Story............ URITHI WA BIBI EP. 8
Author............Steven Morgan.
Contact........... 0764655342,+255659115223.
Naaam,ndugu zangu wasomaji kwa mara nyingine tena kwa uweza wake mungu baba tumekutana Tena tukiwa na afya njema kabisa katika hii chemba yetu ya story zenye maarifa na mafunzo yenye maonyo. Poleni sana ninyi ambao afya zenu zimetetereka kwa namna moja au nyingine kutokana na maradhi mbalimbali ya mwanadamu. Zaidi tuendelee kumwomba Mungu zaidi maana yeye ndie anaye ponya.
Bila kuwachosha, wacha tuendelee na story yetu ya URITHI WA BIBI EP. 8
Kama kawaida , TULIPOISHIA ndipo tunapo ANZIA Ili twende sawa bila kupinda pinda.
TULIPOISHIA.👇
"Eheee ni kweli alafu nilitaka kukuuliza tangia mwanzao kua Chuma Yuko wapi? Na aliye kufa huko ni nani?"
" Mme wangu Chuma aliniaga kua anakwenda kumsalimia Bibi yake huko Kijiji Cha pili lakini inasemekana ,alipofika huko, alimkuta Bibi yake amefariki na haijulikani kilicho sababisha kifo Cha Bibi Chuma."
"Duuuh! Mke wangu,tunavita kubwa na tusipo kua makini tunaweza tukaangamia mmoja mmoja maana Bibi yake chuma ndio alikua hadui yetu namba moja ,na mganga aliniambia kua hadui namba mbili tunaishi nae nyumba moja,bila Shaka atakua ni Chuma!! Chuma ama zako ama zangu na kuanzia Sasa simtaki Tena Chuma katika familia yangu"
Mzee Foya aliongea kwa uchungu huku akimsisitizia mke wake kua Chuma hamtaki tena maana ni hadui yao mkubwa sana hawatakiwi kuishi nae nyumba moja....
Kesho yake ikafika mazishi yakafanyika pande zote mbili watu walilala matanga kisha tarehe za kupanda msalaba zilitajwa pande zote mbili ,kule kwa Chuma msalaba utakua 15/08/20..
Na kule kwa bibi zubeda ni 14/08/20..
Shughuli za mazishi kwa ujumla zilikwisha.
Basi baada ya mazishi kuisha ,mzee foya na familia yake walirudi kwao dar es salaam. Huku Chuma akiwa amebakia nyumbani kwa bibi yake. Siku kadhaa zilipita ,siku moja Chuma akiwa nje ya nyumba yao, nyakati za asubuhi,alitembelewa na ugeni wa ghafla! Yaani ugeni wa kufumba na kufumbua.
"Ahaaha haaa! Usiogope Chuma ,ni Mimi ,unanikumbuka?" " Hapana Mama kwani wewe ni nani?" Alijibu Chuma.
" Chuma mara hii umenisahau? Basi ngoja nikukumbushe! Mimi ni yule Mama nilie kusaidiaga kule Kenya ,kipindi kileeee! Ulipokua unafundishwa uchawi na marehemu Bibi yako,na mara ya mwisho mlipata matatizo nilikusaidiaga na nilikurudisha hadi huku kwenu Tanzania nyumbani kwa Bibi yako.vipi,Bado hujanikumbuka tu Chuma?"
Ahaaa! Nimesha kukumbuka mama ,karibu sana. " Asante sana "
Nilimkaribisha yule Mama mkenya kwani nilimkumbuka vizuri sana,aliwahi kunisaidia sana. Alikuja asubuhi sana kwa njia za kichawi.
"Chuma pole sana kwa msiba ,na nimekuja huku baada ya kupata ripoti siku chache zilizo pita kwenye kikao kikuu Cha wakurugenzi wa umoja wa Africa,moja kati ya ajenda zilizo zungumzwa ni pamoja na rambirambi ya msiba wa Bibi yako.wakuu wote wanakupa pole na wamenichagua Mimi ili nikusaidie kulipa kisasi kwa wahusika wote akiwemo mzee Foya na familia yake na yule mganga wa mgeta Alumbile Kalumba.leo nimekuletea pesa hizi taslimu milioni mbili na laki nane Kama pole ,kwa niaba ya wanachama wote wa ndani na nje ya nchi za Africa. Bibi yako hakua mchawi mdogo alikua ni mchawi mkubwa sana na mchango wake unajulikana katika nchi zote za umoja wa Africa."
