story : URITHI WA BIBI. EP.2
( Grandmother's inheritance.Ep.2)
Author : Steven Morgan
Email : stevennemes2k@gmail.com
Kabla hatujaendelea ngoja tukumbushane kidogo pale tulipoishia.
Ndugu msomaji tumeona jinsi binti chuma mashaka anavyo fundishwa jinsi ya kuendesha aina za ndege za kichawi .Tumeona kati ya mifagio miwili, mkubwa wa nje wa chelewa na mdogo wa ndani wa ukindu pamoja na ungo, vyote vikiwa ni aina za usafiri wa kichawi.Tumeona bibi yake na chuma amechukua ungo na kuweka manjonjo yake kisha kwa pamoja na mjukuu wake chuma walianza kuyakata mawingu kwa raha zao! Lakini baadae bibi aliamua kumpeleka mjukuu wake kenya ,kwa usafiri wa ungo ,lakini mambo yalikua mabaya kwani baada ya kufika kwenye anga la kanisa moja la kiroho mjini Nairobi, ndege yao iliyumba na wote walishuka chini kwa kasi pamoja na ungo wao.!! Lakini bibi ghafla alipaa juu na kutoweka kabisa maeneo yale ,alibakia mjukuu wake Chuma ambae ndio siku yake ya kwanza katika shughuri za uchawi.Masikini chuma amebakia yeye mwenyewe akiwa uchi wa mnyama pamoja na ungo wake asijue cha kufanya ndani ya uwanja wa kanisa la kiroho.Ikiwa ni bado usiku sana chuma akatulia akisubiri asubuhi ifike ili azijue mbivu na mbichi.
Nini kiliendelea? Chuma anaendelea kusimulia Endelea nayo.
Nikiwa bado nipo nje ya kanisa la kiroho nikihangaika,lakini hakuna nilicho kifanya zaidi ya kubakia palepale ,nililitazama lile kanisa, kwa juu lilikua limeandikwa (Kenya assemblies of God - Buruburu). Usiku ule wote ukaniishia mimi yani kama waswahili wanavyosemaga kua ,usiku wa deni haukawii kucha (the night of debt does not last long), ndivyo ilivyokua ,asubuhi ikafika ,maana nilianza kusikia sauti za ndege wakilia na majogoo yakiwika.Lakini kuna sauti nilikua nikiisikia ikipenya masikioni mwangu kama sauti ya bibi! Ikiniambia "chuma ili upate msaada ,inakupasa ulale kifudifudi muda wote yani ulalie tumbo,kinyume na hapo utaumbuka,zingatia hilo sasa" sauti hii ilikua ikijirudia rudia mpaka masikio yalikua yanauma . Kulizidi kupambazuka na kua kweupe,!! Ghafla nikasikia mayowe mtu akiita "jamani mje mjionee maajabu,mchawi amenasa hapa kanisani!!" Nilishtuka sana,kumbe alikua ni mlinzi wa kanisa tayari ameshaniona!! Haraka nikalala kifudifudi huku furushi langu la makalio yakiwa juu na ungo ukiwa pembeni.Watu walijaa sana,kila mtu alisema lake huku mwingine nilimsikia akisema "jamani afu mchawi mwenyewe ni binti mdogo sana,bado mwali alafu ana umbo zuri!!"
Sikuyajari maneno yao ,mimi niliendelea kulala kifudifudi huku watu wakiendelea kuyashangaa makalio yangu yalio chafuka kwa vumbi na maungaunga ya kichawi. Nilijisikia vibaya sana ila sikua na namna. Mara nikamsikia mtu akiongea na simu.."haloo mchungaji,wahi kanisani,kuna mchawi mtoto ameanguka" Nilishtuka tena kwa presha baada ya kusikia kua mchungaji anakuja!! Niliona sasa huo ndio mwisho wangu! Watu walizidi kujaa na mimi nilizidi kuduwaa huku nikiwa nimelala chali.
Huwezi amini ghafla nikamwona mmama mmoja akipenya kwenye ule umati wa watu na kunijia mimi huku akiwa uchi !! Bila shaka alikua haonekani na watu wengine zaidi yangu.sura yake ilikua ni ngeni kwangu ! Lakini akaja akaniezeka kibao kimoja cha makalio kisha akaniambia kua ninyanyuke tuondoke kwani hakuna mtu anaeniona kwa sasa!! Nikweli sikuonekana maana ghafla! Niliwasikia watu wakisema huku wakikimbia kua "ameyeyuka" "jamani ameyeyuka yeye na ungo wake!!" Kiukweli sikuyeyuka bali,nilipotea kwenye macho yao kimiujiza baada ya yule mama kuja kunigusa na kuninyanyua.kiukweli yule mama alie nisaidia ,alikua ni mchawi wa kulekule kenya ! Ila amenisaidia kwa kunipa nguvu tena za kichawi .Ngoja nitoboe siri moja hapa,kwamba mchawi yeyote anapokwama sehemu,asipolala kifudifudi ,hawezi kupata msaada kutoka kwa washirika wenzake labda ajiokoe mwenyewe.
Basi watu wakawa wanatimka huku na kule huku na sisi taratibu tukaondoka kwa miguu mbali kidogo na kanisa nikiwa na yule mama,wote tukiwa uchi na kuto kuonekana (invisible). Yule mama aliniambia kua nisiogope ,kwani atanisaidia kurudi nyumbani Tanzania.Nikiwa nimeshika ungo wangu yule mama ,akanikumbatia ,ghafla tukapotea nikaja kushtuka ,nikajikuta nipo ndani ya nyumba ya yule mama . "Itakubidi leo ushinde hapa kwangu mpaka usiku Ili niandae usafiri wa haraka kwaajiri yako."yalikua ni maneno ya yule mama nami,sikua na lakusema zaidi ya kumshukuru.yule mama hakutaka kunijua sana zaidi ya kutambua kua Mimi ni mshirika mwenzake. Ikawa hivyo ,nilishinda kutwa nzima kwa yule mama!! Mpaka giza likaingia ,ilikua ni usiku wa saa mbili, Kama kawaida yule mama aliingia ndani na kutoka na fagio kubwa la njelewa likiwa na mpini mrefu ."Binti unajua kuendesha usafiri huu?" Aliniuliza. "Hapana mama ,Mimi bado mgeni Sana kweye hayo mambo " nilimjibu. " Sawa ,Sasa ngoja kwanza nikuandalie chakula Cha kichawi ,maana huwezi kunitembelea ,alafu uondoke bila kula hata supu." Nilishtuka sana .. "chakula Cha kichawi?" Nilimuuliza. " Ndio ,kwani hujawahi kula? Mbona unaonekana kua ni mgeni sana?" Aliniuliza.. "ni kweli mama yangu ,ndio kwanza siku yangu ya kwanza leo,bibi yangu alinibeba,hivyo Sijui mengi sana!!" Nilimjibu yule mama. Yule mama akacheka sana ,Kisha akaingia tena chumbani kwake na kutoka na bakuri kubwa la aluminium,likiwa limejaa nyama nisio ijua na mchuzi mwingi ila ulikua mwekundu sana.
"Kunywa na kula hizi nyama ,kutakufanya wewe uwe na nguvu nyingi,hebu kula kwanza alafu ntajua Cha kufanya!" Alinifosi kunywa ile supu,niligoma lakini akanifosi mpaka akaninywesha! Sio Siri ule mchuzi ulikua mtamu sana,japo ukiutazama ilionekana kua ni damu kabisa.sikua na jinsi ,kwakua nilikua na njaa Kali,nikala na zile nyama zote,nazo pia zilikua tamu sana ,yani utamu wake sijui nifananishe na mnyama gani!!!
"Vizuri Sana binti, unaonekana ni muelewa Sana ,Sasa usafiri uko tayari lakini kabla hatujaondoka inatakiwa twende tukawachawie watu kwanza (kuwanga) ili kupata nguvu zaidi!" Aliongea yule mama huku Mimi nikitikisa kichwa ,kama ishara ya kumkubalia.
Yule mama akiwa uchi kama mimi lakini ukimtazama alionekana Kama amevaa kaniki ,alinichukua nakutoka nje ya nyumba yake,akanishika mkono Kisha akapiga mguu chini kwa nguvu!! Ghafla tukajikuta tupo kwenye mitaa flani huko ulaiyani kwenye makazi ya watu. Tukaenda kwenye nyumba moja ambapo tulitua juu ya paa,kwakua ilikua mapema Kama usiku wa saa tatu hivi, wenye nyumba walikua bado hawajalala ila watoto zao baadhi walionekana wamelala vyumbani. Kwakutumia maneneo makali ya kiimani tuliweza kuingia ndani bila ya kufungua milango,tulifikia sebuleni ambako tulimkuta mtu na mke wake wakitazama sinema runingani.Tukaanza kuwazunguuka kwa kuwasoteasotea na makalio.Kuna muda Kama walikua wakihisi Kama kuna Jambo linatendeka! Lakini hawakua na uhakika .Nilimsikia yule mzee akimwambia mkewe .. "mbona nyumba imekua nzito ghafla? itakua kuna wachawi wameingia mke wangu,hebu niletee ile biblia yangu." Tuliposikia habari ya biblia tukashtuka automatic na kujikuta tupo nje juu ya paa, kule ndani walianza kufanya maombi mazito wakilitaja mara nyingi jina la Yesu na Mungu baba. Sio Siri tulipata tabu Sana , nikajihisi Kuungua mwili mzima ,yule mama akanishika mkono ,tukakimbia huku atua zetu zikisikika kwenye mabati ,tuliruka na kupaa Kama ndege na kwenda kutua barabarani. Asikudanganye mtu,neno la mungu ni kiboko ya wachawi haswa unapomtaja mara nyingi bwana yesu na Mungu baba,mchawi hawezi kukukalia karibu.
Basi baada ya hapo tukaenda kwenye nyumba nyingine ambapo ile tunatua tu kwenye paa,tulihisi Kama tumekanyaga misumari ya Moto !! Haraka tena tukakimbia kwa kuruka juu na kutua mtaa wa pili!! Nikaamua nimuulize yule mama kua inakuaje lile paa linaumiza namna ile? Akaniambia kua yule mwenye nyumba aliweka chumvi ya mawe batini ndio maana ilitupa shida.Hapa naomba nikufafanulie kidogo ndugu msomaji kuhusiana na chumvi ya mawe. Chumvi ya mawe ni ulinzi mkubwa sana wa nyumba yako Kama hutaki wachawi wakujie.Unaweza kuchukua chumvi kidogo ukanuiza na maneno kidogo alafu ukairusha batini ,hapo mchawi hawezi kuingia ndani,au ukachukua chumvi kidogo alafu ukaiweka kwenye kila pembe au cona ya nyumba yako ,hapo pia mchawi hawezi kuingia wala kutoka .Au ukachukua chumvi ya mawe na kuiweka kwenye mvungu was kitanda unacho lalia ,hapo mchawi hata Kama ameingia ndani,lakini hatoweza kukusogelea au kukugusa.Huwezi amini lakini ukweli ndio huo ,Kama unasumbuliwa Sana na wachawi, fanya hivyo ,utalala vizuri sana bila kuchezewa.Kama uhamini ngoja nikuhaminishe kitu, je,umeshawahi kujiuliza kua ,ni kwanini kanisani maji ya baraka wanaweka chumvi na sio sukari? Jiulize vizuri ndio utahisi kua chumvi ya mawe ina Siri nzito kuliko haya niliyo kueleza.
Basi tukiwa bado tupo pale njiani Mimi na yule mama mkenya,tukawaza Cha kufanya nini, mwisho yule mama akasema kua twende kwenye nyumba ya mwisho kwa kijana mmoja hua anaringaga Sana wacha tukamkomeshe.Tulishikana mikono na kuruka juu sana na tulipotua , tulitua kwenye paa la nyumba la huyo kijana.Mama akanyoosha mkono juu ikaja dawa flani ya ungaunga akaiweka batini nyingine akaipeperusha kwa kuipuliza .Kisha akasema kua Mustafa hajalala bado ,huyu kijana ni mbishi Sana,ila muda si mrefu atalala tu. Tukasubiri kidogo baadae tukaingia ndani tena chumbani kwa yule kijana! Tulimkuta akiwa amevalia bukta huku akiwa tumbo wazi na mikono yake ikiwa nyuma Kama ameficha kitu . Niliogopa Sana kwani yule kijana alikua akitutazama sana mpaka nikahisi kua huenda ikawa anatuona. "Mama mbona huyu kijana anatushangaa Sana! Au anatuona?" Nilimuuliza mama .. " mh! Sidhani Kama atakua na uwezo huo!" Alijibu mama kwa hofu. Lakini tulipo angalia pembeni mwa kile chumba tukayaona marimao kadhaa na sindano zikiwa zinaning'inia juu yake! Mama alishtuka Sana Kisha akasema " tukimbie tunaonekana!!" Wakati huo yeye tayari ameshapiga guu lake chini na kutoweka peke yake.Na Mimi nilitaka kufanya hivyo, lakini kabla sijanyanyua mguu yule kijana alinikamata na sikuwa na ujanja tena!! .
Nilijiona mtu mwenye mikosi Sana kwani ,kila mara Mimi ndio wa kukamatwa tu! Kumbe yule kijana aliweka mtego wa kuona wachawi .Hata wewe ndugu msomaji endapo utachukua malimao au ndimu Saba,na sindano za kushonea nguo kwa mkono saba, Kisha ukachukua kila sindano moja ukaichomeka kwenye ndimu au rimao lake ,usiikandamize Sana,choma juu juu ili sindano ining'inie Kisha chukua hizo ndimu weka eneo ambalo upo Kisha tulia,hapo unaweza ukaona vitu vilivyo jificha visionekane kwa macho.(invisible) Lakini nikuonye usije ukafanya zoezi hili Kama una roho nyepesi ,maana wachawi huwa wanatisha Sana wanapokuja kwako.Kabla hujafanya hivyo jiulize kua baada ya kumwona mchawi utamfanya nini? Je, unaweza kumkamata akiwa na sura ya kutisha? Kama huwezi usijaribu ni hatari Sana.
Basi,nikiwa mikononi mwa yule kijana Mustafa ,sikua na ujanja kwani mchawi ukisha kamatwa huwezi fanya lolote zaidi ya kuokolewa baadae na mchawi mwenzio. " unaitwa nani wewe binti?" Ilikua ni sauti ya ukari ya yule kijana aliniuliza. " Naitwa chuma" nilimjibu. " Chuma! Hahahaha haa! Chuma leo hunaga bahati " alishangaa yule kijana Kisha akasema .." chuma wewe unaonekana ni binti mzuri Sana ,una umbo zuri ,makalio makubwa Sasa kwanini,unakua mchawi ? Ona Sasa ulivyojiweka Kama kinyago Wakati wewe ni mrembo!!!" Yalikua ni maneno ya yule kijana Mustafa. Mimi sikujibu chochote zaidi ya kuinamisha kichwa chini kwa haibu!! " Sasa nikufanye nini binti chuma?" Aliniuliza lakini nilinyamaza kimya . Sauti ya hajabu ikapita masikioni mwangu kua nilale kifudifudi ili nipate msaada ,nami nikafanya hivyo muda uleule ,yule kijana Mustafa alishangaa Sana kua nina maana gani ya Mimi kulala pale sakafuni kifudifudi huku makalio yangu yaliyojaa minofu yakiwa juu yakitikisika. " We binti ndio nini Sasa?, Au una nitega? Nitakubaka kweli Mimi mwenyewe nimedata vilevile!" Nilishtuka nilivyosikia yule kijana Mustafa anataka kunibaka ,nilimtazama nikaona taratibu bukta aliyovaa inanyanyuka juu yani tayari alishakua na hisia Kali na Mimi japokua nilikua Kama kinyago lakini Mustafa alivutiwa na Mimi,ama kweli huyu kijana ni jasiri Sana kwa mtu mwingine huwezi kunitazama mara mbili,nilitisha sana.
Taratibu Mustafa akaanza kunisogelea pale nilipolala na akaanza kuyachezea makalio yangu ,nikajua Sasa muda si mrefu huyu kijana atanibaka !!
Nikatulia Kama maji ya kisimani,ghafla mbele yangu namwona yule mama mkenya ananipa mkono ,nami nikamshika mkono tukapotea na kuibukia nyumbani kwa yule mama mkenya. " Pole Sana binti,hizi ni ajari ndogondogo huwa zinatokeaga maana siku hizi watu wengi wanajua jinsi ya kujikinga na wachawi." "Asante mama " nilijibu.." ehee! Nambie ,vipi yule kijana Mustafa mbona alikua anakuchezea makalio alikua anataka kukufanya nini? ". "Alikua anataka kunibaka !!" Nilimjibu . " Kukubaka? Huyu kijana ana hatari kweli na angesubutu kufanya hivyo, basi jua la asubuhi ,asingeliona tena,angekufa.! Alishtuka yule mama alivyosikia kua nilitaka kubakwa ningari kwenye hari ya vazi la kichawi. Baada ya hapo yule mama akauchukua ungo wangu na kuupigia maombi maarumu Kisha ule ungo ukapotea kimiujiza. Kisha akachukua lile fagio lenye mti au mpini mrefu akanishika mkono ,akapiga guu lake chini tukatokea njia ya panda .Akaniambia Sasa muda wa kurudi nyumbani Tanzania umefika.Ilikua bado ni usiku Sana Kama Sasa nane hivi! Baada ya hapo akaulaza ule mfagio chini Kisha akanipaka dawa flani nayeye pia akajipaka Kisha tukaukalia ule mfagio.sijui nini kilitokea lakini tukajikuta tupo juu ya anga kwenye spidi Kali zaidi ya ndege za kivita!! Haikuchukua dakika nyingi tukajikuta tupo nje nyumbani kwa bibi. Bibi alitoka nje akiwa kwenye hari yake ya kichawi,akatupokea na akamshukuru Sana mshirika mwenzake raia wa Nairobi Kenya. Yule mama hakutaka kukaa Sana alituaga na akaondoka na usafiri wake kwa haraka.
*********** ITAENDELEA ***************
Je,nini kitafuatia? Usikose kufuatilia sehemu ya tatu ya URITHI WA BIBI.Uhondo ndio kwanza unaanza. Hujachelewa, fanya ku LIKE PAGE, COMMENT , au SHARE ili wengine wapate kuburudika na kuelimika pia.Asante.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni