilipofika sehemu niliyo itaka nikamkaria mgongoni Kama farasi ,nikatulia huku nikisikiliza kinacho endelea.

 "Karibuni wageni waarikwa wote , karibuni kamati maarumu za mapishi kwa ajiri ya kikao chetu leo. Kwanza kabisa nitoe pole kwa wale wote walio ondokewa na wapendwa wao akiwemo Bibi Mbokeleni au Bibi Chuma. Tuna mkumbuka sana kwa MCHANGO wake mkubwa katika kushirikiana kimataifa haswa katika nchi za umoja wa afrika alishawahi kua katibu mkuu . Saramu za pole na rambirambi tulizielekezea kwa mjukuu wake Chuma, nafikiri wengi mnamjua,na wale msio mjua Basi Leo mtamwona. Chuma popote ulipo simama juu uwasalimie wageni wenzako.""


Mkuu aliamuru nisimame juu  niwasalimie wenzangu,nilisimama juu Kisha nikalia Kama paka mwenye jazba,Kisha wageni wote waarikwa nao pia wakashangilia kwa sauti mbalimbali, wengine walilia Kama mbwa,Simba,bundi,dudumizi ,na wengine walilia kwa sauti nyingi za hajabu usio weza kuzifananisha na kiumbe chochote.

Baada ya happy nikakaa kwenye siti yangu,na mkuu aliendelea.


"Asanteni sana ndugu zangu. Baada ya kusalimiana ,napenda kutangaza kua Chuma ana vita Kari ya kisasi dhidi ya mzee Foya na familia yake pamoja na mganga mmoja hatari Sana anaitwa  Alumbile Kalumba,anaishi huko mgeta vijijini. Lakini kazi hiyo ya kisasi tayari Kuna mwana mama toka Kenya atamsaidia Chuma katika kazi hiyo.

Tuachane na hayo ,wacha nizungumze mada muhimu ya leo. Leo nime waita hapa kuwakumbusha Jambo kubwa la muhimu Sana.Ndugu zangu huu mwaka ni mwaka wa kutoa sadaka kwa hiyo ,wote wenye zamu yao ,wajiandae na wale ambao hawajaoa au kuolewa ,wajitahidi mwaka huu watafute wachumba ili tupate sadaka katika uzao wao na Kama hamtazaa Basi mtawatoa kafara wapendwa wenu. Nadhani tume elewana!! Huu ndio ujumbe mkubwa wa leo. Tukiwa tunasubiria kamati ya chakula kutuandalia msosi,kamati ya burudani ijiandae kutuburudisha.Asanteni."


 Basi baada ya mkuu kumaliza kuongea ,vikundi mbalimbali vya burudani  vilianza kutoa burudani,tulicheza Sana ngoma . Ninaposema tulicheza ngoma,sio hizi ngoma mnazo zijua,ngoma tulizokua zinapigwa ni wale watu tulio wafanya viti,ndio walichukuliwa pia kupigwa na kutoa mlio wa ngoma harisi ,nilimuonea huruma Sana yule kijana Sadi ,kwani mtu Alie mchukua alikua akimpiga kichwani huku amemkalia mgongoni. Hapakua na namna tulicheza Sana ,baadae ngoma zikanyamaza ,tukachukua siti zetu tukaketi,msosi ulikua tayari tulipewa msosi wa minyama minyama ya hajabu, nafikiri ni nyama ya mtu na si mnyama maana wengine walipewa mpaka viganja na visigino ambavyo vilionekana kabisa ni vya mwanadamu. Tulikula  na kunywa vinywaji vya damu nzito za watu.

Mwishoni mkuu akasimama na kufunga kikao Kisha akasema "kila mtu ahakikishe anakirudisha kiti chake msije mkasahau"


Basi kila mtu akatoa maneno ya mamraka kurudisha kiti chake ,nami pia nikachukua Sadi wangu na kumuamuru arudi nyumbani. Akatoweka  nami nikaenda kupanda ile ndege kubwa ya abilia ,ikaondoka kwa kuvuma Kama ngumbeo. Ilipofika tabata maeneo fulani nilishuka nikapotea kichawi na kuibukia ndani ya chumba changu pale gesti. Nilikua uchi wa mnyama kabisa ,na ilikua ni saa kumi na nusu usiku,kwakua. Choo na bafu kipo humohumo chumbani sikupata shida ,nilioga Kisha nikalala .


Nilikuja kushtushwa na mlio mkubwa wa simu ,ni ile simu aliyo nihonga  yule Kijana  Sadi. Nilipotazama simu ,niliona jina la Sadi ndio aliye kua anapiga. Nikapokea..

"Halooo Sadi" 

"Halooo mpenzi Chuma"

"Ukome wewwkijana ,huo upenzi na wewe umeanza lini?"

"Jamani Mbona unakua mkari hivyo Chuma!! Ok sawa Kama hutaki mimi niwe mpenzi wako ,Basi nitakua  rafiki yako tu inatosha. 

"Sawa nambie ulikua unasemaji ?"

" Chuma ,mwenzio nimeamka asubuhi hi,sijielewi kabisa,yaani kichwa kinaniuma Sana,na mgongo pia unauma sana, sijui tatizo nini Chuma ,hata kunyanyuka siwezi."

 

Sadi aliongea hivyo kunieleza Mimi lakini Mimi nilijua ni nini haswa kinacho msumbua . Hari hiyo kiukweli haiitaji miti shamba unaweza ukatumike tu dawa zozote za maumivu na ukapona.Kiukweli nilimuonea Sana huruma Sadi na nilishaanza kumpenda kweli japo sikutaka ajue Kama nampenda.


"Kwa hiyo Sadi nikusaidieje?"

"Naomba uje unichukue unipeleke hospitality,kichwa kinaniuma Sana."

"Hapana Sadi ,wacha tu nikununulie dawa za maumivu ,Kisha unielekeze unapokaa nikuletee ,sawa?

"Nitashukuru Sana Chuma rafiki yangu ,njoo huku buguruni ,ulizia kwa mangi dalari ,ukifika, ulizia kua chumba Cha Sadi au Sadiki Kiko wapi? Wakikuonesha we ingia tu ndani moja kwa moja maana mlango uko wazi."

 "Sawa Sadi nakuja muda si mrefu"


Nikajiandaa kwa kuvaa nguo zangu za kawaida na nika angalia muda , tayari ilishafika saa tatu asubuhi. Nikafunga mlango wangu ,funguo nikaenda kuiacha pale kaunta.kisha nikaondoka ,nilinunua dawa kadhaa za maumivu na matunda Kama ndizi machungwa pia nikanunua mboga Kama mchicha ,nyama na mazaga zaga  mengine kibao.

 Nikafuata maelekezo yake niliulizia chumba chake ,nilioneshwa nikaingia ndani maana mlango ulikua wazi .


"Karibu sana Chuma ,siamini Kama umekuja kuniona Chuma! Ukizingatia tumeonana Jana tu!"

 "Usijari Sadi,hebu jitahidini unyanyuke unywe hizi dawa za maumivu."

  Sadi alijitahidi kunyanyuka lakini alishindwa. Nika amua kumnyanyua kinguvu ,alilalamika Sana kwa maumivu. Nikampa dawa akanywa ,nikampa na ndizi za kuiva akala,nikammenyea na machungwa akala pia.

Nikawaambia Sasa pumzika wakati Mimi nakuandalia chakula Cha baadae .


"Nashukuru sana rafiki yangu"

"Sawa usijari,je ,vyombo viko wapi nimekuja na msosi inabidi nipike !"

"Duh! Asante,vyombo vyote angalia hapo  kabatini jiko hilo hapo mezani la gesi."

"Sawa Sadi wewe pumzika tu utakua sawa tu muda si mrefu."

Niliendelea kuandaa mboga Kisha nikaivisha wali,muda huo nilimuonea Sadi akinyanyuka mwenyewe kitandani na kujinyoosha viongo vyake vya mwili.

"Duh! Chuma ,nimepona rafiki yangu Chuma ,wacha nikaoge kwanzanitoe uchovu"

" Mi si nilikwambia kua muda si mrefu utakua sawa! Sasa Nenda kaoge alafu uje tule. "

" Sawa Chuma dakika tano tu ntakua nimeshamaliza.Asante Sana."

 Sadi alienda kuoga ,nami nikaandaa chakula mezani tayari kwa kuliwa. Wakati nipo pale chumabani kwa Sadi mara , akatokea yule Mama wa Kenya kichawi,akiwa uchi wa mnyama ,akaniambia kua natakiwa kujenga mahusiano na huyu kijana Sadi ili nimuandae mapema kwaajili ya kuja kumtoa sadaka Kama alivyo sema mkuu kwenye kikao. Nikasema kua ni sawa Ila huyu kijana Mimi nimesha anza kumpenda kweli Sasa nitawezaje kweli kumuua? 

"Utaweza tu Chuma we jitahidini tu uishi nae  ,na. Uzae nae mtoto mmoja Kisha ,ndio unamtoa sadaka ."

" Sawa mama nimekuelewa"

Yule mama akapotea ghafla,! Mara Sadi nae muda uleule akaingia. 

Tukala chakula Kisha tukawa tunaongea mambo mbalimbali yakiwemo ya kufahamiana zaidi.


" Sadi nikikupa nafasi ya kuchagua ,kua Mimi niwe ,rafiki yako tu,au ndugu yako ,au Dada yako,au jirani yako! Au mpenzi wako! Je,wewe utachagua nafasi ipi kati ya hizo?"

"Duh ! Kwa kweli kabisa kutoka moyoni ,Mimi nitachagua uwe mpenzi wangu wa pekee! "

"Basi karibu moyoni mwangu Sadi,nimeamua kukukabidhi moyo wangu mwepesi Kama karatasi, tafadhari usije ukanisariti Sadi."

" Chuma wacha kunitania bana ! Hivi ni wewe unae ongea hivyo au!"

"Sadi sijachanganyikiwa naongea nikiwa namaanisha au hunipendi, Kama hutaki Basi wacha niondoke!"

"Hapana Chuma ,unajua siamini kabisa lakini Kama unaniaminisha hivyo! Basi na Mimi nasema kua , nakupenda kweli na ikiwezekana hata leo amisha mizigo yako hapa tuanze maisha yetu.

    

Sadi bila kujua kua anamkaribisha shetani ndani,na pia ana mkaribisha ezraeli mtoa raho yake,ana amua kumchukua Chuma na kwenda nae mpaka kule gesti alipo panga,atamsaidia kubeba mizigo yake ,na Chuma Sasa  rasmi ameamia kwa Sadi Kama kuishi Kama mke na mume huku Chuma akiwa na  mipango yake ya maangamizi........................


Itaendelea..............

Je, Chuma atafanikiwa mipango yake ya kumtoa kafara Sadi? ,Je Chuma ataweza kulipa kisasi kwa mzee foya na yule mganga wa mgeta Alumbile Kalumba? Kwa uweza wa Mungu tutakutana Tena katika episode ya 10 ya  URITHI WA BIBI.

URITHI wa Bibi 15

 Story... URITHI WA BIBI EP.15. Mwisho. Mtunzi....Steven Morgan πŸ“²......... 0659115223 Naam kwa Mara nyingine tena ndugu msomaji tumekutana ...