Story......... URITHI WA BIBI EP . 10
Mtunzi : Steven Morgan
Contact : +255659115223
Naam, ndugu wasomaji karibuni Tena katika muendelezo wa story yetu . Japo mwendo wa kinyonga lakini tutafika. Pia unaweza kunipiga teke, kwa kunichangia kikombe Cha kahawa π·Cha Mia tano tu! Ili mniongezee meendo wa kuwaletea Mambo mazuri . Sio lazima ila ukijisikia kwa moyo ..... +255659115223 tigo pesa.
Tuachane na hayo ,Sasa turudi kwenye story yetu.Kama kawaida tulipoishia ndipo,tunapoanzia.
ILIPOISHIA EP9...
Sadi nikikupa nafasi ya kuchagua ,kua Mimi niwe ,rafiki yako tu,au ndugu yako ,au Dada yako,au jirani yako! Au mpenzi wako! Je,wewe utachagua nafasi ipi kati ya hizo?"
"Duh ! Kwa kweli kabisa kutoka moyoni ,Mimi nitachagua uwe mpenzi wangu wa pekee! "
"Basi karibu moyoni mwangu Sadi,nimeamua kukukabidhi moyo wangu mwepesi Kama karatasi, tafadhari usije ukanisariti Sadi."
" Chuma wacha kunitania bana ! Hivi ni wewe unae ongea hivyo au!"
"Sadi sijachanganyikiwa naongea nikiwa namaanisha au hunipendi, Kama hutaki Basi wacha niondoke!"
"Hapana Chuma ,unajua siamini kabisa lakini Kama unaniaminisha hivyo! Basi na Mimi nasema kua , nakupenda kweli na ikiwezekana hata leo amisha mizigo yako hapa tuanze maisha yetu.
Sadi bila kujua kua anamkaribisha shetani ndani,na pia ana mkaribisha ezraeli mtoa raho yake,ana amua kumchukua Chuma na kwenda nae mpaka kule gesti alipo panga,atamsaidia kubeba mizigo yake ,na Chuma Sasa rasmi ameamia kwa Sadi Kama kuishi Kama mke na mume huku Chuma akiwa na mipango yake ya maangamizi........................
Endelea..
Basi ,maisha yaliendelea kati ya Chuma na Sadiki au Sadi. Imeshapita Sasa takribani mwaka mmoja. Lakini Chuma hakupata mtoto bado !
Siku moja hasubui na mapema Sadi aliamka mapema ili ajiandae kwenda mihangaikoni,alimwamsha mkewe Chuma.
"Mke wangu Chuma ..!" "Ndio mpenzi nambie" " unajua Chuma huu ni mwaka Sasa lakini !" " Lakini nini?" Alidakia Chuma kwa ukari.
" Lakini sioni dalili zozote za wewe kua ni mjamzito,nimejitahidi kweli lakini sielewi tatizo ni nini!?"
" Kwa hiyo una maana gani?". " Maana yangu ni kutafuta suruhisho la tatizo hili ili nasi tuwe na watoto wetu Kama wengine. Baadae nikitoka mihangaikoni , nitakuja kukuchukua twende tukapime afya zetu za uzazi ili atakae bainika na kasoro, apate tiba ,sawa mke wangu?"
"Sawa Sadi kipenzi ni Jambo jema hilo"
Nilimkubalia mume wangu Sadi,kwa kile anacho kitaka. Lakini kiukweli Mimi ndie nilikua na sababisha Sadi asiwe na uwezo wa nguvu za kiume ili asizae na Mimi maana ,sikutaka mwanangu akose baba maana nilijua kua siku za Sadi za kuishi zilikua zinahesabika. Nilikua na hakika kabisa kua Sadi hawezi kuumaliza mwaka huu. Basi , niliendelea na shughuri za pale nyumbani ,nilipomaliza nikapumzika nikawa naangalia tv. Mara ghafla upepo mkali ulivuma pale ndani vitu vilivyokua vyepesi vilipeperuka huku na kule . Sikuelewa ile hari ni nini? Nilibaki nimeduwaa Kama zoba! Nilikuja kushtuliwa na kofi zito na mtu nisie mjua kwa haraka,mpaka akili zilipokuja kukaa sawa,ndipo nilipojua kua alie kuja pale kwangu alikua ni mkuu amenijia kwa hasira kubwa sana.
" Chuma umejisahau Sana,tunahitaji sadaka yako Sasa,wenzako wote wametoa kasoro wewe Chuma!"
"Sawa mkuu nitatoa naomba nipeni muda kidogo" " Chuma huna Tena muda was kutosha ila kwa heshima ya Bibi yako Mbokeleni nakupa muda wa kutosha ,kuanzia Sasa anza kazi ya kumwandaa mhusika ,sawa Chuma?"
"Ndio mkuu"
Mara ghafla mkuu akapotea ! Nikavuta pumzi Kisha nikaishusha taratibu ,nikawa nahema kwa hofu.
Mtu pekee wa kumtoa sadaka ni Sadiki na si mwingine,nilikataa kumbebea ujauzito sababu nilijua yeye ni marehemu mtarajiwa siwezi kuishi na mtoto asie kua na baba.
Bila kupoteza muda nikaanza maandalizi ya kumdhuru Sadi mume wangu. Nikachukua nguo yake na kuanza kuichawia,Kisha akaja yule Mama wa Kenya palepale . " Naona unaandaa mtego wa kumnasa mnyama wako" "ndio mama lakini hata hivyo nimepungukiwa na sanda ambayo ndio ingekamilisha mtego huu!"
"Usijari Chuma Mimi sanda ninayo ipo nyumbani Kenya,ila ngoja nikuletee ukamilishe mtego wako."
Huwezi amini lakini ndivyo ilivyo kua, sanda ikaja palepale! Baada ya yule Mama mkenya kuiita pale kwa mamraka ya kichawi.
Ndugu msomaji nilipokua naandaa mtego wa kumnasa mtu wangu,si masihara huu ni mtego hatari Sana. Ukiponyeka katika mtego huu ,Basi huwezi kuja kufa kwa kurogwa tena ,utakuja kufa kwa amri ya Mungu tu!!
Nikachukua ile sanda,nikashona suruali kwa sindano na uzi wa mkono. Kisha nikakata upande mwingine wa sanda, nikashona tisheti Kisha tukazipigia ndumba nyingine nikisaidiwa na yule mamangu mkenya. Kisha nikachukua nguo za mume wangu anazo pendaga Sana kuzivaa mara kwa mara. Tukazichawia kisha tukazipoteza kichawi! Zilizo baki pale Sasa ,ni zile nguo za sanda nilimuwekea kabatini mume wangu ili akirudi azivae ,hatoshtuka maana yeye na watu wengine wa kawaida wataziona Kama ni nguo tu za kawaida za siku zote lakini nyuma ya pazia ni sanda.
Baada ya kuweka zile nguo kabatini ,hatua iliyo fuata ni kupanga tarehe na mwezi wa kufa mtu yule katika mwaka huu.Na aina gani ya kifo atakufa mtu huyo?
Ndugu msomaji Duniani Kuna mambo,!
Huu mtego nilio uhandaa,sio Kama namuua moja kwa moja! Bali katika ulimwengu wa kimwili ataonekana amekufa kweli, lakini kiroho na mwili wa kweli tutakua tumeuteka na kuuficha kichawi,mpaka itakapobainika wazi katika jamii kua yule mtu amekufa na amezikwa ndipo sisi tunapoanza kumtumia mtu wetu katika uharisia wake harisi akiwa Kama Msukule.
Basi tukapanga tarehe fulani na mwezi fulani ndio itakapokua mwisho wa Sadiki kuishi Duniani. Zile nguo tulizozitengeneza kwa sanda ,atatakiwa kuzivaa mara40 ,na sisi tutalala matanga siku arobaini ingari yeye bado yupo hai.
Basi mtego ulikamilika ,tukaweka kila kitu sawa. Kwakua muda ulishaenda ,nikapika chakula Cha mchana ,nikamwekea mume wangu Kisha nami nikala na mshirka mwenzangu. Baada ya hapo tukaendelea kupiga story za hapa na pale.
Sasa tuachane na Chuma pale nyumbani ngoja tumwone Sadi katika harakati zake.
Sadiki akiwa na mawazo makubwa huku akitembea barabarani kwa mwendo wa kinyonga,mara ghafla.. ..honi ya gari! Piiii! Piiiiiiii! Piiiipiiipiiiii !!
Nikashtuka Sana maana kiukweli Sadiki Mimi nilisha jisahau Kama nipo barabarani ,mawazo yalini zonga Sana. Mara akashuka mtu mmoja kwenye lile gari lililo paki pembeni baada ya kunikosakosa kunigongea. Alikua ni mbaba mtu mzima ,alivalia suti nyeusi ,akiwa na mwonekano wa kichungaji.
" Kijana habari! Naitwa mchungaji Nelson ,kanisa langu lipo kule maeneo ya segelea."
" Mimi naitwa Sadi au Sadiki naishi kule buguruni na mke wangu."
"Sawa kijana ila unaonekana haupo sawa kabisa je,ni nini shida?"
"Mchungaji, ni kweli Nina shida kubwa sana, Mimi na mpenzi wangu Chuma tumeishi takribani mwaka mmoja Sasa! Lakini mke wangu hata dalili za uja uzito Hana ,nami nataka watoto mchungaji sijui nini shida"
"Usijari kijana hakuna kinachoshindikana Kama tu uta mshirikisha mwenye ezi Mungu! Je, baada ya hapo wewe umepanga kulimaliza tatizo hilo kwa njia gani?"
"Mchungaji,nimepanga hivi ninaporudi nyumbani nimchukue mke wangu niende nae hospitali tukapime ili, atakae bainika na kasoro,atibiwe."
" Sawa kijana,fanya hivyo mara moja ila,mkiona hamjafanikiwa, Basi ,chukua hizi namba zangu zasimu 07xxxxxxxxx. Utanipigia ili kulimaliza tatizo lenu maana hakuna kinacho shindikana Kama ukijikabidhi kwa Yesu kristu awe bwana na mwokozi wako."
" Asante mchungaji ,namba nimeshazisevu nitakutafuta nitakapo kuhitaji ,wacha Sasa nirudi nyumbani."
"Sawa kijana ila punguza mawazo usije ukapata hajari ! Safari njema.
Basi,nika agana na mchungaji Kisha nikapanda bajaji nikarudi zangu nyumbani.
Lakini nilipofika nje ya mlango wa chumba changu nilisikia sauti ya mke wangu na sauti nyingine ya mmama mtu mzima akiongea ,walikua wanazungumza mazungumzo ya kawaida huku sauti ya tv ikisikika kwa mbali.Nilijua mke wanting yupo na jirani yake anapiga stori.
Nikabisha hodi kwa kugonga mlango na kunena kwa sauti.
" Hodi hodi mke wangu,nimerudi mumeo"
"Karibu mume wangu"
Sauti ya mke wangu ilisikika Kisha kimya kingi kilitanda Kisha ghafla nikahisi kichwa kuuma kwa ghafla Kisha nikarudi kwenye hari yangu.
Mara mlango ukafunguliwa na mke wangu nikaingia ndani, kiukweli ndani kulikua kuzito Sana ,nywele zilikua zina nisisimka,lakini pia nilishangaa Sana kutoona mtu mwingine ndani wakati nilimsikia mke wangu akipiga story na mtu mwingine,nikabaki nimeduwaa!!
"Mume wangu vipi ! Mbona upo hivyo?"
"Nashangaa mke wangu,niliwasikia mkiongea huku ndani na mwenzio ,Sasa nashangaa ninavyoona kua upo mwenyewe humu,je ulie kua unaongea nae Yuko wapi? Au umemficha mvunguni?"
"Mume wangu nawe kwa wivu! Humu Wala hakuna mtu labda tv ndio uliyo isikia ! "
" Sawa mke wangu tuachane na hayo,niandalie maji ya kuoga Kwanza mamana nahisi joto Kali Sana."
Nilimwandalia mume wangu maji ya kuoga ,Kisha akaenda kuoga . Nilikua nahofu kumbe mume wangu alitusikia tukiwa tunaongea ,na alipogonga hodi yule mmama mkenya akapotea kichawi ghafla ! Ndo maana mume wangu alihisi kichwa kuuma na kizunguzungu kwa sababu pale ndani kulitawaliwa na nguvu za kiza .
Mume wangu alitoka bafuni Kisha akaja ndani.
" Mke wangu nimeshamaliza kuoga hebu niandalie nguo nzuri za kuvaa na kupendeza"
Kichaa kapewa rungu ,nikafungua kabati na kuchukua tisheti na jinsi, kwa macho zinaonekana hivyo lakini kiukweli ndio zile nguo nilizo zishona kwa sanda !! Nilimpa zile nguo mume wangu,akazivaa Kisha nika mwandalia chakula tukala wote pia japo Mimi tayari nilisha kula. Mimi nikimwangalia mume wangu nilimwona amevaa sanda kabisa juu na chini lakini kwa wewe ndungu msomaji mwenye macho mawili ,ukimwangalia mume wangu utamuona amevalia tisheti na jinsi, hata yeye mwenyewe mume wangu akijitazama ,anajiona amevaa tisheti na jinsi,nguo zake anazozipendaga.
Tukamaliza kula ,nami nilijiandaa ,nikabadili nguo Kisha tukatoka na kufunga mlango wetu, Safari ilikua ni kwenda hospitali kwenda kupima afya za vizazi vyetu.
Nikiwa na mume wangu kwa mguu tulitembea kwenda kwenye hospitali moja ya Aghakhan ,tulipofika tulionana na dokta . Tukajieleza Kisha dokta akachukua vipimo vyake ,tukasubili kwa nusu saa, dokta alitupati majibu kua ,wote sisi vizazi vyetu viko sawa Wala hakuna tatizo lolote la kutibika kibaolojia. Cha msingi ni kumwomba mungu zaidi maana yeye ndie anaye toa.
"Tunashukuru Sana dokta kwa majibu na ushahuri wako!"
"Asanteni karibuni Tena!"
"Tunashukuru dokta"
Baada ya hapo nikamchukua mke wangu Tukapanda bajaji tukarudi nyumbani. Nilipofika nyumbani nilikua sijielewi elewi kwa kweli nilikua nahisi Kama wenge ,sikutaka kwenda kokote pale ,niliwasha tv nikawa naangalia ,mpaka Usiku ukaingia .
Sijui Kama nilikula chakula Cha Usiku maana nilipokuja kushtuka nilikua tayari nipo kitandani chumbani nimelala. Pembeni alikua mke wangu nae amelala pia. Sikutaka kumwamsha maana na Mimi mwenyewe macho yalikua mazito ,ishara ya usingizi mzito ukininyemelea, sikua na ujanja nililala Kama fofofo!!
Mara nikajikuta nipo mtaani kwetu nyakati za usiku Sana ,huku nikikimbizwa na watu wa hajabu nisio wajua wameshika mapanga,wengine wameshika mikuki , wengine walibeba mawe makubwa lakini walipokua wananirushia Yale mawe yalikua yanakuja kwa spidi kubwa utadhani yalikua hayana uzito. Lakini yalinikosa kosa na kuangukia pembeni ,yalichimba ardhi Kama pango yalipotua chini.
Nililia Sanaπππ huku nikiendelea kulia na kuita kuomba msahada lakini hakuna alie nisikia hata kidogo mtaa mzima ulikua kimya . Mikuki ilinikosakosa nikazidi kukimbia ,jasho zilinivuja na nguvu ziliniishia kabisa ,nikaanguka chini ,huku wale watu na siraha zao tofauti wakiwa wanakuja taratibu,mmoja wao alinikaribia na akanioneshea ishara ya kunichinja shingo yangu na damu yangu kuinywe. Jamaa lile likanyanyua panga lake juu akijiandaa kuniua. Mwili wangu haukua na nguvu ,nikaita mpaka ni kachoka,mwishoni namwona lile lijamaa limejikinya kushusha panga lake kwa Kasi ili anikate shingo yangu,nilinena kwa kumwomba mungu wangu.. "Ee Mungu wangu uniokoe ,Kama hii ni ndoto ,unihamshe nitoke katika usingizi huu nikiwa salama,Mungu wangu niokoe"
Lile panga lilipokua linashuka ,na kukaribia kwenye shingo yangu nilipiga kelele kubwa mpaka nikashtuka usingizini!!!
Kumbe kulikua tayari kumeshakucha, mke wangu alishtuka nae kwa kelele nilizopiga .
Mwili wangu wote uliloa jasho ,mapigo ya moyo yalikua yanaenda mbio sana,.
"Vipi mme wangu Mbona hivyo" nilimuuliza mume wangu kwa unafki kwani nilikua najua vizuri Sana kilichomkuta.
Ndugu msomaji ndoto ni ujumbe mzuri Sana Kama utajua maana yake. Ndoto inaweza kukupa ujumbe mzito juu ya hadui anaye kufuatilia maisha yako.
Kwakua mume wangu Sadi,nilisha muweka kwenye tageti zangu ,hiyo ndoto aliyo iota ni ishara kwamba Kuna hadui mwenye Roho mbaya na lengo baya Sana katika maisha yake na hadui ameshaanza mashambulizi makali dhidi yake,hivyo anatakiwa kua makini, raha sivyo anaweza kupotea kwa kufa na kuchukuliwa Msukule.
"Mke wangu nimeota ndoto mbaya Sana ,mpaka moyoni nimekosa amani kabisa"
" Mme wangu hiyo ni ndoto tu Wala usiwe na wasiwasi,ngoja nikakuandalie maji ya kuoga utoe uchovu.
Nilienda kumwandalia maji mme wangu ,tulienda kuoga wote tukarudi ,nikaandaa chai tukanywa Kisha akaniaga kwenda kwenye mizunguuko yake ya kujitafutia ridhiki.
" Mke wangu tutaonana badae kidogo "
Nilimuaga mke wangu Kisha nikaondoka . lakini kiukweli moyoni nilikua na hofu Sana kutokana na ile ndoto ya Jana Usiku. Nikakumbuka kua nina namba ya mchungaji Nelson wa segelea. Nikampigia simu ,akasema kua yeye Yuko kanisani ila ,ingekua vizuri Mimi niende huko kuliko kuongea kwenye simu.
Nikapanda gari moja kwa moja segelea kanisani.
Ilikua ni siku ya juma tatu,mchungaji nilimwona akiwa anakagua ujenzi wa kanisa jipya.
" Karibu Sana Sadiki,twende ofisini kwa mazungumzo zaidi"
Tulienda ofisini na mchungaji Nelson.
"Karibu ndugu Sadiki,unaweza kuketi hapo, mmhmm! Bila Shaka nakumbuka nilikutana na wewe kule barabarani na nikakosakosa kukugonga na gari langu ,si ndio?"
"Bila Shaka mchungaji!"
"Sawa kabisa na ulinielezeaga tatizo lako na mkewe kuhusu uzazi vipi ! Uliishia wapi ?
" Tulienda hospital na mke wangu tulipima ,lakini Cha hajabu! Wote tukaonekana hatuna tatizo,Yani wote ni wazima,ila dokta ametushahuri tu tumwombe Mungu tu maana yeye ndie anae to.!!"
"Mh! Sawa ndugu sadii,Mungu pekee ndie anaye toa na ndie anaye twaa,umekuja sehemu sahihi tatizo lenu litakwisha "
"Amen mchungaji! Lakini ukiachana na hilo mchungaji, Kuna Jambo lingine linanitatiza Sana"
Nilimuelezea mchungaji kila kitu kuhusiana na ile ndoto na ile siku narudi nyumbani na kusikia mke wangu anaongea na mtu Kisha baadae baada ya kuingia ndani anasema alikua ni yeye tu na tv pekee.
" Sadiki upo kwenye hatari kubwa sana,tena ni hatari ya kufa,inaonekana Kuna hadui anakufuatilia,na ameshaanza kukushambulia, na hadui huyo hayupo mbali ,yupo ndani kwako."...................
Itaendelea...............
Je,Binti Chuma atafanikiwa kumtoa sadaka Sadiki?
Je,vipi maisha ya mzee Foya yanaendeleaje?
Je,Chuma ataweza kulipiza kisasi kwa mganga Alumbile Kalumba Alie muua Bibi yake?
Hayo na mengine mengi ya hajabu utayajua zaidi kwenye episode zijazo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni