Ijumaa, 8 Novemba 2024

URITHI wa Bibi 9

 Story........ URITHI WA BIBI EP.9

Mtunzi........ Steven Morgan


Contact.....+255659115223


Ilipoishia....👇


"Sawa karibu" nilimjibu yule kijana kwa urahisi kabisa bila usumbufu.

"Asante sana mrembo Chuma naomba nipe dakika 3 tu nikachukua vinywaji vyangu kule kwenye meza yangu nihamishie hapa."

"Sawa nenda." Nilimjibu. Sasa wakati anaenda kuchukua vinywaji vyake yule kijana ,Mimi Kuna kitu kikanishtua au naweza sema nilipata message ya kichawi,nikanyanyuka haraka na kwenda chumbani kuangalia vizuri huo ujumbe.............. ...............


Endelea 👇

Nikanyanyuka haraka kwenda chumbani kuangalia huo ujumbe vizuri.Nikaingia kwenye kile chumba nilicho Kodi, nikafungua begi langu kubwa na kutoa kioo changu ndipo nilipo mwona mkuu aliniambia kua ,kutakua na kikao Usiku huo kwa hiyo nisikose. Nikafanya maandalizi ya haraka kwaajili ya kikao .Kisha nikarudi pale baa kwenye kile chakula changu, muda ulikua umeshaenda kidogo ilikua ni saa4 Usiku. Nikamkuta yule kijana Sadi bado yupo pale kwenye meza yangu ananisubiri,huku akiwa anaendelea kula chakula chake taratibu.

"Chuma Mbona umenitoroka ghafla sijakukuta lakini nikajipa moyo nikahisi labda ulienda msalani (chooni). Vipi kwema lakini? Mbona unaonekana Kama haupo sawa?"

Sadi aliniuliza ,sijui alinionaje lakini nahisi nilikua tofauti kutokana na maandalizi ya kichawi niliyo yafanya. Hapa naomba niwape Siri moja ndugu wasomaji, uchawi siku zote huwa ni Kama vazi,hivyo nilipoenda kujiandaa maana yake nilisha vaa vazi la uchawi,na pale nilipokaa na Sadi,naweza kufanya chochote kile kinacho husiana na uchawi,na Kama ulisha wahi kumwangalia mtu usoni afu ukamwona Yuko tofauti kuliko siku zote ulivyo mzoea yaani anatisha sana na huwezi kumtazama mara mbilimbili ujue,huyo mtu sio wa kawaida kwa mda huo,lazima atakua amevaa kikoti Cha uchawi na amejiandaa na Jambo fulani hata Kama mchana kaa nae mbali.


Basi tuachane na hayo ,turudi pale mezani ,nikiwa bado nipo na yule kijana Sadi,nikawa naendelea kula chakula changu bila kuhofia chochote. Akili yangu haikua pale kabisa,hata Sadi alipokua akiniongelesha nilimwona Kama inzi anae nisumbua.

"Chuma sio Siri nimevumilia nimechoka ,wacha tu nikwambie ukweli,Mimi nahisi kukupenda kweli,na Kama utanihafiki ,nitakuoa tuishi Kama mke na mume!"

"Unajua Sadi unaniletea utani sana hapa!"

"Hapana Chuma Mimi nakupenda kweli na sio masihara!"

"Sasa wewe kijana Yani umeniona leo tu,alafu unaniambia unanipenda! Hivi unanijua vizuri kweli wewe?"

" Haijarishi Chuma ,kwa Sasa ninachokijua Mimi ni kukupenda wewe tu,suala la kukujua vizuri,nitakujua baadae."

" Sadi wacha kujifanya shujaa,endapo ukinijua hata kwa dakika moja huto tamani Tena kukaa karibu yangu"

"Mh! Wacha kunitisha Chuma wewe ni mrembo sana nitawezaje kukaa mbali nawe?"

"Sadi hivi kweli unaweza ukaishi na jini?"

"Kwanini unaniuliza hivyo Chuma! Inamaana wewe pia ni jini?"

"Ndio Sadi Mimi ni jini" nilimdanganya yule kijana ili asinizoee.

" Hahahaha! Wacha uongo Chuma jini hawezi kula vyakula Kama unavyo kula wewe ,labda utakua hunitaki tu , ila Mimi nakupenda tu hata Kama wewe ni jini"


"Sawa Sadi ila ni vyema ukakaa mbali nami ili nisije nikakudhuru."

 "Chuma naomba nikuachie namba yangu ya simu ili siku nyingine ukipenda unitafute tuongee zaidi"

" Sadi Sina haja ya namba zako kwa sababu hata hiyo simu yenyewe Sina"

"Chuma sikia hapa Nina simu mbili chukua hi simu moja Kuna laini yangu humo ya Vodacom pia Kuna namba yangu humo imeandikwa jina la Sadi,nafikiri tutawasiliana Chuma"


"Asante Sadi ila kwa Sasa naomba uniache mwenyewe nitakupigia kesho sawa?"

" Sawa Chuma Basi nikutakie Usiku mwema mpendwa."

"Nawe pia Sadi "


Tuliagana na Sadi Kisha akaondoka na kuniacha Mimi mwenyewe pale mezani.

Nikalipa bili ya chakula Kisha nikarudi ndani kwenye chumba changu. Kwakua muda ulikua umeshaenda ,nikatoka nje ya ile gesti kichawi Kisha Kuna ndege ilinipitia palepale tukaondoka kwenye kikao. Kikao kilifanyika mlandizi ,tulipofika tukashuka tukiwa wengi sana Kama vile tulikua tumepanda Basi la mwendo Kasi. Kila mtu akakaa kwenye siti yake kasoro Mimi tu ndio nilikosa siti.

Ndugu msomaji ninaposema nimekosa siti simaanishi siti unayoijua wewe Kama stuli,kigoda au Kochi. Bali siti zetu sisi huwa ni watu harisi ndio huwa tuna wakalia Kama siti, Kama ulishawahi kulala Usiku na uka amka asubuhi ukiwa umechoka sana na mwili unauma  baadhi ya sehemu,ujue ulibebwa Usiku na mchawi na ulienda kutumika Kama siti.


Basi ,baada ya Mimi kukosa siti ,nikaamua na Mimi kutafuta siti yangu.Nikatumia maneno ya mamraka yasio pingika,labda Mungu pekee ndio wa kuzuia. Nikamwita yule kijana Sadi kwa mamraka ya kichawi.

Hapa naomba nielezee kidogo ,ndugu msomaji . Kama ulishawahi kusikia sauti ikikuita kwa jina lako haswa  nyakati za Usiku alafu ukashtuka usingizini na kuitika kwa sauti,bila kujua anaye kuita ni nani! Wakati mwingine unaweza ukatoka nje kuangalia anayekuita usimwone yeyote. Ujue kua hiyo ni sauti ya mamraka ya kichawi inayokuita kwa dharula ili ukatumike na sio kurogwa. Sasa unapo ona hari hiyo inakupasa ukemee kwa jina la Mungu baba na  Yesu kristu ili kujinusuru katika janga hilo la kutumika.


Basi turudi pale kwenye kikao mlandizi,niliendelea kumwita yule kijana Sadi kwa majina yake mawili ,japo jina lake la pili sikulijua nilitumia jina la Adamu Kama ndo jina la baba yake ,kwa hiyo nilimwita "Sadiki Adamu njooooo", "Sadiki Adamu njooooo" x3 .

Nilirudia rudia kumwita kwa jina hilo mara tatu.  Huwezi amini ila ndivyo ilivyo kua ,yule kijana akatokea palepale nilipo huku akiwa amepiga goti. Nika muinamisha akawa anatembea kwa mikono na miguu, nilipofika sehemu niliyo itaka nikamkaria mgongoni Kama farasi ,nikatulia huku nikisikiliza kinacho endelea.

 "Karibuni wageni waarikwa wote , karibuni kamati maarumu za mapishi kwa ajiri ya kikao chetu leo. Kwanza kabisa nitoe pole kwa wale wote walio ondokewa na wapendwa wao akiwemo Bibi Mbokeleni au Bibi Chuma. Tuna mkumbuka sana kwa MCHANGO wake mkubwa katika kushirikiana kimataifa haswa katika nchi za umoja wa afrika alishawahi kua katibu mkuu . Saramu za pole na rambirambi tulizielekezea kwa mjukuu wake Chuma, nafikiri wengi mnamjua,na wale msio mjua Basi Leo mtamwona. Chuma popote ulipo simama juu uwasalimie wageni wenzako.""


Mkuu aliamuru nisimame juu  niwasalimie wenzangu,nilisimama juu Kisha nikalia Kama paka mwenye jazba,Kisha wageni wote waarikwa nao pia wakashangilia kwa sauti mbalimbali, wengine walilia Kama mbwa,Simba,bundi,dudumizi ,na wengine walilia kwa sauti nyingi za hajabu usio weza kuzifananisha na kiumbe chochote.

Baada ya happy nikakaa kwenye siti yangu,na mkuu aliendelea.


"Asanteni sana ndugu zangu. Baada ya kusalimiana ,napenda kutangaza kua Chuma ana vita Kari ya kisasi dhidi ya mzee Foya na familia yake pamoja na mganga mmoja hatari Sana anaitwa  Alumbile Kalumba,anaishi huko mgeta vijijini. Lakini kazi hiyo ya kisasi tayari Kuna mwana mama toka Kenya atamsaidia Chuma katika kazi hiyo.

Tuachane na hayo ,wacha nizungumze mada muhimu ya leo. Leo nime waita hapa kuwakumbusha Jambo kubwa la muhimu Sana.Ndugu zangu huu mwaka ni mwaka wa kutoa sadaka kwa hiyo ,wote wenye zamu yao ,wajiandae na wale ambao hawajaoa au kuolewa ,wajitahidi mwaka huu watafute wachumba ili tupate sadaka katika uzao wao na Kama hamtazaa Basi mtawatoa kafara wapendwa wenu. Nadhani tume elewana!! Huu ndio ujumbe mkubwa wa leo. Tukiwa tunasubiria kamati ya chakula kutuandalia msosi,kamati ya burudani ijiandae kutuburudisha.Asanteni."


 Basi baada ya mkuu kumaliza kuongea ,vikundi mbalimbali vya burudani  vilianza kutoa burudani,tulicheza Sana ngoma . Ninaposema tulicheza ngoma,sio hizi ngoma mnazo zijua,ngoma tulizokua zinapigwa ni wale watu tulio wafanya viti,ndio walichukuliwa pia kupigwa na kutoa mlio wa ngoma harisi ,nilimuonea huruma Sana yule kijana Sadi ,kwani mtu Alie mchukua alikua akimpiga kichwani huku amemkalia mgongoni. Hapakua na namna tulicheza Sana ,baadae ngoma zikanyamaza ,tukachukua siti zetu tukaketi,msosi ulikua tayari tulipewa msosi wa minyama minyama ya hajabu, nafikiri ni nyama ya mtu na si mnyama maana wengine walipewa mpaka viganja na visigino ambavyo vilionekana kabisa ni vya mwanadamu. Tulikula  na kunywa vinywaji vya damu nzito za watu.

Mwishoni mkuu akasimama na kufunga kikao Kisha akasema "kila mtu ahakikishe anakirudisha kiti chake msije mkasahau"


Basi kila mtu akatoa maneno ya mamraka kurudisha kiti chake ,nami pia nikachukua Sadi wangu na kumuamuru arudi nyumbani. Akatoweka  nami nikaenda kupanda ile ndege kubwa ya abilia ,ikaondoka kwa kuvuma Kama ngumbeo. Ilipofika tabata maeneo fulani nilishuka nikapotea kichawi na kuibukia ndani ya chumba changu pale gesti. Nilikua uchi wa mnyama kabisa ,na ilikua ni saa kumi na nusu usiku,kwakua. Choo na bafu kipo humohumo chumbani sikupata shida ,nilioga Kisha nikalala .


Nilikuja kushtushwa na mlio mkubwa wa simu ,ni ile simu aliyo nihonga  yule Kijana  Sadi. Nilipotazama simu ,niliona jina la Sadi ndio aliye kua anapiga. Nikapokea..

"Halooo Sadi" 

"Halooo mpenzi Chuma"

"Ukome wewwkijana ,huo upenzi na wewe umeanza lini?"

"Jamani Mbona unakua mkari hivyo Chuma!! Ok sawa Kama hutaki mimi niwe mpenzi wako ,Basi nitakua  rafiki yako tu inatosha. 

"Sawa nambie ulikua unasemaji ?"

" Chuma ,mwenzio nimeamka asubuhi hi,sijielewi kabisa,yaani kichwa kinaniuma Sana,na mgongo pia unauma sana, sijui tatizo nini Chuma ,hata kunyanyuka siwezi."

 

Sadi aliongea hivyo kunieleza Mimi lakini Mimi nilijua ni nini haswa kinacho msumbua . Hari hiyo kiukweli haiitaji miti shamba unaweza ukatumike tu dawa zozote za maumivu na ukapona.Kiukweli nilimuonea Sana huruma Sadi na nilishaanza kumpenda kweli japo sikutaka ajue Kama nampenda.


"Kwa hiyo Sadi nikusaidieje?"

"Naomba uje unichukue unipeleke hospitality,kichwa kinaniuma Sana."

"Hapana Sadi ,wacha tu nikununulie dawa za maumivu ,Kisha unielekeze unapokaa nikuletee ,sawa?

"Nitashukuru Sana Chuma rafiki yangu ,njoo huku buguruni ,ulizia kwa mangi dalari ,ukifika, ulizia kua chumba Cha Sadi au Sadiki Kiko wapi? Wakikuonesha we ingia tu ndani moja kwa moja maana mlango uko wazi."

 "Sawa Sadi nakuja muda si mrefu"


Nikajiandaa kwa kuvaa nguo zangu za kawaida na nika angalia muda , tayari ilishafika saa tatu asubuhi. Nikafunga mlango wangu ,funguo nikaenda kuiacha pale kaunta.kisha nikaondoka ,nilinunua dawa kadhaa za maumivu na matunda Kama ndizi machungwa pia nikanunua mboga Kama mchicha ,nyama na mazaga zaga  mengine kibao.

 Nikafuata maelekezo yake niliulizia chumba chake ,nilioneshwa nikaingia ndani maana mlango ulikua wazi .


"Karibu sana Chuma ,siamini Kama umekuja kuniona Chuma! Ukizingatia tumeonana Jana tu!"

 "Usijari Sadi,hebu jitahidini unyanyuke unywe hizi dawa za maumivu."

  Sadi alijitahidi kunyanyuka lakini alishindwa. Nika amua kumnyanyua kinguvu ,alilalamika Sana kwa maumivu. Nikampa dawa akanywa ,nikampa na ndizi za kuiva akala,nikammenyea na machungwa akala pia.

Nikawaambia Sasa pumzika wakati Mimi nakuandalia chakula Cha baadae .


"Nashukuru sana rafiki yangu"

"Sawa usijari,je ,vyombo viko wapi nimekuja na msosi inabidi nipike !"

"Duh! Asante,vyombo vyote angalia hapo  kabatini jiko hilo hapo mezani la gesi."

"Sawa Sadi wewe pumzika tu utakua sawa tu muda si mrefu."

Niliendelea kuandaa mboga Kisha nikaivisha wali,muda huo nilimuonea Sadi akinyanyuka mwenyewe kitandani na kujinyoosha viongo vyake vya mwili.

"Duh! Chuma ,nimepona rafiki yangu Chuma ,wacha nikaoge kwanzanitoe uchovu"

" Mi si nilikwambia kua muda si mrefu utakua sawa! Sasa Nenda kaoge alafu uje tule. "

" Sawa Chuma dakika tano tu ntakua nimeshamaliza.Asante Sana."

 Sadi alienda kuoga ,nami nikaandaa chakula mezani tayari kwa kuliwa. Wakati nipo pale chumabani kwa Sadi mara , akatokea yule Mama wa Kenya kichawi,akiwa uchi wa mnyama ,akaniambia kua natakiwa kujenga mahusiano na huyu kijana Sadi ili nimuandae mapema kwaajili ya kuja kumtoa sadaka Kama alivyo sema mkuu kwenye kikao. Nikasema kua ni sawa Ila huyu kijana Mimi nimesha anza kumpenda kweli Sasa nitawezaje kweli kumuua? 

"Utaweza tu Chuma we jitahidini tu uishi nae  ,na. Uzae nae mtoto mmoja Kisha ,ndio unamtoa sadaka ."

" Sawa mama nimekuelewa"

Yule mama akapotea ghafla,! Mara Sadi nae muda uleule akaingia. 

Tukala chakula Kisha tukawa tunaongea mambo mbalimbali yakiwemo ya kufahamiana zaidi.


" Sadi nikikupa nafasi ya kuchagua ,kua Mimi niwe ,rafiki yako tu,au ndugu yako ,au Dada yako,au jirani yako! Au mpenzi wako! Je,wewe utachagua nafasi ipi kati ya hizo?"

"Duh ! Kwa kweli kabisa kutoka moyoni ,Mimi nitachagua uwe mpenzi wangu wa pekee! "

"Basi karibu moyoni mwangu Sadi,nimeamua kukukabidhi moyo wangu mwepesi Kama karatasi, tafadhari usije ukanisariti Sadi."

" Chuma wacha kunitania bana ! Hivi ni wewe unae ongea hivyo au!"

"Sadi sijachanganyikiwa naongea nikiwa namaanisha au hunipendi, Kama hutaki Basi wacha niondoke!"

"Hapana Chuma ,unajua siamini kabisa lakini Kama unaniaminisha hivyo! Basi na Mimi nasema kua , nakupenda kweli na ikiwezekana hata leo amisha mizigo yako hapa tuanze maisha yetu.

    

Sadi bila kujua kua anamkaribisha shetani ndani,na pia ana mkaribisha ezraeli mtoa raho yake,ana amua kumchukua Chuma na kwenda nae mpaka kule gesti alipo panga,atamsaidia kubeba mizigo yake ,na Chuma Sasa  rasmi ameamia kwa Sadi Kama kuishi Kama mke na mume huku Chuma akiwa na  mipango yake ya maangamizi........................


Itaendelea..............

Je, Chuma atafanikiwa mipango yake ya kumtoa kafara Sadi? ,Je Chuma ataweza kulipa kisasi kwa mzee foya na yule mganga wa mgeta Alumbile Kalumba? Kwa uweza wa Mungu tutakutana Tena katika episode ya 10 ya  URITHI WA BIBI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

URITHI wa Bibi 15

 Story... URITHI WA BIBI EP.15. Mwisho. Mtunzi....Steven Morgan 📲......... 0659115223 Naam kwa Mara nyingine tena ndugu msomaji tumekutana ...