Story .......... URITHI WA BIBI EP. 6
Author..............Steven Morgan
Contact : ...WhatsApp.. +255 659 115 223
Naam ,kwa mara nyingine tena kwa neema za mungu tumekutana tena katika sehemu ya sita ya story yetu. Tumshukuru Kwanza mungu kwa neema zake pia atusamehe pale tulipokosea na awasamehe pia wale wanao endelea kutukosea maana hawajui wanayo yatenda. Hatupaswi kuhukumu anaye hukumu ni Mungu pekee,sisi yatupasa kujirinda tu dhidi ya wale wabaya.
Nb: Tumtangulize Mungu kwa Kila Jambo maana, Yeye ndie muweza wa yote.
Story yetu tulipoishia ndipo tunapo anzia ili twende sambamba.
TULIPOISHIA....👇
Mama mwenye nyumba alinielekeza mambo mengi haswa majukumu ya kazi. Nikaingia chumbani kwangu nikabadirisha nguo,Kisha nikatoka nikiwa na kanga moja ambayo imenichora umbo langu la mwili haswa makalioni ambapo sio siri ,sijisifii kweli Mungu amenibariki minyama ya makario.
Nikakatiza pale sebureni ambapo alikaa baba mwenye. Nyumba na mkewe . Nilijisahau nilijua kua bafu na choo vipo nje hivyo, nilitaka kutoka nje. " Wewe binti vipi! Mbona hivyo?" " Naenda kuoga mama!" " Wewe si nilikwambia kua bafu na choo vipo chumba Cha tatu pembeni? Sasa huko nje unaenda wapi! Au umeshazoea huko kwenu vijijini milimani huko?
" Nilijisahau tu mama samahani!" " Sawa Chuma tumekuelewa nenda tu kaoge mama!!"
Aliongea mzee Foya huku akinitazama kwelikweli. Basi nikageuka na kuelekea huko bafuni . " We baba Maria vipi? Mbona unamtazama Sana yule binti kwa nini?"
Nilimsikia mama mwenye nyumba akimsema mmewe kua alikua akinishangaa Sana. Nafikiri ni kwa sababu ya ile kanga niliyovaa na umbo langu ,lilimpa shida Sana.
Basi nikaelekea bafuni ,ile nafungua mlango tu!
Namwona bibi yuko kule bafuni,kiukweli nilishtuka Sana ,ilibaki kidogo tu ,nipige kelele.
" Tulia Chuma, nimekuja tu kuona unapokaa ,ni pazuri Sana, nafikiri tutaonana baadae ,mida ya kazi,kuna kazi ya kufanya leo". "sawa bibi"
Bibi alitoweka Kisha nami nilioga na kuondoka chumbani kwangu.
Ile naingia chumbani tu! Nakuta kioo kipo kitandani kwangu. Kioo hiko hakikua kigeni kwangu kwani nilikitambua vizuri tu ,kua ndio kile alichonipa Bibi na nilikiweka kwenye begi langu ,Sasa sijui kilitoka vipi kukaa pale kitandani.!! Nikakisogelea Kisha nikakitazama ,nilichokiona ni tofauti na nilicho kitarajia! Nilijua nitajiona Mimi mwenyewe,lakini, huwezi amini,nilimwona Bibi zubeda wa kule kwetu morogoro, ambae ana undugu na mzee Foya, na mzee Foya ndipo alipofikia kwa Bibi zubeda ambapo siku moja kabla ya kuja huku dar tulienda na Bibi kumwangia mzee Foya na ndipo nilipo kwama kwenye tumbo la mzee Foya.
Sasa tuachane na hayo,turudi pale ndani chumbani kwangu ,nilizidi kukitazama kile kioo,nikamwona Bibi zubeda akiniteta na jirani yetu mmoja wa kulekule nyumbani . Huyo jirani alikua anaitwa mama majuto ,alimpelekea umbea Bibi zubeda kua eti Mimi na Bibi yangu ni wachawi Sana na pia ikiwezekana, wamwambie mzee Foya kua Mimi ni mchawi anifukuze. Kama nilivyo eleza hapo mwanzo kua ,kioo ni msaada mkubwa Sana kwa wachawi,nimeweza kumwona Bibi zubeda kwenye kioo changu Cha kichawi kwa sababu yule Bibi zubeda na mwenzake walikua wakizungumza sehemu ambayo kulikua na kioo kilichokua wazi yani hakikufunikwa. Kwa hiyo kwetu sisi inakua ni Kama CCTV camera.
Basi baada ya hapo Sura ya Bibi zubeda na mwenzake zikapotea Kisha ikaja sura ya mkuu wetu wa uchawi, mkuu alinikazia macho Kisha akasema ," Chuma nadhani unajua Cha kufanya" Kisha mkuu akapotea.
Nikamwita Bibi zubeda kwenye kioo akatokea tena. Nikachukua begi langu Kisha nikatoa mdori wa kike, nikaanza kuukaba kwenye shingo ule mdori huku nikinuiza maneno ya ufundi. Mara nikaanza kumwona Bibi zubeda kwenye Koo akijishika shingo huku akitoa macho ,kuhashiria maumivu makari. Alihangaika mpaka alianguka chini ,huku Mimi nikiwa bado naendelea kumkaba yule mdori ,mwishoni nikamnyonga shingo ya Yule mdori ,na Bibi Zubeda nae alijinyoosha palepale. Yani nimuua kabisa asije akaniharibia kwa bosi wangu Foya.
Nikachukua kile kioo na kukirudisha kwenye begi, nikikabadili nguo Kisha nikatulia kitandani. Mara nikasikia mama Maria yani mama mwenye nyumba ananiita, " Chuma , Chuma toka uje tule " kumbe mama alikua amesha pika ,nikatoka kuelekea sebuleni, ile nafika tu sebuleni, mara namwona ..................................
ENDELEA 👇
"Chuma,chuma toka nje uje tile"
Kumbe mama alikua amesha pika ,nikatoka kuelekea sebuleni, ile nafika tu sebuleni, mara namwona Bibi amekaa pale kwenye Kochi katikati ya mzee foya na mkewe bibi nae aliketi. Nilishtuka sana mpaka mama Maria na mumewe mzee foya au baba Maria walishtuka sana. " Vipi Chuma mbona umeshtuka ghafla kwa hofu ? Vipi! ". Alihoji bosi wangu mama Maria mke was mzee foya. " Hapana mama niko sawa tu!" Nilijibu kwa mkato Kisha nami nikaketi kwenye Kochi la mtu mmoja lililokua pembeni.
Nikajisevia chakula pale mezani Kisha bibi nae akajisevia chakula chake bila ya kuonekana na mtu. Mimi pekee ndio nilie kua namwona bibi. Wakati wote tunaendelea kula ,bibi aliniongelesha ,na Mimi pia nilimjibu yani tulikua tunaongea kwa sauti bila ya mtu mwingine kujua. Hapa utashangaa kua kwanini wengine hawakujua kua Mimi naongea na mtu mwingine? Kiukweli mchawi huwa aongei taratibu yani hanong'oni ,kwani kama mchawi akijaribu kunong'ona basi Kila mtu anaweza akamsikia. Ndomana Mimi na Bibi tulikua tunaongea kwa sauti ili tusishtukiwe .
" Vipi Chuma mbona unakula huku unaimba ,utajing'ata shahuri yako!!"
Aliongea mama Maria. Lakini kiukweli nilikua siimbi wimbo wowote ila ,nilipokua nanyanyua mdomo na kuongea kwa sauti na bibi, kumbe wao walinisikia ila walinielewa tofauti yani wao walinisikia kama vile nilikua naimba kumbe nilikua naongea na bibi ambae wao hawaku muona.
Mimi na bibi tuliendelea kuongea mambo mengi haswa yale mauaji ya Bibi zubeda tuliyo yafanya jioni ile .
Baada ya hapo bibi akachota ubwabwa tonge moja kwenye sahani ya mke wa mzee foya yani mama Maria Kisha akalimeza lile tonge Kisha bibi aka anza kujibinya binya tumbo kama vile linamuuma. Mara ghafla! Mama Maria bosi wangu nae akaanza kujishika tumbo na kugugumia maumivu ya tumbo. Kumbe bibi alipochota lile tonge na kufanya alivyofanya, alimroga yule mama mwenye nyumba, ila huu urogi mdogo tu wa kumshikisha mtu adabu hauna madhara sana zaidi ya kuumwa na tumbo na mwishowe kuharisha.
Ndugu msomaji bila Shaka kama utakua umewahi kula chakula alafu baada ya muda mfupi tumbo likakuuma sana tena sana mpaka unaacha chakula na kwenda kulala kidogo ili ujinyooshe upate nafuu.
Sasa hari kama hiyo huwa mara nyingi husababishwa na wachawi yani ukiona hivyo ujue, ulipokua unakula ,mchawi alikuja na kukitemea mate chakula chako Kisha akakuroga tumbo.!!!
Hapa naomba niwasaidie kidogo kuepukana na hatari hii. Dawa pekee ya kuepukana na mchezo huu ni, kama wewe ni mcha Mungu,Kabla ya kula kiombee chakula kwanza kwa imani yako Kisha endelea kula ,utakua salama. Lakini pia kwa wale wasiojua hata maana ya kusali na kumwomba Mungu basi, hakikisha unapokula chakula chochote unatumia kijiko cha Chuma na usipende kula chakula ukiwa nje ( hadharani) pendelea Kula chakula ukiwa ndani na usisahau kutumia kijiko ,utakuwa salama katika janga hili.
"Chuma hebu mwangalie mama amepatwa na nini?" Ilikua ni sauti ya mzee foya. "Sawa baba" nilimjibu kwa mkato Kisha nikaanza kumwangalia mama Maria,muda huo bibi alikua akicheka na kung'ong'a kwa kukenua kenua meno huku akiwa kwenye muonekano wa kutisha kwelikweli.
"Chuma naomba uninyanyue taratibu unipeleke chooni " mama aliongea Kisha baba nae alinyanyuka tukasaidiana kumnyanyua na kumpeleka chooni. Tukamwacha huko chooni huku sisi tukiwa sebuleni tunamsubiri. Muda huo watoto walisha lala muda Maria na kaka yake Matias.
"Chuma hebu wachukue hawa watoto kawalaze chumbani kwao." "Sawa baba" nilimjibu bosi Kisha nikaanza kumnyanyua Maria nikampeleka chumbani kumlaza Kisha nikamrudia Matias lakini wakati namrudia matiasi ,bibi pale alipokaa kwenye kochi bado alikua akiendelea kucheka sana Kisha akanioneshea ishara ya kuniaga Kisha akatoweka. Wakati namnyanyua mtoto Matias,simu ya bosi ikaita ,wakati bosi anaongea na simu Mimi nilisha ondoka kumlaza Matias chumbani. Ile natoka kuja tena sebuleni,namkuta bosi mzee foya analia machozi mwamwamwa.. " bosi vipi tena kulikoni?" Nilimuuliza ili nijue kinacho mliza ni nini? Japo moyoni nilijua nini kinacho endelea.
Alizidi kulia mpaka alianguaka chini na kugalagala!!!!
Mara ghafla akaja mkeo mama Maria kutoka kule chooni alipokua baada ya kusikia sauti ya mmewe akiria. Lakini baada ya kufika yeye, mmewe alinyamaza na akawa anamshangaa mkewe. Mimi na mama Maria pia tukawa tunamshangaa baba Maria kwa kua alikua akiria sana alafu akanyamaza ghafla kulikoni!!!
" Baba Maria mbona sikuelewi? Unachoriria ni nini? Na kilicho kufanya unyamaze ni nini?"
"Mama Maria ! Kwanza Kabla ya kukuambia ninacho lilia ! Naomba kwanza nikuambie kilichonifanya ninyamaze ghafla!!"
"Sawa baba Maria nakusikiriza" alijibu mama Maria.
" Mke wangu, Mimi na chuma tulikupeleka chooni ukiwa hata kutembea huwezi! Sasa imekuaje umekua na nguvu za kutembea kwa haraka ukaja hapa sebuleni mwenyewe?"
" Baba Maria,baada ya kula kile chakula,tumbo lilianza kuniuma sana Kisha nikahisi kama vile nataka kwenda haja kubwa. Lakini ,mliponinyanyua na kunipeleka na kuniacha kule chooni,hakuna nilicho kinya zaidi ya kutoa upepo muda wote Kisha tumbo limetulia!! Haya Sasa nambie wewe unachoriria ni nini?
Mzee foya kabla hajaanza kuzungumza ,akaanza kulia tena huku akimtaja bibi zubeda wa morogoro.
"Jamani bibi zubeda wa morogoro,amefanya nini?" Aliuliza mama. "Sijui" nilijibu Mimi kwa ufupi. "Amefariki masikini wa Mungu!!!" Baba alionge kwa uchungu mkubwa. " Amefariki?" Alijibu mama kwa kushangaaa sana. " Ndio amefariki jioni hii hii ya leo,amekutwa ndani kwake ameanguka chini na kufariki " alizidi kuongea mzee foya. "Alikua anaumwa?" Aliuliza mama. " Hapana kifo chake Wala hakijahusika na kuumwa itakua ni mambo ya ushirikina,na nikomgundua mtu alie husika na kifo hochi,basi na yeye nitamfanya mfu."" Aliongea mzee foya kwa uchungu
Mzee foya baada ya kuria kwa muda mrefu kutokana na taarifa ya kifo cha bibi zubeda wa morogoro,alinyamaza Kisha akamwambi mkewe aketi chini wazungumze kua itakuaje?
" Mke wangu kesho inabidi niwatangulize huko morogoro kwenye msiba mapema,lakini Mimi nitakuja jioni sababu kuna sehemu nitapitia kutafuta ukweli wa kifo cha ndugu yangu bibi zubeda. Na nikimjua hadui alie husika ,hama zake ,hama zangu." Mzee foya aliongea kwa hasira sana,huku Mimi na mama Maria tukiwa tumetulia kama tumezubaa vile. Basi kwa kua muda ulikua umeshaenda,Kila mtu aliingia chumbani kulala............. ............ .................. .....
ITAENDELEA.
Je,mzee foya atagundua chanzo cha kifo cha ndugu yake Bibi zubeda? Je, na kama atamgundua hadui alie husika ,nini atakacho kifanya? Hayo na mengine mengi usikose kufuatilia sehemu ya saba ya URITHI WA BIBI.
Naamini kwa uweza wa Mungu tutakutana tena kipindi kijacho kunako majaariwa. Maarifana uhondo ndio kwanza unaanza ,Wala hujachelewa,mambo ni mengi sana ,muda ni mchache.
Nb:Mtangulize Mungu kwanza kwa Kila Jambo.🙏