Asante sana mama yangu ,kwa upendo wenu kwangu,nafurahi Kama utakua pamoja nami katika kulipa hiki kisasi.
"Usijari Chuma tupo pamoja,ila Kuna Jambo nilisahau kukwambia kua ,wakuu wamesema kua ,hakuna kufanya msalaba au arobaini. Unachotakiwa Sasa kuendelea na maisha yako Kama kawaida kuongeza juhudi katika kuhudhuria vikao vya kichawi na kuchawia ,hii itakusaidia kujiongezea nguvu zaidi. Pia uki hitaji msaada wowote kwangu, niite kichawi muda wowote nitakuja kukupa msahada."
Sawa mama ,nimekuelewa nashukuru sana kwa maelezo yako .Nami Nita yafanyia kazi zaidi yote uliyo nieleza.
Basi baada ya kumalizana na yule mgeni wangu akatoweka ghafla katika uono wa macho yangu ,Yani aliondoka kichawi.
Siku hiyo nilikaa nyumbani siku nzima nikiwa peke yangu ,nilifikilia mengi sana,ilamwishoni nikapata wazo la kuhama pale kijijini ! Ukizingatia pale kijijini Sina ndugu wa karibu ninae elewana nae. Kwakua nilikua na pesa za kutosha,sikutaka kupoteza muda ,niliandaa mizigo yangu ,nilikuwa na mabegi mawili yenye kila kitu kilicho nifaa.
Ilipofika jioni niliondoka na kuelekea Msamvu stendi ya mabasi ili niende zangu dar es salaam. Huko dar Sina ndugu Wala sijui nitafikia kwa nani! Maana bosi wangu najua amesha kua hadui yangu . Kwakua nilikua na pesa,sikua na wasi wasi .
Nilipata Basi la Abood na Safari ilianza na hatimae saa mbili Usiku nilifika ubungo. Sikua na sehemu ya kwenda bali nilitafuta nyumba ya wageni ili nipate kulala kwa Usiku huo. Nilipata chumba katika gesti moja ya maeneo Fulani pale tabata. Nililipia Kisha wakanipa funguo nikaenda ndani ili kuweka mizigo yangu. Nikaweka mizigo Kisha nikaingia kuoga na kubadiri nguo Kisha,nikatoka gesti nikaingia pale baa ambapo niliona watu wakila chakula na kunywa. Namimi nilichagua kukaa kwenye meza isio kua na mteja yeyote ,nika agiza chips mayai na nusu ya kuku wa kukaanga na maji Safi ya lita moja na nusu ya Kilimanjaro.
Nikawa naendelea kula taratibu huku nikisikiliza mziki wa kizamani uliokua ukipigwa pale kaunta. Mara nikaona Kuna kijana mmoja alikua akinikonyeza na kunipa ishara za kuniita. Siku mjibu chochote lakini yeye mwishoni aka amua kuja hadi kwenye meza niliyo kaa,akachukua kiti akasogeza karibu yangu,Kisha akawa ananihojihoji.
" Binti mrembo unaitwa nani?"
"Chuma"
"Chuma jina zuri sana,Mimi naitwa Sadi au wengine wanapenda kurefusha jina langu na kuniita Sadiki. Ok, Chuma naona hapa upo mwenyewe nami nilikaa kule mwenyewe,nikaona sio mbaya nije hapa nikuombe kampani yako ili tufurahi wote pamoja tukiwa meza moja."
"Sawa karibu" nilimjibu yule kijana kwa urahisi kabisa bila usumbufu.
"Asante sana mrembo Chuma naomba nipe dakika 3 tu nikachukua vinywaji vyangu kule kwenye meza yangu nihamishie hapa."
"Sawa nenda." Nilimjibu. Sasa wakati anaenda kuchukua vinywaji vyake yule kijana ,Mimi Kuna kitu kikanishtua au naweza sema nilipata message ya kichawi,nikanyanyuka haraka na kwenda chumbani kuangalia vizuri huo ujumbe.............. ...............Itaendelea
Samahani kwa kuwaletea story fupi,hii ni kutokana na sababu zisizo zuhirika.🙏
Je ,huo ujumbe ni upi? Je,yule kijana nae kitamkuta nini?
Mambo ni mengi muda mchache, Fuatilia sehemu ya 9 kesho .kizaa zaa kimeanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni